Baba_Enock
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 7,076
- 2,445
Kinachonishangaza Tanzania ni jinsi usalama unavyoratibiwa. Ukisema hakuna usalama sikubaliani na hili kwani viongozi na watu maarufu usalama wao haujawahi kuwa wa mashaka kabisa.........
siku tatu jamaa anakula bata tu na akaondoka na point tatu muhimu? Hii ni hatari, hivi hawa wanaojifanya sijui intelijensia pindi tu kunapokuwa na mkusanyiko wa cdm wapo wapi? Binafsi na mpongeza huyu jama! Huyu na mfananisha na michael scoff au matt damon!! Ningependa ajitokeze tu hata kupitia jf atujuze namna alivyo waingiza shule hao wanyarwanda wa tz na vilaza wao usalama wa ccm.
Wacha nakubaliana nawe, nakubaliana nawe katika hilo, nchi hii ni nchi ya watu wa kitu kidogo, fikra rojo na mtizamo takataka... hakuna anaeogopa kufanya uhalifu kwakua toka juu mpaka chini mfumo umeoza kabisa.Mwanakijiji usishangae sana kama tunakuwa na rais mwizi unategemea huko chini watafanya nini kama sio kuendeleza umburukenge.
Mafisadi wanalindwa, walikuja na ngonjera mpya ya magamba sasa sijui wataleta mpya ipi? Ngoja kwanza wajilipe na hii Dowans mpya inayokuja kwa njia za kiubabaishaji.
Ila.. huyo nadhani kaamua kwenda mbele zaidi tu ya wengine; maana wapo wengi mijini wanaojipitisha kama "Msaidizi wa rais".. nimesoma habari moja (iliripotiwa hapa) jamaa aliyejifanya ni Askofu Malasusa akijaribu kumtapeli Meya wa Ilala sijui! Nadhani watu wameshajua namna ya kutapeli kwa kutumia madaraka maana wanajua watu wanaogopa wenye mamlaka. Ndio maana miye mwenzenu nawapuuzia sana watu wenye kujiona wana madaraka fulani! Kwamba wanafikiri kwa sababu yamadaraka yao wanaweza kukufanya uinamishe kichwa ukainama, ubong'oe na ukabong'oa.
Hapo kuna tatizo katika Halmashauri yote kwa ujumla, mtu anajitambulisha kwa mdomo kisha wanampokea na kufanya kazi kubwa hivyo tena siku 3! No kukagua kitambulisho, no mawasiliano anakotoka!!!!! agrrrrrrrrrrrrrrrr, ni aibu hata kuisoma hii aise
kazi kweli kweli wamekutana matapeli wote
mwenyekiti huyo amedai baada ya halmashauri kufanya mawasiliano na wizara iligunduika kuwa hakuna kiongozi yeyote aliyetumwa huko na hakuna rekodi zozote za jina linalohusiana na mtu huyo. Kwa mujibu wa shimilimana dk ilongo mlawa baadaye alikamatwa juzi na kuwa anashikiliwa na polisi kwa mahojiano na kamanda wa polisi mkoa wa kagera henry salewi alipopigiwa simu kuhusu tukio hilo aliomba apewe muda kwa maelezo kuwa alikuwa anaendesha kikao.