Kituko Ngara: Daktari "Feki" afanya ziara, apewa ulinzi na polisi; agharimiwa - kwa siku Tatu!

Serikali kwa wilaya za pembezoni haifiki, huko huko kati ya ngara na karagwe kuna mtu alishawahi kuwa na nchi yake analipisha kodi watu na ilidumu miaka kadhaa sio siku 3. Pia hata Tabora kuna mtu kishakuwa na nchi yake na jeshi pia tra yake.
 
Kama Magogoni watu wanazamia dhifa na sherehe mbalimbali sembuse huku Ngara?? inteligencia yetu inauwezo wa kugundua kwamba maandamano yatakuwa na rabsha na sio kwingineko!!!
 
Dokta baada ya kukamatwa na kupekuliwa katika kituo cha polisi Ngara hakuwa na kitambulisho chochote.
 
Huyu BINGWA nimemkubali. Hata hivyo ana uhakika kuwa baadhi ya watendaji serikalini wanatekeleza majukumu yao bila kufuata taratibu.
 
Kipindi huyu jamaa yuko Ngara nami nilikuwepo kikazi nikamshuhudia, alikuaja na basi la Taqwa liendalo Burundi.Alifika ofisi ya Mkurugenzi akajitambulisha na kupewa usafiri na ulinzi,alitembelea zahanati kadhaa na vituo vya afya.Kuna zahanati moja alifika akakuta choo ni kichafu kweli kweli akamuita mkuu wa kituo hicho akamwambia asafishe na akakisafisha vizuri, pia aliwakuta watumishi wazembe baada ya kuongea na wananchi akamwagiza mkurugenzi amwamishe haraka sana...Sio siri kipindi hicho kulika na heka heka pale halmashauri.Kichekesho zaidi Naibu waziri wa kilimo alikuwepo na alipata taarifa za huyu bwana lakini inaonekana hawafahamiani. Nampongeza kwa ujasiri wake tunahitaji viongozi feki kama hawa wawe real....kwa upande wangu huyu jamaa apewe tuzo ya ujasiri kwa kupeleka maendeleo mbele.Vituo vyote alivyotembelea usafi umefanyika vizuri,vyoo vimechimbwa,wodi zimesafishwa kuna vituo vya afya wamepewa mashuka mapya kipindi cha ziara yake
 
Huyu mtu anatakiwa apewe hiyo kazi ya ukaguzi, ameonyesha anaipenda na anaweza kuifanya kwa uadilifu mkubwa

Provided hakuomba rushwa katika maamuzi yake anafaa kabisa kuliko wenye authority ambao kila wanapotaka kufanya maamuzi wanfikiria personal gains, fanya au ninapeleka taarifa huwezi kazi ili uondolewe
 
kituko kimoja hakijakwisha kinatokea kituko kingine,hii ndo tanzania bana, hapa kuna ukosefu umakini kwa kiasi kikubwa

Nafikiri serikali imekuwa kubwa mno kiasi kwamba hata kui-manage effectively imewashinda. Kama JK alijivunia mkongo wa mawasiliano kutua Tanzania kwa nini kuwsiwe na effective IT katika wizara na idara za serikali. Wanashindwa nini kufunga mtandao nchi nzima katika idara zote ili kurahisisha mawasiliano?. Mtu upo wizara ya afya unatoa press release kwa njia ya email kupitia wafanyakazi wote.

Ila wanaogopa Mtandao utabadilisha watu mawazo!
 
Ndani ya BONGO-DAR-ES-SALAAM! hii inatoa taswira ya usalama na mawasiliano yalivyokuwa butu Tz,kumbe ndo maana makontena yanakamatwa nje ya nchi na siyo ndani ya nchi,...inteligencia ilikuwa busy na CDM!
 
Huyu ni shujaa aliyechoka na longlongo za serikali tukipata viongozi kama hawa tungekua mbali sana
 
Ila.. huyo nadhani kaamua kwenda mbele zaidi tu ya wengine; maana wapo wengi mijini wanaojipitisha kama "Msaidizi wa rais".. nimesoma habari moja (iliripotiwa hapa) jamaa aliyejifanya ni Askofu Malasusa akijaribu kumtapeli Meya wa Ilala sijui! Nadhani watu wameshajua namna ya kutapeli kwa kutumia madaraka maana wanajua watu wanaogopa wenye mamlaka. Ndio maana miye mwenzenu nawapuuzia sana watu wenye kujiona wana madaraka fulani! Kwamba wanafikiri kwa sababu yamadaraka yao wanaweza kukufanya uinamishe kichwa ukainama, ubong'oe na ukabong'oa.

