Kitu gani kinanisumbua?

Kitu gani kinanisumbua?

Oohhh..kila status anayoweka mtu yyt ina maana au sababu yake!!

Inavyoonekana Alionyesha penz lake kwako kwa kujaribu namna anavyojua ila hukujali alichokua anafanya kwa juhud kukupa ujumbe toka ndani yake..sasa umempoteza na wewe umejipotezesha ( au pengine hakua fungu lako), and it seems nothing you can do again to her and nothing she expects from you again!! (Nimewaza tu)
This might be same thing here bro
 
Hello everybody,

Mimi ni kijana mwenye miaka 20+....
Nimekua member wa JF kwa muda sasa nikisoma nyuzi katika majukwaa mbali mbali, lakini nilivyo pitia hili jukwaa kwa muda wa week chache nimesukumwa sana kuandika kitu nikasaidika toka kwa wadau wa hapa kwani, kwa asilimia kubwa naona watu wanatoa ushauri wa kujenga sana wenye msaada kwa hawahitaji japokua watani hawakosi pia.
Bila kupoteza muda nijielekeze moja kwa moja kwenye nia iliyo nileta kwenu.

Tangu nianze safari yangu ya mahusiano mpaka sasa nimesha vunja mahusiano na wanawake wanne mpaka sasa. Mwanzoni mwa mahusiano huwa naishi na mwanamke kwa furaha na kumpenda sana na moyo wangu huwa unaamini kuwa huenda akawa wangu wa maisha lakini nikisha kaa nae kwa miezi kadhaa au mwaka najikuta napoteza hamasa juu yake.

Yaani naanza kumuona wa kawaida, huwa najichukia jinsi kiwango changu cha kumjali kinavyo shuka pia naanza kuwa busy sana na ratiba zangu binafsi.

Yaani huwa nakaa chini najitahidi kurudisha upendo wa nliokua nao awali lakini najikuta nafanya kwa siku chache tu halafu hali inakua ile ile.
Mfano naweza nisimtafute hewani hata siku tatu mfululizo na yeye asipo nitafuta ndio imetoka.
Naacha kuwanae karibu kabisa na nikiulizwa kwanini nimebadilika huwa naomba msamaha lakini maswali yakizidi nakasirika na tunakosa maelewano mwishoe tunavunja mahusiano.

Hivi karibuni nimeachwa na mdada nilie pendana nae sana na kudumu nae kwa muda wa miaka miwili na nusu sababu ikiwa ni hihi ya kutokujali na kumpuuzia kabisa.

Hali hii naiogopa najitahidi niwe consistent na ku_mantain kiwango cha juu cha mpenzi lakini nashindwa kabisa.
Sasa sjui chaguo langu bado au ni nini hasa yaani dah i can't explain. ..

Nadhani hakuna mwanamke anaweza kukubali kuvumilia mabadiliko yangu nogopa kuishi bachelor siku za usoni.
Hivi ni kipi shida hasa! kwa mtu anaeweza kunijuza shida yangu na utatuzi wake atakua amenisaidia sana....

Natanguliza shukran zangu za dhati kwa mchango wako kwani naamini huenda ukanisaidia ku improve kwa namna moja ama nyingne.
utoto hauna tiba, nafuu yake ni kuendelea kula ukue utoto utoke.
 
Oohhh..kila status anayoweka mtu yyt ina maana au sababu yake!!

Inavyoonekana Alionyesha penz lake kwako kwa kujaribu namna anavyojua ila hukujali alichokua anafanya kwa juhud kukupa ujumbe toka ndani yake..sasa umempoteza na wewe umejipotezesha ( au pengine hakua fungu lako), and it seems nothing you can do again to her and nothing she expects from you again!! (Nimewaza tu)
Siku zote kila mtu anaamini upande wake upo sahihi
 
Mi nafikiri ni kawaida tu.
Inakuaje kwa wale wanao fanikiwa kudumu na mtu mpaka unatamani ungekua wew, maana hii kuachana achana inashusha reputation kabisa yaan unaweza anza kukosa confidence na jinsi ulivyo kabisa
 
Ni kawaida,kinachotakiwa ni kuridhika,usipotosheka hawaishi hao,utajikuta unazeeka na mambo ni hayohayo.Hata kama utachukua miss world itafika siku utamuona wa kawaida,kwahiyo weka limit,uoe na uanze kitu kinachoitwa kuvumiliana...
 
Ni kawaida,kinachotakiwa ni kuridhika,usipotosheka hawaishi hao,utajikuta unazeeka na mambo ni hayohayo.Hata kama utachukua miss world itafika siku utamuona wa kawaida,kwahiyo weka limit,uoe na uanze kitu kinachoitwa kuvumiliana...
Hahahah nimecheka hicho.[emoji16] kitu kuvumiliana
 
Hao wanawake unaokaa nao unakuwa umewatamani tu. Ndio maana "wanachuja" kama mtu amekula mua utamu wake ukaisha. Ukija KUPENDA HASA (sio kutamani) hutaweza kukaa siku mbili bila ku-communicate nae
 
mkuu rbt inawezekana huwa hupendi kikweli

inawezekana unaamua kuwa na mtu bila kujali kama ni true love au infatuation

maanake infatuation pia inafanana kabisa na love isipokuwa yenyewe ni hisia zitokanazo Zaidi na mihemko labda kwa sababu ya mwonekano wa mtu hasa,mara nyingi aina hii ya upendo kudumu ni mara chache sana

ila true love kufa sio rahisi maana ni hisia zile za ndani kabida kumwelekea mwenzi wako,na huenda hata ukaashangazwa na upendo unavyojengeka,unaweza ukakutana na mtu leo ukamwona wa kawaida sana yaani wala asikushtue,hata baada ya miezi kadhaa ila kadri wakati unavyopita na unavyozidi kuinterract na mtu huyo unajikuta kidogo kidogo unaanza kumwona special na anaanza kukuvutia,tena anaweza akawa wa kawaida sannn au hata sio mzuri au mzuri tu sana pia inawekana

em nikuulize huwa unachukua muda gani kufall in love na hao the so called ma ex wako?

mkiwa kwenye mahusiaono huwa mnasolve vipi ikitokea mmekosana?

ni activities zipi ambazo mnafanya mara nyingi Zaidi mkiwa pamoja?

katika wote ulioachana nao ikitokea umemkubuka mmojawapo huwa unakumbuka nini?
 
Kila mtu yuko hivyo...awe mwanamke awe mwanaume. Inchofanya watu wanaishi pamoja miaka mingi ni.
1. Mazoea
2. Kuwa na vitu vya kufanya pamoja kama kulea watoto, biashara n.k.

Tiba yake ni hii..ukipata mpenzi unaye mpenda tafuta kitu cha kufanya naye pamoja ambacho kitawaweka karibu. Ambacho kitawafanya mpigiane simu mara kwa mara na kuongea mara kwa mara.
 
Kama Vile Wanawake Walivyo na Uzuri wa Ndani Ambao Huwezi Kuuona kwa Macho Ndivyo na Sisi Wanaume Tulivyo na Pesa za Ndani Sana Huwezi Kuziona kwa Macho


Lakini Zipo!
 
Nami ilikuwa ivo ivo japo am mwanamke na nilipokuja kususiwa mimba ndo nikachukia kabisa mahusiano ..achana na kumchoka MTU mapema ila nilichukia kabisa.nipo ndoani ili niendelee kuishi.Only that
 
Back
Top Bottom