Kituko Ngara: Daktari "Feki" afanya ziara, apewa ulinzi na polisi; agharimiwa - kwa siku Tatu!

HII HABARH NI YA MWAKA 2011 KUNA WATU HAWAJAANGALIA TAREHE

HUYO JAMAA NI SHIIDAA, BILA KUINGIA THEATRE ANGEENDELEA KULA KUKU KWA MRIJA.

TZ UNAWEZA KUJFANYA TISS UKALA BATA
 
Duhh kweli hii ndiyo bongo, lolote lawezekana.

Hata mkurugenzi wa halmashauri hajui utaratibu,sheria hivi hawa watu watafundishwa mpaka lini yani wewe unapokea mgeni bila hata barua wala taarifa. Wazee wa intelegensia nao!!!!

Aaaahhh karagabao. MMJ inafurahisha lakini ni hatari sana.
Usiwalaumu si unajua serikali ya ziara za kushtukiza
 
Wakurugenzi wa halamashauri ni makada wa ccm waliogombea vyeo mbalimbali wakashindwa ndio wamepewa ukurugenzi wa halmashauri nchini. unategemea nini!
 
Haya ni matokeo ya kufanya kazi kwa hofu na kutaka kumridhisha mkuu. Kwa nini mawasiliano na wizara husika hayakufanyika mapema? Hofu ya kuonekana hawajui majukumu yao? hofu ya kutumbuliwa? Kimsingi ninachoona viongozi hawa wamekosa uhuru wa kufanya kazi. Wanatambua kuhoji ni sumu kali sana inaweza kuwapotezea kibarua.

Ina maana huyu jamaa asingeingia kwenye chumba cha upasuaji,labda kwa sasa angekuwa anatembea Halmashauri nyingine. Ujinga ungekuwa uleule tu maana ni lazima watu wangepeana taarifaa kuwa mkuu anakuja, wekeni mambo sawa. Huo muda wa kutafuta uhalali wake ungetoka wapi.

Hali ya kutohoji kwa sasa ni tatizo kubwa mno kwenye taasisi za serikali. Ikiwa utahoji mambo halali kwa mtu halali, una hatari kubwa sana ya kukosa kazi. Tukio hili, hapa naona ingekuwa halali kabisa kwa Mkurugenzi kujiuzulu na ingekuwa halali kabisa kwa Raiskumwajibisha Mkurugenzi.

Mzee vipi mbona povu jingi sana? Angalia tarehe,..., uzi wa mwaka 2011 huu kipindi cha JK na si cha JPM
 
Hahahahahahahaha lol! Niacheni niinyoshe nchi!!!

breakingnews.jpg


Kama vile mlolongo wa vituko na kashfa havijaisha serikalini huko Ngara mtu aliyejitambulisha kuwa ni daktari wa magonjwa ya binadamu na afisa kutoka Wizara ya Afya ameivuruga wilaya ya Ngara mkoani Kagera na kuitia hasara baada ya kufunga kituo cha afya Bukililo na kushuhudia kazi ya upasuaji wa wagonjwa katika hospitali ya misheni Rulenge. Yote yakigharimiwa na kufanyika chini ya halmashauri ya Ngara inayoongozwa na CCM.

Mtaalamu huyo ambaye alijitambulisha kwa jina la Dr. Illongo Mlawa kabla ya kugundulika kuwa ni tapeli aliongozana na msafara wa watendaji wa halmashauri akiwa na ulinzi wa polisi kwa kile alichodai ni kukagua shughuli zilizoko chini ya wizara hiyo. Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo John Shimilimana aliyekuwa pia katika msafara huo,alijitambulisha kuwa ni Naibu Katibu mkuu idara ya Utumishi.


Aidha mtaalamu huyo'feki' alikaa kwenye halmashauri hiyo kwa siku tatu huku akigharamiwa kila kitu kama kiongozi kutoka wizarani, na kupewa ulinzi wa jeshi la polisi ambalo hivi karibuni limejikuta likikumbwa na kashfa ya kutumia nguvu zaidi . "Ameitia halmashauri yetu hasara kubwa nimeishamuagiza mkurugenzi ahakikishe gharama zote zilizotumika kwa ajili yake zinarudishwa,alikuwa na msafara mkubwa wa magari wakati akizungukia vituo vya afya"alieleza mwenyekiti huo.


Aidha mwenyekiti huyo alilalamika kuwa alilazimika kuwaita madiwani siku ya Jumamosi ili wakutane na kiongozi huyo,ambaye alitoa maelekezo ya kutaka watumishi wa idara ya afya kulipwa stahili zao haraka baada ya kupokea malalamiko ya kutolipwa kila alipopita.


Mgeni huyo katika wilaya ya Ngara alikifunga kituo cha afya Bukililo kwa madai kuwa hakuridhika na kiwango cha huduma zilizokuwa zinatolewa,na mwenyekiti kudai kuwa halmashauri iliingia gharama kubwa kuwahamisha wagonjwa kwenda vituo vingine. Pia John Shimilimana aliiambia Fikrapevu kuwa baada ya kuagiza kufungwa kwa kituo hicho walimbembeleza kuwa wagonjwa wangeweza kupoteza maisha kwa uamuzi huo wa ghafla,jambo alilodai angelifikilia baadaye baada ya kuwa wametekeleza agizo lake.


"Kama mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngara nilimbembeleza asikifunge kituo cha Bukililo kwani wagonjwa wengi wangeteseka na kupoteza maisha,tuliwahamishia katika vituo vingine"alisema Shimilimana.


Pia kutokana na wadhifa wake na kujitambulisha kuwa ana taaluma ya udaktari na ni kiongozi wizarani aliruhusiwa kuingia katika chumba cha upasuaji wa wagonjwa katika hospitali ya Misheni Rulenge na kushuhudia madaktari walivyokuwa wakiendelea na majukumu yao. Hata hivyo mwenyekiti huyo alidai kiongozi huyo alianza kushtukiwa baada ya kuingia na kutoka katika chumba cha upasuaji katika hospitali ya Rulenge ambapo pamoja na kuvaa mavazi yanayotumiwa na madaktari tayari kwa upasuaji hakuweza kuhoji wala kuuliza suala lolote linalohusiana na taaluma hiyo.


Mwenyekiti huyo amedai baada ya halmashauri kufanya mawasiliano na wizara iligunduika kuwa hakuna kiongozi yeyote aliyetumwa huko na hakuna rekodi zozote za jina linalohusiana na mtu huyo. Kwa mujibu wa Shimilimana Dk Ilongo Mlawa baadaye alikamatwa juzi na kuwa anashikiliwa na polisi kwa mahojiano na kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Henry Salewi alipopigiwa simu kuhusu tukio hilo aliomba apewe muda kwa maelezo kuwa alikuwa anaendesha kikao.



SOMA KITUKO HIKI CHA AINA YAKE NA VINGINE HAPA

 
Mzee vipi mbona povu jingi sana? Angalia tarehe,..., uzi wa mwaka 2011 huu kipindi cha JK na si cha JPM
Ha wengine si walaumu sana; watu wanarukia kujibu tu; miye nilikuwa nakumbushuia baada ya habari za yule Wakili na yule mnunuzi wa majumba ya Lugumi. Kila kitu kinawezekana..
 
Back
Top Bottom