Abraham Lincon
Member
- Oct 22, 2010
- 78
- 0
Kuna baadhi ya watanzania hii leo wamepokea simu inayodaiwa kutoka kwa mh. Kikwete akiomba apigiwe kura itakayomrudisha madarakani kwa kipindi cha pili. Nashukuru Mungu sikupigiwa simu hiyo. Jambo la kuchekesha na kusikitisha ni pale anaposema atajirekebisha katika makosa yote aliyofanya katika kipindi chake cha uongozi kinachoisha. Binafsi nashindwa kumuelewa huyu mheshimiwa. Sidhani kama hata akipewa miaka 100 kuna chochote kitakachoongezeka hasa ukizingatia ubinafsi uliokithiri wa viongozi katika serikali yake. Ubinafsi uliochochea ufisadi papa wa kutisha, rushwa zilizokithiri na matatizo mengine kibao katika jamii. Sielewi kwa nini mheshimiwa hakuyaongelea hayo wakati wa kampeni badala yake akadai serikali yake imefanya makubwa. Kwa nini aombe msamaa wa makosa aliyofanya gizani?(kwa njia ya simu). Njia hii aliyoitumia mheshimiwa huyu inanifanya niamini kuwa ni kweli yeye pamoja na kundi lake wanahusika katika kumchafua Dr. Slaa ambaye pia alichafuliwa kwa njia hii hii ya simu! Hiki ni kituko kikubwa ambacho hata hivyo hakitamsaidia chochote. Watanzania tumechoka, tunataka mabadiliko! Chagua mh. Dr. Slaa, chagua CHADEMA. Mungu ibariki Tanzania, Mungu bariki uchaguzi mkuu Tanzania.