Kitila Mkumbo: Lowassa hana budi kukubali matokeo

Kitila Mkumbo: Lowassa hana budi kukubali matokeo

Dk Kitila, imefikia wakati iwapo huwezi kuchambua mambo kisomi ukae kimya na sio kudhalilisha uprofesa wako na kuonekana mtu wa njaa badala ya taaluma. Nimekuwa nakufuatilia hoja zako tangu utoke CHADEMA hoja zako dhidi ya chama kile ziko kinjaa zaidi ya kisomi ukijaribu kuibeza CHADEMA bila vigezo vya kisomi wala Critical Thinking bali kushabikia upande wa CCM au wowote ule ulio rival na CHADEMA

Nimesoma habari zako kwenye gazeti la Mwananchi ukibeza Lowassa kujitangaza ushindi siko katika Lowassa kujitangaza ushindi bali nipo kwenye uchambuzi wako uko mweupe hauna uhalisia kwa kuangalia matokea ya Tume kisha kumtaka Lowassa akubali kashindwa maana number zinakubaliana na ushindi wa Magufuli

Dk Kitila kumbuka kwamba uchaguzi huu haukuwa na Tume Huru kwahiyo anything possible chama tawala kucheza rafu na kujipa ushindi, rafu hizi huchezwa kitaalamu kuanzia chini kwa wabunge ili kwenye urais waweze kuhalalisha kuwa walishinda kihalali. Kwa kudispute kauli yako kutolea mfano wa wabunge naweza sema Mwakyembe(Kyela) Mabula (Mwanza), Sauli (Tukuyu) hawa ni moja ya wabunge ambao hawajashinda kihalali na namba kama hii ni kubwa zaidi ya 60, hii ni katika mbinu za chama tawala kujihalalisha kuwa kilishinda kihalali angalia matokeao ya awali yalivyoyangazwa kisha wakagomea na kujikuta washindi ukizingatia msimamizi mkuu wa uchaguzi majimboni ni Mkurungezi wa wilaya anayefanya kazi kwa niaba ya CCM.

Hata madikteta kama Hosni Mubarak walikuwa wakishinda kwa zaidi ya 85% kwenye chaguzi zao lakini baada ya kutolewa madarakani kwa mapinduzi vyama vyao havikufikisha 10% ya kura kwahiyo usijaribu kubeza wenzio kwa sababu nyepesinyepesi, nakuuliza swali iwapo uchaguzi ulikuwa wa Huru na Haki kwanini polisi walivamia KItuo cha CHADEMA cha kukusanyia kura? Jambo ambalo ni haki katika chaguzi huru? Kwanini polisi walivamia kituo cha Haki za Binadamu kilichokuwa kinakusanya kura kama NEC? Jibu ni kwamba chama tawala kiliogopa kuumbuliwa wizi wake wa waziwazi maana namba za Tume na wengine zisingefanana. Na ulizo la ziada kwanini CCM ilitumia nguvu nyingi kupinga Tume Huru ya Uchaguzi iwapo hushinda kihalali?

Mwisho hakujawahi kuwa na uchaguzi Tanzania wenye ushindani kama huu na matokea ya Tume hayaonyeshi uhalisia wa ushindani uliokuwepo nchini na kwa kukupa ushahidi tangu Magufuli atangzwe nchi iko kimya kama imepata msiba maana watu wanasense kuna kitu kilifanyika ambacho si halali. Miaka yote akitangazwa mshindi wa CCM wananchi huendelea na shughuli zao kama kawaida lakini si uchaguzi huu. Dk Kitila tumia zaidi taaluma na akili sio ushabiki usio na maana

1. wakati unaingia kwenye uchaguzi ulijua kuwa tume siyo huru? akili yako na hao viongozi wako ilitakiwa ianzie hapo; kama tume siyo huru kuna haja gani ya uchaguzi?? kwa nn tusibadili kwanza tume kisha ndio tuingie kwenye chaguzi??

2. lowassa ndie aliyekuwepo mwaka 2010 wakati mlisema slaa kashinda! lowassa ndiye aliyemweka kikwete 2005 madarakani anajua kila kitu bwana mdogo, kila kitu!! sijamtaja sumaye na mwizi wa kura maarufu bwana kingunge ambao wote ni ukawa...hizi ni fugure kubwa sana

3. kwa nn CCM wamepata wabunge wengi? hauoni mnaji conttradict?? yaani wabunge wengi wa CCM...ambao hamlalamiki ila rais awe CDM

kaa chini fikiri, utamwona kila mtu mbaya..EL, SUMAYE NA KINGUNGE wanajua kila kitu na wangeweza ku intervene!! au waliamini CCM washakuwa malaika??kama wameshindwa hilo dogo....wangewezaje urais???

unataka kila mtu aseme lowassa kaibiwa kura

iwe kaibiwa au la; ni kuwa wamezidiana ujanja thats it!!

fanya kazi
 
Kale Kajamaa ni Njaa Kali na Kinafiki sana. Hivi Chama chake ACT wasaliti wamewapa viti Vingapi?
 
