Kitila Mkumbo: Lowassa hana budi kukubali matokeo

Kitila nimemdharau jana nilipomuona
'anausafisha uchaguzi huu' akiwa BBC..
nimemdharau sana.....eti anakuja kusema TWAWEZA hawakukosea utafiti wao
results imeenda sawa sawa na TWAWEZA walivyo predict
nilibaki mdomo wazi

Kila anayetofautiana na nyie kimawazo lazima mumdharau. Hivi nyie jamaa mtabadilika lini, Inamaa mawazo yenu nyie tu ndio mazuri kuliko ya wengine?

Ifike mahali lazima muheshimu mawazo ya wengine kama yanavyoheshimiwa ya kwenu ingawa ni mawazo ya kipumbavu!!
 
Kama kuna wasomi ambao huwa nawaona bogus ni Kitila Mkumbo.Ni wale wasomi wanaoitwa wasomi uchwara ambao wanauza taaluma zao kwa fedha.

Wasomi huwa wana misimamo isiyo yumba.Huyu bwana ni kinyume kabisa.Yaani wana siasa wanamnunua kirahisi kweli.Shame on him.
Dar es Salaam. Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Kitila Mkumbo amesema aliyekuwa mgombea wa urais wa Chadema, Edward Lowassa, hana budi kukubali matokeo licha ya kupoteza nafasi hiyo.

Pia Profesa Mkumbo alisema mgombea huyo kisheria, hakuwa na haki ya kujitangaza mshindi wa nafasi ya urais katika uchaguzi wa mwaka huu.
Juzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilitangaza matokeo ya kura za urais zilipopingwa Jumapili, Oktoba 25 mwaka huu na kumtangaza mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli mshindi, lakini Lowassa siku hiyo pia alisema ameshinda katika uchaguzi kwa kura 10,268,795 sawa na asilimia 62 na kuitaka tume hiyo kumtangaza mshindi.

Profesa Mkumbo ambaye pia alipendekezwa na chama cha ACT- Wazalendo kugombea nafasi hiyo na kukataa, alisema Lowassa aliingia kwenye kinyang?anyoro hicho akifahamu kuwa tume ndiyo yenye mamlaka ya kumtangaza mshindi.

Alisema licha ya mchuano mkali kati yake na mgombea wa CCM anatakiwa kukubali matokeo.

?Hivyo Lowassa na wenzake wa Ukawa hawana msingi wowote wa kisheria au kisiasa kutangaza ushindi wenyewe. Walikubali kushiriki katika uchaguzi huu wakati wakifahamu kikamilifu kuwa NEC ndiyo yenye jukumu la kutangaza mshindi na mshindwa katika uchaguzi.?

Aliongeza: ?Zaidi ya hayo, takwimu za uchaguzi zinaeleza pia.?

Hata hivyo alisema katika uchaguzi huu ambao ni wa kihistoria kutokana na upinzania mkali kati ya CCM na upinzani tofauti na miaka ya nyuma, bado upinzani umepoteza nafasi ya ubunge licha ya kujinyakulia viti 76 huku CCM ikiwa na viti 188.

?Kupoteza viti hivyo ni ishara kwamba ushindi wa Lowassa haukuwa wa uhakika,?alisema Profesa Mkumbo na kuongeza;
?...nawashauri Ukawa kukubali kwamba Dk Magufuli ndiye rais mtaule wa awamu ya tano.

Wahakikishe wanashirikiana na kufanya kazi naye kazi kwa karibu katika kipindi chake cha miaka mitano ya uongozi.

Kwa namna hiyo wataweza kuwa chachu ya kupata Katiba Mpya itakayowezesha kubadili mazingira ya kikatiba na kisheria katika uchaguzi ujao.?
 
Kitila na Francis walikuwa viongozi wa DARUSO pindi walipokuwa chuo kikuu Dares Salaam. Kila migomo ilipotokea walijifanya wapo upande wa wanafunzi na baadae wanawageuka ghafra! sijajua uprofessor aliupataje!
 
Na huyu ni POLEPOLE MWINGINE AKIWA KATIKA HARAKATI ZA KUUSAKA UKUU WA WILAYA NA UBUNGE WA KUTEULIWA,NAFIKIRI ISHU HAPO SIO PROF.KITILA KAONGEA...YANI ATA AJE OBAMA HAELEWEKI HADI HAKI IPATIKANE KWA KWELI,No Comment!!!

atapewa ubunge wa kuteuliwa kama mbatia
 
Dar es Salaam. Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Kitila Mkumbo amesema aliyekuwa mgombea wa urais wa Chadema, Edward Lowassa, hana budi kukubali matokeo licha ya kupoteza nafasi hiyo.

Pia Profesa Mkumbo alisema mgombea huyo kisheria, hakuwa na haki ya kujitangaza mshindi wa nafasi ya urais katika uchaguzi wa mwaka huu.
Juzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilitangaza matokeo ya kura za urais zilipopingwa Jumapili, Oktoba 25 mwaka huu na kumtangaza mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli mshindi, lakini Lowassa siku hiyo pia alisema ameshinda katika uchaguzi kwa kura 10,268,795 sawa na asilimia 62 na kuitaka tume hiyo kumtangaza mshindi.

Profesa Mkumbo ambaye pia alipendekezwa na chama cha ACT- Wazalendo kugombea nafasi hiyo na kukataa, alisema Lowassa aliingia kwenye kinyang?anyoro hicho akifahamu kuwa tume ndiyo yenye mamlaka ya kumtangaza mshindi.

Alisema licha ya mchuano mkali kati yake na mgombea wa CCM anatakiwa kukubali matokeo.

?Hivyo Lowassa na wenzake wa Ukawa hawana msingi wowote wa kisheria au kisiasa kutangaza ushindi wenyewe. Walikubali kushiriki katika uchaguzi huu wakati wakifahamu kikamilifu kuwa NEC ndiyo yenye jukumu la kutangaza mshindi na mshindwa katika uchaguzi.?

Aliongeza: ?Zaidi ya hayo, takwimu za uchaguzi zinaeleza pia.?

Hata hivyo alisema katika uchaguzi huu ambao ni wa kihistoria kutokana na upinzania mkali kati ya CCM na upinzani tofauti na miaka ya nyuma, bado upinzani umepoteza nafasi ya ubunge licha ya kujinyakulia viti 76 huku CCM ikiwa na viti 188.

?Kupoteza viti hivyo ni ishara kwamba ushindi wa Lowassa haukuwa wa uhakika,?alisema Profesa Mkumbo na kuongeza;
?...nawashauri Ukawa kukubali kwamba Dk Magufuli ndiye rais mtaule wa awamu ya tano.

Wahakikishe wanashirikiana na kufanya kazi naye kazi kwa karibu katika kipindi chake cha miaka mitano ya uongozi.

Kwa namna hiyo wataweza kuwa chachu ya kupata Katiba Mpya itakayowezesha kubadili mazingira ya kikatiba na kisheria katika uchaguzi ujao.?

ETI PROFESA KITILA!KAZI KWELIKWELI,na hayo ndio maoni yake,hovyo kabisa,Kitila soma historia.
 
Back
Top Bottom