Kituko cha mwaka 90

Kituko cha mwaka 90

Kuna mfanyakazi tuliletewa kutoka singida basi nikaenda kumpokea stand then nikawa nampeleka ofisn kwa maza hapo ppf tower ili amuone, atupe na lift ya kwenda home,ile tumefka kwny lift imeanza kupanda juu,nikaona yule dada amechuchumaa lift ilivofunguka nikamuuliza kwann ulichuchumaa akasema nilijua tunapimwa uzito ndo mana nilichuchumaa,hahah!sitamsahau

Ha ha ha nimefurah sana
 
Sio kwamba najidai wala nini ila ki ukweli sikumbuki kitu chochote ambacho nimewahi kuwa mshamba, ninikumbuka nitakitupia!

Usijali sana kwamba hujawahi kukutana na kitu ambacho unaweza kuchangia kama ushamba , yani hivi ulivyochangia kwenye huu uzi tayari nishajua uko mshamba kiasi gani.
 
hahahaha we best huenda ulikua unataka maji ya uzima mchungaji hakujua tuuuu....duh lakin ulitisha maji ya kunywa kanisan!! kama nakuona vile hahahaha
 
Hivi ulishawahi kwenda ugenini ulivokua mdogo alafu ukajikuta umekojoa kitandani jinsi huo usiku unavokua na heka heka.......???? Usitake kujua kilichotokea....
 
Kuna siku jamaa mmoja mgeni kutoka shamba alikuja kwetu kuingia chooni na kuflash sasa yale flash tank huwa

yalikuwa yanapiga kelele wakati maji yanatoka Duh! jamaa alipiga yowe moja alipambana na mlango akitaka kutoka

toi kwa nguvu mwishowe alikuja kupandishia suruali sebuleni.

Ha ha ha ha ha haaaaaaa! Mbavu zangu, jamaa umenichekesha sana!
 
teh teh! Ningekuchapa tu, huwezi kunitia aibu kiasi hicho, siku nyingine ukiona hizo ndizi unapita mbali kama umemuona simba vile

Hahah lkn asubuh dingi alivoenda kazin nilipewa kichapo na maza cha kufa mtu afu nikaambiwa ole wako umwambie baba ako!haha
 
Usijali sana kwamba hujawahi kukutana na kitu ambacho unaweza kuchangia kama ushamba , yani hivi ulivyochangia kwenye huu uzi tayari nishajua uko mshamba kiasi gani.

Hahahaha hahaaaaaaaaaaaaa............. Poapoa!
 
M kipind nikiwa darasa la tatu 2003, ilitokea msichana mmoja kaja na mapera shulen ticha akamgombeza kisha akanichagua mm na mwenzangu tukatupe choon tulipofika tukapeana wazo la kuyala sisi, mim nikaanza kula yule mwenzangu aloponiona mekula akatupa yake choon kisha akakimbilia darasan na mimi nikatupa kisha nikamkimbilia ila akawah kunisemea duuu sikuchapwa ila mwalimu alivyoniumbua duu ilikuwa aibu kinoma
 
Mimi nilijua watu wote wanaovaa miwani ni wasomi wazuri sana na nikatamani niwe kama wao.
 
Daa mimi kuna siku nilienda kwa rafiki yangu kwao mbezi ambaye tulisoma nae chuo..sasa usiku akasema tulale sebuleni maana ni joto sana. Ni nyumba yenye familia kubwa tu. Sasa mimi huwa nishazoea kulala bila nguo, siku hiyo nililala na nguo ila uzalendo ulinishinda usiku wa manane nakavua nguo zote nikabaki kama nilivyozaliwa. Asubuhi ilipofika daaaaah kumbe shuka lilikuwa huko nishazoea najiachia home kwetu chumbani kwangu..kilichotokea naona siku hiyo mama mwenye nyumba hakwenda kazini maana sebureni ndo ilikuwa njia yake na wanae wakike. Daaaaah ilikuwa aibu sitosahahu.
 
Mimi nilijua watu wote wanaovaa miwani ni wasomi wazuri sana na nikatamani niwe kama wao.
Hii inahusika sana mkuu nikiwa std 3 nilikuwa natamani kuvaa miwan kwan nilijua wanaovaa miwan wana akili sana
 
Nakumbuka enzi hizo nilikuwa sijawahi kuingia Hotelini wala mgahawani,

sasa one day rafiki yangu akanipa offer ile kufika kwenye mgahawa wa kisasa kimtindo si nikaanza kupiga hodiii, hodiiii wacha rafiki yangu aangue kichekoooooo, wewe ulifanya yepi enzi za ushamba
Niliendaga ugenini na ndugu yangu,kufika usiku tukajibaraguza hatukula.Usiku wa manane njaa ikazidi nkajikuta niko jikoni,purukushani za masufuria nikamsikia mwenye nyumba anauliza "nani wewe?"nkajibu nyauuuuuuuuu.Nilpotoka ndugu yangu naye akaingia mwenye nyumba akarudia tena "nani huyo?"jamaa likajibu "nyauuu mwingineee".
 
Nakumbuka enzi zile za kubalehe kwa kawaida haka katabia ninako hadi leo huwa nikioga au kukojoa sijiangalii sehem za private.sasa siku moja nakojoa vichakani nika shangaa vitu vingi vyeusi mimi mbio mpaka kwa bibi.bibi bibi nina wadudu wengi wamepanda!kuvua suruali akauliza wako wapi mi nika muonyesha tu ma.vu.zi twangu!aiseee nyumba nzima ilikufa kwa kicheko!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom