Kituko Ngara: Daktari "Feki" afanya ziara, apewa ulinzi na polisi; agharimiwa - kwa siku Tatu!

Huree!!!!!!!, ina maana the so called information age haijafika Tanzania? Au ndiyo yale mambo ya kuogopa wakubwa!! Ila hii ni kali.....
 
Huree!!!!!!!, ina maana the so called information age haijafika Tanzania? Au ndiyo yale mambo ya kuogopa wakubwa!! Ila hii ni kali.....


yaani kuna vitu vingine lazima uamini tu kuwa "vinawezekana Tanzania tu".. ila ningependa kuiona hata picha yake jamaa lazima atakuwa amekaa "kibosi bosi tu".. unaijua ukisoma hii habari pole pole unaweza kujikuta unashangazwa na uwezo wa watu wetu wengine kuhoji au namna ya kutafuta majibu.
 
Najaribu kufikiria gia ya namna gani mtuanaweza kuitumjia kuingilia pale Ikulu halafu akawa Kibosile mmoja hivi wa Ikulu. Ila huyu kakamatwa tu kwani wapo wengine wanaojiita "maafisa wa Usalama" wanapita na kutengeneza deals kila kukicha.

Tafuta kitambi, weka suti na tai halafu jitambulishe, hakuna anayekuuliza kitambulisho wala barua ya utambulisho! Bado tuna matatizo ya kutojiamini mbele ya watu wanaoonekana "smart"
 
Akili kukichwa ukichelewa umeliwa,huyo jamaa nimemkubali sbb siku tatu sio mchezo yaani Tanzania bila wizi(UFISADI)haiwezekani jamani
 
Yaani jamaa asingeamua kwenda kuangalia hizo surgeries angewza kabisa kufanya ziara zake hadi anaondoka huku anashangiliwa na kuimbiwa na kikundi cha ngoma.
 
Siku tatu jamaa anakula bata tu na akaondoka na point tatu muhimu? Hii ni hatari, hivi hawa wanaojifanya sijui intelijensia pindi tu kunapokuwa na mkusanyiko wa cdm wapo wapi? Binafsi na mpongeza huyu jama! Huyu na mfananisha na Michael Scoff au Matt Damon!! Ningependa ajitokeze tu hata kupitia jf atujuze namna alivyo waingiza shule hao wanyarwanda wa tz na vilaza wao usalama wa ccm.
 
I really Love this guy!!
Aidha mwenyekiti huyo alilalamika kuwa alilazimika kuwaita madiwani siku ya Jumamosi ili wakutane na kiongozi huyo,ambaye alitoa maelekezo ya kutaka watumishi wa idara ya afya kulipwa stahili zao haraka baada ya kupokea malalamiko ya kutolipwa kila alipopita.
 
yaani kuna vitu vingine lazima uamini tu kuwa "vinawezekana Tanzania tu".. ila ningependa kuiona hata picha yake jamaa lazima atakuwa amekaa "kibosi bosi tu".. unaijua ukisoma hii habari pole pole unaweza kujikuta unashangazwa na uwezo wa watu wetu wengine kuhoji au namna ya kutafuta majibu.

Mkuu MMK,
hayo ndiyo yalibumburuka.... kwa ninavyoamini mimi,na upuuzi unaoendelea kwa idara za serikali, JAMAA ATAKUWA AMERAMBA RUSHWA KIBAO..KWA KUWATISHIA WAZEMBE KUWATIMUA KAZI....nampa big-up huyo JEMADARI...
 
yaani kuna vitu vingine lazima uamini tu kuwa "vinawezekana Tanzania tu".. ila ningependa kuiona hata picha yake jamaa lazima atakuwa amekaa "kibosi bosi tu".. unaijua ukisoma hii habari pole pole unaweza kujikuta unashangazwa na uwezo wa watu wetu wengine kuhoji au namna ya kutafuta majibu.

In the big picture utagundua kwamba hakuna anayeweza kuthubutu kuhoji wala kumkosoa kiongozi wa juu yake sembuse JK, ndiyo utamaduni wa chama na serikali ya bongo. Maana hawa viongozi wa hizi halmashauri ndiyo wanakutana face to face na wananchi of which wanatakiwa wawe wanamwambia mkulu namna gani mabo yanaenda alijojo akiwatembelea huko. Sasa kama wahusika wenyewe ndiyo hawa thubutuuuuu!
 
