Poz bizo swaxter
Member
- Feb 27, 2013
- 46
- 3
mimi nilienda kwa rafiki angu nikakaribishwa chakula kilikuwa kwenye hotipoti, nikala chote, kumbe kilikuwa cha watu wote, niliona aibu je?
du! Umen gusa Btr low hiyo imenikuta nilizibua ubwabwa
mimi nilienda kwa rafiki angu nikakaribishwa chakula kilikuwa kwenye hotipoti, nikala chote, kumbe kilikuwa cha watu wote, niliona aibu je?
Mbona mwenzio siku yangu ya kwanza kusafiri na ndege nilianza kusalimia wasafiri wote ndani ya ndege,unacheza na ushamba nini..
Nimecheka sana. Lazima wewe utakuwa unatokea Mwanza au Shinyanga
nakumbuka wakati naingia mjini nilifikia kwa duka ya bro wangu sasa nilikaa apo kama mwezi mmoja ivi sasa umeme ukaisha kanambia niende nikanunue umeme kanipa noti ya elfu moja kipindi umeme ukiwa unit moja tsh.30...sinikajifanya nishaujua mji nikachepuka duka la jirani nikasema hapa napata umeme kilo ngapi? jamaa kuona ivo akajiongeza kanambia hapa kwangu umeisha ila chukua hiki kiroba nenda duka lile palee mwambie akupe kilo hamsini...ndugu yangu nilizungushwa karibu mtaa mzima utafikiri waliambiana...mwisho bro ikabidi anifuatilie.....
Battery Low we share the verry same story,mie ilikuwa kwa mjomba na rafiki yangu ambaye alikuwa mchungaji (R.I.P Mchungaji Kyando) ni mbezi beach makonde ss wenyeji wapo nje ila mie na mshkaji sebuleni,ukaletwa ugali maharage jamaa kakata kipande kaenda nje thn mie nikamimina maharage na kisamvu kny hotpot nkaanza kule bt tonge la tatu madogo wawil nao na sahan zao mkonon wanaingia na kuona vile wakatoka wanalia kuwa njaa inauma na mgen anakula ze msosi wote. Siku nyngne tena tumeenda tukakaa nje chin ya mwarobain,mm mshkaj na Mchungaj ss zikaletwa soda zikafunguliwa ila mchngj akawa anaendelea na story,bas mm nkachukua nkapiga km pafu nne ama tano(maana ilikuwa kitu bariiidiiiiii na tumetoka juan) basi kuona vile pasta akasema 'haya tusali tuombee vinywaji' yaan mpaka aibu coz soda isjakuwa almst nusu mlingoti
Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
dah mi bado sijui itakuwaje mana sijawah panda lift kila ikinihusu nakwepa nko radh nipande ngaz had nitoe jasho,pia nilikuwa kwa semina ubungo plaza nilikwepa ngaz za umeme dada mmoja alianguka nilimcheka mi nikatumia ngaz zetu zile,dah yangu sijui itakuwaje