Kituko Ngara: Daktari "Feki" afanya ziara, apewa ulinzi na polisi; agharimiwa - kwa siku Tatu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kituko Ngara: Daktari "Feki" afanya ziara, apewa ulinzi na polisi; agharimiwa - kwa siku Tatu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 26, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 26, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Kama vile mlolongo wa vituko na kashfa havijaisha serikalini huko Ngara mtu aliyejitambulisha kuwa ni daktari wa magonjwa ya binadamu na afisa kutoka Wizara ya Afya ameivuruga wilaya ya Ngara mkoani Kagera na kuitia hasara baada ya kufunga kituo cha afya Bukililo na kushuhudia kazi ya upasuaji wa wagonjwa katika hospitali ya misheni Rulenge. Yote yakigharimiwa na kufanyika chini ya halmashauri ya Ngara inayoongozwa na CCM.

  Mtaalamu huyo ambaye alijitambulisha kwa jina la Dr. Illongo Mlawa kabla ya kugundulika kuwa ni tapeli aliongozana na msafara wa watendaji wa halmashauri akiwa na ulinzi wa polisi kwa kile alichodai ni kukagua shughuli zilizoko chini ya wizara hiyo. Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo John Shimilimana aliyekuwa pia katika msafara huo,alijitambulisha kuwa ni Naibu Katibu mkuu idara ya Utumishi.


  Aidha mtaalamu huyo'feki' alikaa kwenye halmashauri hiyo kwa siku tatu huku akigharamiwa kila kitu kama kiongozi kutoka wizarani, na kupewa ulinzi wa jeshi la polisi ambalo hivi karibuni limejikuta likikumbwa na kashfa ya kutumia nguvu zaidi . "Ameitia halmashauri yetu hasara kubwa nimeishamuagiza mkurugenzi ahakikishe gharama zote zilizotumika kwa ajili yake zinarudishwa,alikuwa na msafara mkubwa wa magari wakati akizungukia vituo vya afya"alieleza mwenyekiti huo.


  Aidha mwenyekiti huyo alilalamika kuwa alilazimika kuwaita madiwani siku ya Jumamosi ili wakutane na kiongozi huyo,ambaye alitoa maelekezo ya kutaka watumishi wa idara ya afya kulipwa stahili zao haraka baada ya kupokea malalamiko ya kutolipwa kila alipopita.


  Mgeni huyo katika wilaya ya Ngara alikifunga kituo cha afya Bukililo kwa madai kuwa hakuridhika na kiwango cha huduma zilizokuwa zinatolewa,na mwenyekiti kudai kuwa halmashauri iliingia gharama kubwa kuwahamisha wagonjwa kwenda vituo vingine. Pia John Shimilimana aliiambia Fikrapevu kuwa baada ya kuagiza kufungwa kwa kituo hicho walimbembeleza kuwa wagonjwa wangeweza kupoteza maisha kwa uamuzi huo wa ghafla,jambo alilodai angelifikilia baadaye baada ya kuwa wametekeleza agizo lake.


  "Kama mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngara nilimbembeleza asikifunge kituo cha Bukililo kwani wagonjwa wengi wangeteseka na kupoteza maisha,tuliwahamishia katika vituo vingine"alisema Shimilimana.


  Pia kutokana na wadhifa wake na kujitambulisha kuwa ana taaluma ya udaktari na ni kiongozi wizarani aliruhusiwa kuingia katika chumba cha upasuaji wa wagonjwa katika hospitali ya Misheni Rulenge na kushuhudia madaktari walivyokuwa wakiendelea na majukumu yao. Hata hivyo mwenyekiti huyo alidai kiongozi huyo alianza kushtukiwa baada ya kuingia na kutoka katika chumba cha upasuaji katika hospitali ya Rulenge ambapo pamoja na kuvaa mavazi yanayotumiwa na madaktari tayari kwa upasuaji hakuweza kuhoji wala kuuliza suala lolote linalohusiana na taaluma hiyo.


  Mwenyekiti huyo amedai baada ya halmashauri kufanya mawasiliano na wizara iligunduika kuwa hakuna kiongozi yeyote aliyetumwa huko na hakuna rekodi zozote za jina linalohusiana na mtu huyo. Kwa mujibu wa Shimilimana Dk Ilongo Mlawa baadaye alikamatwa juzi na kuwa anashikiliwa na polisi kwa mahojiano na kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Henry Salewi alipopigiwa simu kuhusu tukio hilo aliomba apewe muda kwa maelezo kuwa alikuwa anaendesha kikao.  SOMA KITUKO HIKI CHA AINA YAKE NA VINGINE HAPA

   
 2. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji usishangae sana kama tunakuwa na rais mwizi unategemea huko chini watafanya nini kama sio kuendeleza umburukenge.