Mi nadhani huyo m/kiti na mkurugenzi wa halmashauri wanatakiwa wakamatwe mara moja na kushtakiwa kwa kosa la uzembe ulioisababishia hasara halmashauri yao! Kwanini wamgharamie huyo jamaa hata kama kweli ni ofisa kutoka wizarani? Inamaana hawajui kuwa mtumishi analipwa na ofisi yake kuanzia malazi, posho ya safari, na marupurupu yote anapotumwa nje ya ofisi? Huu ni uzembe tu. Au ni rushwa wanampa ili awachunie baadhi ya mambo! This must end now!
 
Mwanakijiji usishangae sana kama tunakuwa na rais mwizi unategemea huko chini watafanya nini kama sio kuendeleza umburukenge.

Mafisadi wanalindwa, walikuja na ngonjera mpya ya magamba sasa sijui wataleta mpya ipi? Ngoja kwanza wajilipe na hii Dowans mpya inayokuja kwa njia za kiubabaishaji.

Tanzania Tanzania,
Nchi yenye mali nyingi,
Watu wengi wa Ulaya, wanaililia sana,
Nimeona ndege wengi, chiriku katia fora,
Kanipendeza mlio, kama mtoto wa nyumbani.

Kiapooo...mimi ni chipukizi wa......nitatumikia chama changu cha....saa yoyoteeee.....muda wowoteeeeee.......na mahali popote patakapoamuriwa.......lol
 
yaani kuna vitu vingine lazima uamini tu kuwa "vinawezekana Tanzania tu".. ila ningependa kuiona hata picha yake jamaa lazima atakuwa amekaa "kibosi bosi tu".. unaijua ukisoma hii habari pole pole unaweza kujikuta unashangazwa na uwezo wa watu wetu wengine kuhoji au namna ya kutafuta majibu.

Hii inatoa picha jinsi watendaji serikalini wanavyoogopa maboss hadi kuwa very subjective katika utendaji wao. Watu wanatumia zaidi macho, mikono, miguu na mdomo katika utendaji badala ya brain ambayo imetengenezwa kitaaluma katika kutenda. Hii hofu haiishii hapa ndiyo maana tunaona mambo mengi yanapitishwa hata bila kufanyiwa critical analysis kwani watu hawasomi content wanasoma authority ya mwanzilishi wa hilo jambo.

Kukosoana Tanzania haitegemei sana taaluma bali mwonekano wa mtu na pia nafasi na influence yake katika serikali. Hii pia inaendelea hadi kwenye maswala ya ajira kiasi kwamba wanapo ajiri hawaangalii uwezo bali association ya mhusika na viongozi wa ngazi za juu. hukumu pia kwenye sheria inaenda hivyo hivyo huku ikikaziwa na rushwa ya pesa na authority. Kweli hakuna order wala chain of comand bali ni shagala bagala kila mtu anafanya kwa kadiri ya nguvu zake na wenye nguvu ndiyo washindi. Hata ujima haukuwa hivi sisi ni zaidi ya babu zetu wakati wa ujima.
 
Kwangu mimi huyu jamaa ni hero ambaye alistahili kabisa kuwa usalama wa taifa maana amethubutu na amewaonyesha ccm na vibaraka wake how poor they are in adminstration skills.tukiwa na watu wenye akili za huyu jamaa kama elfu kumi ivi wananchi watapata clear dermacation ya kuifuta ccm madarakani na hiyo ndo real intelijensia siyo hii ya polisi wetu vilaza wanayoitumia.big up dr.fake na ulistahili udaktari wa heshima kama aliopewa mkulu.kumbe ufisadi hata kwa watu wa chini inawezekana?nashawishika tanzania bila ufisadi haiwezekani.
 
Namushukuru sana huyo jamaa.kafanya kazi ya kujitolea.je mtu ukijitolea ni kosa?Ngara inaonekana hawa madoctor hawaendi kukagua.huyo ni doctor jamii.naona kaenda rulenge tu,akitokea mwingine wa kujitolea ajitahidi kufika hata sehemu za Mugoma,kabanga,kasulu,rusumo na benaco.coz hawa madoctor wa kikwete hawajui kazi wamekalia majungu tu maofisini.big up dr wa ukweli.
 
I liked the guy. Alikuta kituo cha afya sub standard kakifunga. He deserve to be a leader. Ameona kuna ombwe ndiyo kaamua kulijaza. Kama kuna data watuambie mara ya mwisho mtumishi kutoka wizara ya afya amefika lini Ngara? Kama viongozi hawatoki ofisini kwenda kwa wananchi vyote hivi vitatokea. Hii ni kashfa kwa wizara ya Afya kuwa haipo karibu na wananchi na ni somo zuri kwa Waziri Haji Mponda na Katibu mkuu wake Bi. Nyoni.
 
