Kitu gani kinakwamisha hawa waliotesa na kuua wasikamatwe?

chagu wa malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
467
Points
250

chagu wa malunde

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
467 250
Hili jambo mimi linashangaza sana japokuwa mimi nina uelewa mdogo sana wa sheria.

Mfano ibara ya 13(6) ya katiba ya Tanzania inazuia kutoa adhabu au mateso na manyanyaso kwa mtu yoyote yule. Ibara ya 14 ipo wazi kabisa kwamba kila mtu ana haki ya kuishi. Ibara ya 13 (b) inasema hamna mtu atatiwa hatiani mpaka ithibitike kweli ametenda kosa hilo. Kwa ujumla ibara ya 13(6) ya katiba ya Tanzania inataka mtu ashitakiwe kwa kufuata taratibu na sheria za nchi. Pia kifungu cha 27(1) cha sheria ya ushahidi kinataka mtu akiri na kukubali kosa bila kulazimishwa.

Sasa kuna watuhumiwa walikutwa na milango inayosadikiwa ni ya wizi. Walikamatwa na kupelekwa ofisi ya kata kahama wilaya ya ilemela. Palikuwa na Mwanajeshi alikuwa anadai ameibiwa TV. Yeye akahisi hawa ndio wezi wake. Hivyo alianza kuwapiga na kuwatesa akishirikiana na migambo.Pia mtendaji wa kata na mwenyekiti walikuwepo. Kujichukulia sheria mkononi ni kosa na hivyo wanastahili kukamatwa sababu mmoja watuhumiwa alifariki . Mmoja wa watuhumiwa aliyebahatika kupona anasema ofisi ya mtendaji wa kata ilifungwa milango na madirisha mateso yalifanyika humo ndani ili waseme ilipo TV

Waliofanya tukio hili wanafahamika na hata wananchi walijazana hapo ofisini na kushuhudia. Sababu walikuwa katika mikono salama ya mtendaji walishindwa nini kuwapeleka polisi halafu baadae Mahakamani! Pia mzee Michael anasema waliambiwa na mtendaji watoe mil 9 ili kesi iishie hapo kata.

Hivyo kinachoshangaza sasa imepita miezi miwili mbona hawachukuliwi hatua? Au kuna watu wana kinga hata wakiua hawakamatwi?
 

chagu wa malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
467
Points
250

chagu wa malunde

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
467 250
Zawadi ya mwizi ni kisago mpaka umauti umukute

Sina huruma na mwizi kabisa wamenirudisha nyuma sana hawa washenzi

Sent using Jamii Forums mobile app
We unajuaje huyu aliyekufa kama alikuwa mwizi? Hakukamatwa anaiba.alikamatwa na milango inayosadikiwa ya wizi. Akili ndogo pua kubwa. Ilitakiwa uchunguzi ufanyika kwa taratibu za kisheria tena huenda wangepata mengi . Acha usho...
 

chagu wa malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
467
Points
250

chagu wa malunde

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
467 250
Zawadi ya mwizi ni kisago mpaka umauti umukute

Sina huruma na mwizi kabisa wamenirudisha nyuma sana hawa washenzi

Sent using Jamii Forums mobile app
Shog... Kama wewe na kelele zote unakuta umeibiwa Tv ya laki nne. Ndio sababu ya kuvunja sheria. Watu wameibiwa mamil na wanafuata sheria za nchi
 

Forum statistics

Threads 1,389,958
Members 528,065
Posts 34,039,736
Top