Well said Mwanamutapa umeongea sahihi huyo jamaa hajui kuchambua uchambuzi wa kinjaa na kishabiki badala ya kisayansi
 
Mimi huyu Kitila ananishangaza kwa mengi sana....
kinachonishangaza ni jinsi Zitto alivyo muamini huyu

Huyu profesa ni kiazi kweli , uchambuzi wa siasa na yeye wapi na wapi mtu kasomea pyscology Leo mchambuzi wa siasa this is only in Tanzania
 
Usitaraji kupata uchambuzi wenye afya kipindi hiki.watu wako na harakati za kujikomba waambulie nafasi kuramba viatu vya mzee.ukuu wa vitengo ndugu......!!
 
Mkumbo acha upumbavu ysmekushinda ya act unaingilia ya Chadema we we uliombwa ugombee urais Act kwanini ulikataa? Ungegombea kisha ukakubali matokeo achana Na Chadema ulifukuzwa unaifuata fuata
 
Huyu sio mchambuzi analazimisha , anaganga njaa so ajiunge Na CCM? Ukweli anaujua bado anataka kupotosha wizi Wa kura umefanyika anataka watu wakubali kirahisi kama Wao ACT Na Mama yao walivyokubali AACHANE NA CHADEMA
 
1. wakati unaingia kwenye uchaguzi ulijua kuwa tume siyo huru? akili yako na hao viongozi wako ilitakiwa ianzie hapo; kama tume siyo huru kuna haja gani ya uchaguzi?? kwa nn tusibadili kwanza tume kisha ndio tuingie kwenye chaguzi??

2. lowassa ndie aliyekuwepo mwaka 2010 wakati mlisema slaa kashinda! lowassa ndiye aliyemweka kikwete 2005 madarakani anajua kila kitu bwana mdogo, kila kitu!! sijamtaja sumaye na mwizi wa kura maarufu bwana kingunge ambao wote ni ukawa...hizi ni fugure kubwa sana

3. kwa nn CCM wamepata wabunge wengi? hauoni mnaji conttradict?? yaani wabunge wengi wa CCM...ambao hamlalamiki ila rais awe CDM

kaa chini fikiri, utamwona kila mtu mbaya..EL, SUMAYE NA KINGUNGE wanajua kila kitu na wangeweza ku intervene!! au waliamini CCM washakuwa malaika??kama wameshindwa hilo dogo....wangewezaje urais???

unataka kila mtu aseme lowassa kaibiwa kura

iwe kaibiwa au la; ni kuwa wamezidiana ujanja thats it!!

fanya kazi

Mkuu sidhan km unashirikisha vema ubongo wako
1. Yan ukatae kwnda kwny uchaguz kisa tume si huru? Harakat zilifanyika kupata tume huru kupitia katiba mpya lkn unajua nn kilijiri na hyo katiba ilipoishia kutokana na mfumo mbovu uliopo.
2. Kwa kusema kuwa lowassa,kingunge na sumaye kwa ss wako cdm so unatarajia waibe kura pia ili cdm ishinde? Kwa hyo kwa mtazamo wako uchaguz huu ilikua kwny kuiba kura na si kushnda kihalali?
3. Mtoa uzi ameeleza kuwa wizi umeanzia kwny ngaz ya ubunge na had udiwan pia.
4. Achana na uchaguz mkuu tu ccm wameibiana kura ht wao kwa wao kwny kura za maoni,km Nape ambaye ni kiongoz mwandamiz wa chama alituhumiwa kwa wizi kwny kura za maoni,leo unatetea kuwa hawa wameshnda kihalali ht pale ambapo ushahd upo? Shame..!
Inasikitisha si ww tu hata watu mitaan wanajisifu kwmb ccm ni mafia wanajua kushnda kwa hila/wizi,hiv mtu aliyeshnda kwa kuiba kura unataraj kesho atakutumikia kwa uadilif kwel?
 
Ibara number 41 ya katiba ya JMT inazungumzia uchaguzi wa raisi. Ninaomba wanasheria mtusaidie kupata ufafanuzi kifungu cha saba.

(6) Mgombea yeyote wa kiti cha Rais atatangazwa kuwaamechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata kura nyingi zaidikuliko mgombea mwingine yeyote.

(7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzikwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basihakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka yakuchunguza kuchaguliwa kwake.

Ufafanuzi ninaoumba ni kama tangazo la tume juu ya raisi litakuwa na kinga ya kutokuchunguzwa na mahakama yoyote hata pale ambapo maamuzi ya tangazo hilo hayajazingatia matakwa ya Ibara hii ya 41 mfano kama kifungu cha 6 ama chochote kikiwa kimekiukwa.

Kifungu cha saba kinasema wazi "Iwapo mgombea ametangazwa na tume ya uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa raisi kwa mujibu wa ibara hii (ya 41)". Vipi kama kilichotangazwa hakiko kwa mujibu wa ibara hii? Bado tangazo hilo ni legal binding?

Swali lingine, ni chombo gani kinatakiwa kuhakiki compliace ya tume ( iliyopewa nguvu hiyo kwenye) ili kujiridhisha kwamba inachokitangaza kimefanyika inline with stipulations za ibara hii ya 41?