Siku tatu jamaa anakula bata tu na akaondoka na point tatu muhimu? Hii ni hatari, hivi hawa wanaojifanya sijui intelijensia pindi tu kunapokuwa na mkusanyiko wa cdm wapo wapi? Binafsi na mpongeza huyu jama! Huyu na mfananisha na Michael Scoff au Matt Damon!! Ningependa ajitokeze tu hata kupitia jf atujuze namna alivyo waingiza shule hao wanyarwanda wa tz na vilaza wao usalama wa ccm.

Kinachonishangaza Tanzania ni jinsi usalama unavyoratibiwa. Ukisema hakuna usalama sikubaliani na hili kwani viongozi na watu maarufu usalama wao haujawahi kuwa wa mashaka kabisa na hii pekee inaonyesha ni jinsi gani kulivyo na efficient system ya usalama na iwapo uta atempt kufanya tendo hatarishi kwa group fulani la watu utakamatwa kabla ya kunyanyua hata tambo chache kuelekea kutekeleza azma yako. swali langu ni kuwa inakuaje mambo yanayohusu commoners huo usalama unakuwa kama vile umesafiri? Inamaana katika scrutiny ya information zinazochukuliwa na hao wenzetu ya mambo ya raia yana kuwa droped na viongozi hawapewi briefing? Mimi sijawahi kufanya wala kuwa trained in issues of security ila common sense yangu inaniambia in the field information haiko field specific na wala haitoki in isolation bali iko in a mixed manner kiasi mhusika lazima upate hiyo mix na kila moja lazima uipe umuhimu wake hapo sasa kwanini vitu ambavyo vilitakiwa kujulikana hasa kwa upande wa raia kabla havijatokea huwa inakuwa kama the guys are not informed ila inapokuja kwenye usalama wa individuals hasa wenye authority vinatunguliwa kabla havija tokea?

Natamani ni fanye research ya aina fulani hivi ni initiate move za hatari hivi zenye mchanganyiko wa issues za raia na viongozi nione how long will it take hao kunidaka na ikitokea wakani daka basi angalau ni jue wamenidaka kwa issue ipi specific and why? Nahiyo nitajua wakati wa kesi yangu. Sasa wakiamua kunifunga itakuwa pleasure vile vile hata huko jela bado nitakuwa naendelea na research yangu kuona waliopo ni wangapi wamekuwa victimized kwa sample ya hilo gereza nitakapo kuwa nami nita document hii kwa faida ya kizazi kijacho nadhani kama nimeshindwa kuleta effective change atleast hiyo itakuwa legacy yangu hapa duniani; dalili za mkataji tamaa!
 
Tukumbuke pia issue ya Dr Bahati Gewe miaka ile, alifanya operation kadhaa hospitali ya mkoa Dodoma wasimgundue. Kumbe ni house girl by profession
 
Hii ndo Bongo na hakuna linaloshindikana Tanzania. Ndo maana wawekezaji huja mikono mitupu na kuondoka mabilionea sasa kwanini wabongo nao wasijaribu?
 
Ningekuwa mwanasheria ningemtetea huyu jamaa. Licha ya naye kula keki ya taifa japo kwa siku 3 lakini ametuonyesha nchi ilivyokuwa na viongozi wa aina yake. Iliwahi kutokea Dodoma hakuna aliyejifunza. Dah! Osama angejua angekuja hapa amiliki vidala dala vyake poa kabisa, sijui kwanini alijichanganya kwenda Abbotabad.

Jamaa hana kosa kubwa kihivyo, limekuzwa tu. Mbona BAE wameingia toka UK na wakaiba hazina hadi leo hatujui nani aliiba. Mbona hatujui Kagoda ni ya nani na nani alivunja sanduku la BoT na kuondoka na mshiko. Mbona midege inabeba Twiga na hatujui inakwenda kutua nchi gani. Mbona vindege vidogo vinatua bulyanhulu na kuondoka na dhahabu usiku na hatujui zinakwenda wapi n.k

Kwani jamaa kafanya kosa gani kubwa! yeye hakualikwa semina elekezi sasa posho angepataje na tangu miaka 50 hajui keki ya taifa ina rangi gani. aachiwe huru tu, by the way kwani gharama zake zote zinazidi posho moja ya semina elekezi!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Back
Top Bottom