Ngugu wana JF,
Kuna thread ilianzishwa hapa kuhusu yaliyojiri bungeni leo kuhusu Wabunge Wenje, Moses na Tundu Lissu. Ni kweli Tundu Lissu amesema Naibu Waziri kadanganya bunge na yeye na ushahidi. Kilichotokea ni kwamba Tundu Lissu alikatishwa kumwaga radhi hadharani. Baada ya maswali na majibu, kabla ya Waziri David Mathayo kuanza kusoma bajet yake, ndo Mwenyekiti wa bunge kamtaka Tundu Lissu atoe uthibitisho saa tano na kama hana afute kauli yake. Ndipo Moses na Wenje walipoibuka na malumbano kuhusu Tundu Lissu kuongezewa muda. Mwisho wa yote, Wenje katolewa nje. Ninachoona kwa tafsiri yangu ni kama ifuatavyo;
- Kulikuwa na ulazima gani wa wabunge Wenje na Moses kumkingia kifua kumtetea Lissu kuongezewa muda wakati Lissu mwenyewe hajadai kuongezewa muda? Tena Lissu alikuwa yatari kutoa ushahidi wake papo hapo? Nionavyo mimi baadhi ya wabunge wa CHADEMA wanatafuta cheap popularity.
- Rafiki yangu Wenje hakujua kuwa leo Lawrence Masha yupo mle ndani (kama mgeni bungeni)
- Je kwa nini bunge la awamu hii imejaa malumbano yasiyo na msingi? Miongozo ya spika, taarifa, etc. malumbano yasiyo ya msingi.