Exactly! Madaraka kidogo mtu anajiona mungu mdogo! Watu wengi hawajui madaraka = utumishi. But for this i blame it squarely on nyerere na policies zake. Yeye ndio alijenga hii hofu ya viongozi!
 
Mambo nya chama cha magamba, wako wapi kina JiniasBrein na wenzake? Wale wenye mapenzi ya dhati kwa serikali na chama chake? Iko kama muvi flani vile...
 
Huyo jamaa ni bonge la Researcher: tungepata ripoti nzuri sana juu ya utendaji ktk hospitali zetu na halmashauri kwa ujumla kama angemaliza kufanya analysis:

Hizi halmashauri zetu bwana na zenyewe zimezidi kwa ubadhilifu na pia Polisi nao wamezidi kwa kukurupuka, wanatoa huduma kwenye vitu vya kipuuzi, vya kimsingi(kama kuwalinda wanaharakati wetu wa CDM) wanaacha.
 
Mi nadhani huyo m/kiti na mkurugenzi wa halmashauri wanatakiwa wakamatwe mara moja na kushtakiwa kwa kosa la uzembe ulioisababishia hasara halmashauri yao! Kwanini wamgharamie huyo jamaa hata kama kweli ni ofisa kutoka wizarani? Inamaana hawajui kuwa mtumishi analipwa na ofisi yake kuanzia malazi, posho ya safari, na marupurupu yote anapotumwa nje ya ofisi? Huu ni uzembe tu. Au ni rushwa wanampa ili awachunie baadhi ya mambo! This must end now!

Mkuu viongozi wengi tu hasa hawa wa halmashauri hawana training yoyote. Mtoto wa mjomba amemaliza shule tu na anakipenda chama chake basi amechukua position. Ingawa wengi tunawashangaa wanavyo-operate wao wanaona wako sawa tu maana na viongozi wao ni hivyo hivyo. Very very sad!
 
Kipindi huyu jamaa yuko Ngara nami nilikuwepo kikazi nikamshuhudia, alikuaja na basi la Taqwa liendalo Burundi.Alifika ofisi ya Mkurugenzi akajitambulisha na kupewa usafiri na ulinzi,alitembelea zahanati kadhaa na vituo vya afya.Kuna zahanati moja alifika akakuta choo ni kichafu kweli kweli akamuita mkuu wa kituo hicho akamwambia asafishe na akakisafisha vizuri, pia aliwakuta watumishi wazembe baada ya kuongea na wananchi akamwagiza mkurugenzi amwamishe haraka sana...Sio siri kipindi hicho kulika na heka heka pale halmashauri.Kichekesho zaidi Naibu waziri wa kilimo alikuwepo na alipata taarifa za huyu bwana lakini inaonekana hawafahamiani. Nampongeza kwa ujasiri wake tunahitaji viongozi feki kama hawa wawe real....kwa upande wangu huyu jamaa apewe tuzo ya ujasiri kwa kupeleka maendeleo mbele.Vituo vyote alivyotembelea usafi umefanyika vizuri,vyoo vimechimbwa,wodi zimesafishwa kuna vituo vya afya wamepewa mashuka mapya kipindi cha ziara yake


Oh dearGod, natamani ningekuwa mwanasheria nimtetee huyu bwana (Nawaomba wenye uwezo mjitokeze kumtetea)..lakini pia ningekuwa RAISI, Ningemteua kuwa Mbunge na kumkabidhi wizara. Inaonesha anakerwa sana na hali mbaya katika sekta ya afya kutoka moyoni,potelea mbali hata kama alilipwa posho out of thta..mimi sioni hata kidogo utapeli wake..ila naona sana USHUJAA kutoka kwake..He is real patriotic. Long Live man.
 
Hivi TZ lini tutakuwa makini na utendaji wetu? Mkulu naye anatapeliwa kirahisi, viongozi ngazi za chini nao mtindo ule ule sasa hii nchi ina wasomi kweli? Niliwahi kusikia tena siku moja kituo cha uwekezaji nacho kilitapeliwa na mzungu kikawa tayari kugawa ardhi kule Bagamoyo kumbe jamaa kule alikotoka hata ofisi hana!!! MKWER'EEEEEEEEEEE!!
 
Back
Top Bottom