Vipi ikitokea msemaji wa tume, on insanity, corruption, Rebellion, conspiracy, au threat grounds akamtangaza mtu kuwa raisi bila taratibu na mahitaji ya ibara hii ya 41 kufuatwa, bado itakuwa ni lawful, binding and enforceable announcement?

NAOMBA TUJADILIANE NA KUELEIMISHANA KWA HOJA. Na ni vizuri tukiwa tunarejea mfano wa kifungu cha sita hapo juu
 
Huwezi kujua uhalisia wa uhalali wa uchaguzi huu hadi uwe unajua kilichokuwa kinatendwa nyuma ya pazia!

Mbona mnatuaminisha kuwa kunakitu nyuma ya pazia kwanini msiweke ushahidi hapa tukaona hayo ya nyuma ya pazia!!!?? maana ukawa malamishi hamjaanza leo. Tumeshawazoea
 
Mkuu sidhan km unashirikisha vema ubongo wako
1. Yan ukatae kwnda kwny uchaguz kisa tume si huru? Harakat zilifanyika kupata tume huru kupitia katiba mpya lkn unajua nn kilijiri na hyo katiba ilipoishia kutokana na mfumo mbovu uliopo.
2. Kwa kusema kuwa lowassa,kingunge na sumaye kwa ss wako cdm so unatarajia waibe kura pia ili cdm ishinde? Kwa hyo kwa mtazamo wako uchaguz huu ilikua kwny kuiba kura na si kushnda kihalali?
3. Mtoa uzi ameeleza kuwa wizi umeanzia kwny ngaz ya ubunge na had udiwan pia.
4. Achana na uchaguz mkuu tu ccm wameibiana kura ht wao kwa wao kwny kura za maoni,km Nape ambaye ni kiongoz mwandamiz wa chama alituhumiwa kwa wizi kwny kura za maoni,leo unatetea kuwa hawa wameshnda kihalali ht pale ambapo ushahd upo? Shame..!
Inasikitisha si ww tu hata watu mitaan wanajisifu kwmb ccm ni mafia wanajua kushnda kwa hila/wizi,hiv mtu aliyeshnda kwa kuiba kura unataraj kesho atakutumikia kwa uadilif kwel?

Mzee wenu alianza kwa kuwaambia nyie mfanye kazi ya kumpigia kura na suala la kuzilinda mumuachie maana analimudu.
Baadae akabadilika, akawaambia mumpigie kura nyingi hata wakiiba zisitoshe kunyang'anya ushindi.
Mwishoni akabadilika tena na kuwataka mpige kura zenu na kuzilinda.
Siwezi kumlaumu hasa kwa kuzingatia hali ya afya yake, basi hata washauri wake!!
Umeongea kuhusu suala la ujanja kwenye zoezi la uhesabuji kura, ulisikia kuhusu watu 166 waliokamatwa kati yao wakiwa ni IT experts kutoka nje ya nchi? Je wewe uliwahi kuwasikia kabla hawajakamatwa?
Na ulijiuliza kwa nini viongozi wa Chadema waliweweseka sana baada ya tukio hilo, na unakumbuka maelezo yao?
Mpaka hapo hakuna wizi wa kura boss, matokeo ni halali na tafiti za awali mlizozipinga sana zinathibitisha hilo.
Chadema walijaribu kuiba kura kwa "bahati mbaya" hawakuweza wamebaki kulialia tu......
 
Kitila Mkumbo hebu fanya uchambuzi kuhusu matarajio na mafanikio ya chama chako cha ACT kwenye uchaguzi huu.
 
Last edited by a moderator:
Mimi huyu Kitila ananishangaza kwa mengi sana....
kinachonishangaza ni jinsi Zitto alivyo muamini huyu

Wote wanajua wanachofanya si zzk wala kitila.
Kila mtu kapewa kazi maalum kwa ajiri ya mwenzake
 
Mzee wenu alianza kwa kuwaambia nyie mfanye kazi ya kumpigia kura na suala la kuzilinda mumuachie maana analimudu.
Baadae akabadilika, akawaambia mumpigie kura nyingi hata wakiiba zisitoshe kunyang'anya ushindi.
Mwishoni akabadilika tena na kuwataka mpige kura zenu na kuzilinda.
Siwezi kumlaumu hasa kwa kuzingatia hali ya afya yake, basi hata washauri wake!!
Umeongea kuhusu suala la ujanja kwenye zoezi la uhesabuji kura, ulisikia kuhusu watu 166 waliokamatwa kati yao wakiwa ni IT experts kutoka nje ya nchi? Je wewe uliwahi kuwasikia kabla hawajakamatwa?
Na ulijiuliza kwa nini viongozi wa Chadema waliweweseka sana baada ya tukio hilo, na unakumbuka maelezo yao?
Mpaka hapo hakuna wizi wa kura boss, matokeo ni halali na tafiti za awali mlizozipinga sana zinathibitisha hilo.
Chadema walijaribu kuiba kura kwa "bahati mbaya" hawakuweza wamebaki kulialia tu......

Ukweli mchungu, wamezidiwa ujanja!!!
 
Back
Top Bottom