  Mafisadi wanalindwa, walikuja na ngonjera mpya ya magamba sasa sijui wataleta mpya ipi? Ngoja kwanza wajilipe na hii Dowans mpya inayokuja kwa njia za kiubabaishaji.
   
 3. e

  elimukwanza Senior Member

  #3
  May 26, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 167
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Duhh kweli hii ndiyo bongo, lolote lawezekana.

  Hata mkurugenzi wa halmashauri hajui utaratibu,sheria hivi hawa watu watafundishwa mpaka lini yani wewe unapokea mgeni bila hata barua wala taarifa. Wazee wa intelegensia nao!!!!

  Aaaahhh karagabao. MMJ inafurahisha lakini ni hatari sana.
   
 4. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,462
  Likes Received: 1,375
  Trophy Points: 280
  Huyu mtu anatakiwa apewe hiyo kazi ya ukaguzi, ameonyesha anaipenda na anaweza kuifanya kwa uadilifu mkubwa
   
 5. FiQ

  FiQ JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  duh, me hata nikisikia nchi imeuzwa na tuhame fasta cna ubishi!
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  May 26, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nyie subirini tu..
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  May 26, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Unajua hata mimi nimejiuliza kama huyu jamaa ni shujaa au mhalifu..
   
 8. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #8
  May 26, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  hahahahahaaa!!!
  Asee!!
  Mimi kesho naenda Central hapa A town, nawaambia mi ni katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani, na ninashughulikia maswala ya mabunduki yasiyotumika. Nawaambia wayachome moto yote!!
   
 9. Y

  Yakuonea JF-Expert Member

  #9
  May 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 601
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  kituko kimoja hakijakwisha kinatokea kituko kingine,hii ndo tanzania bana, hapa kuna ukosefu umakini kwa kiasi kikubwa
   
 10. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #10
  May 26, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  Aisee... E'bwana wee!.. Huyo jamaa ni creative mixer risk taker! big up to him!..

  Ingawaje kwa jicho lingine siamini kama alikua pekeyake katika mpango huo wa kuitia hasara halmashauri hiyo!..
   
 11. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #11
  May 26, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  dah! Kama alikuwa peke yake bac jamaa anaweza kuthubutu nampa hongera yake.pia inawezekana hilo litakuwa ni deal lao
   
 12. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #12
  May 26, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  duh kwa siku tatu?
  kumbe kunasiku nchi itatekwa nyara hii, kama mtu anaweza kuja na kupoa kwa siku tatu
  na wala sio masaa matatu ina maana hawa polisi wanahushishwa kwenye matukia hata ya kiharifu bila
  wao kujua, huu ni wakati wa mawasiliano ya technology kutumika serikalini
  kuna siku mtu hatateka BANK kwa kutumia hao hao polsi bila wao kujua
   
 13. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #13
  May 26, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  hivi ghalama za matumizi ya zihara huwa inakuwaje ?
  maana naanza kuwa na wasiwasi tunaweza kuwa tunalipia hivi zihara hewa mabilioni kila mwaka watu
  wanachukua hela yetu ya kodi na kwenda kununulia ngono
   
 14. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #14
  May 26, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Imenivutia sana habari hii. Najishauri sijui nimpongeze jamaa kwa kuwashika sharubu geshi la polishi, uongozi wa wilaya na halmashauri yake ama nimlaani kwa kutaka/kuwasababishia usumbufu wagonjwa (katika kituo cha afya alichoagiza kifungwe)
   
 15. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #15
  May 26, 2011
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mbona habari haionyeshi wamejuaje kama huyo jamaa ni Dr feki? mwanakijiji fafanua kidogo habari hiyo.
   
 16. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #16
  May 26, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Tatizo mambo karibu yote ni feki feki tu!!! Hata sishangai...
   
 17. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #17
  May 26, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Mtu atoka wizarani alafu halmashauri wanamgahrimia kila kitu.

  Nini tunajifunza

  • weye vyeo wnachakua malipo double double hivi anachukua wiarani aienda na mkoani au wilayani anakomba.
  • poor communication katika ofisi za serikali Threee days is too much
   
 18. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #18
  May 26, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kwasasa vitu feki ndiyo vinawezekana nchi hii, jaribu chako cha ukweli uone utakavyopigwa vita. Kwahili, intelijensia inabidi irudi kwenye majukumu yake halisi.
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  May 26, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Najaribu kufikiria gia ya namna gani mtuanaweza kuitumjia kuingilia pale Ikulu halafu akawa Kibosile mmoja hivi wa Ikulu. Ila huyu kakamatwa tu kwani wapo wengine wanaojiita "maafisa wa Usalama" wanapita na kutengeneza deals kila kukicha.
   
 20. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #20
  May 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,423
  Likes Received: 19,746
  Trophy Points: 280
  huyu jamaa wa ukweli ibaya sana
   
Loading...