Kitila Mkumbo: Lowassa hana budi kukubali matokeo

Kitila Mkumbo: Lowassa hana budi kukubali matokeo

Kitila nimemdharau jana nilipomuona
'anausafisha uchaguzi huu' akiwa BBC..
nimemdharau sana.....eti anakuja kusema TWAWEZA hawakukosea utafiti wao
results imeenda sawa sawa na TWAWEZA walivyo predict
nilibaki mdomo wazi

Yaani huu uzi watu wawili mmeamua kudiscus maisha ya mtu..

Acheni tabia za kike
 
Nimejiuliza kama hata TV alikuwa anatazama
manake dosari zingine zilikuwa too much..
anajidharaulisha...alipaswa kutumia taaluma yake kutetea the weak
sio kutetea dola

Kwa sababu aliamua kuwa kwa side of an oppressor basi hayo kwake yalikuwa the so called dosari ndogo ndogo... japokuwa hizo hizo zime nullify Zanzibar election. He is just a Coward.
 
nchi hii inatatizo la unafkizesheni, umbea, unafiki, na kujipendekeza ndiyo sifa kuu za wasomi baadhitulio nao.

Kama leo pale diamond jubilee, nimemwona dkt ave maria, akikata mauno pale, sikujua kumbe nae ni gamba!
 
Huyo Ave Maria ni gamba hatari,hata wakati wa katiba ya warioba,Ave Maria alikuwa akizunguka media mbalimbali kuwashambulia UKAWA! Ni mpuuzi flani kama Dr.Banna
 
Dar es Salaam. Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Kitila Mkumbo amesema aliyekuwa mgombea wa urais wa Chadema, Edward Lowassa, hana budi kukubali matokeo licha ya kupoteza nafasi hiyo.
Pia Profesa Mkumbo alisema mgombea huyo kisheria, hakuwa na haki ya kujitangaza mshindi wa nafasi ya urais katika uchaguzi wa mwaka huu.
Juzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilitangaza matokeo ya kura za urais zilipopingwa Jumapili, Oktoba 25 mwaka huu na kumtangaza mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli mshindi, lakini Lowassa siku hiyo pia alisema ameshinda katika uchaguzi kwa kura 10,268,795 sawa na asilimia 62 na kuitaka tume hiyo kumtangaza mshindi.
Profesa Mkumbo ambaye pia alipendekezwa na chama cha ACT- Wazalendo kugombea nafasi hiyo na kukataa, alisema Lowassa aliingia kwenye kinyang?anyoro hicho akifahamu kuwa tume ndiyo yenye mamlaka ya kumtangaza mshindi.
Alisema licha ya mchuano mkali kati yake na mgombea wa CCM anatakiwa kukubali matokeo.
?Hivyo Lowassa na wenzake wa Ukawa hawana msingi wowote wa kisheria au kisiasa kutangaza ushindi wenyewe. Walikubali kushiriki katika uchaguzi huu wakati wakifahamu kikamilifu kuwa NEC ndiyo yenye jukumu la kutangaza mshindi na mshindwa katika uchaguzi.?
Aliongeza: ?Zaidi ya hayo, takwimu za uchaguzi zinaeleza pia.?
Hata hivyo alisema katika uchaguzi huu ambao ni wa kihistoria kutokana na upinzania mkali kati ya CCM na upinzani tofauti na miaka ya nyuma, bado upinzani umepoteza nafasi ya ubunge licha ya kujinyakulia viti 76 huku CCM ikiwa na viti 188.
?Kupoteza viti hivyo ni ishara kwamba ushindi wa Lowassa haukuwa wa uhakika,?alisema Profesa Mkumbo na kuongeza;
?...nawashauri Ukawa kukubali kwamba Dk Magufuli ndiye rais mtaule wa awamu ya tano. Wahakikishe wanashirikiana na kufanya kazi naye kazi kwa karibu katika kipindi chake cha miaka mitano ya uongozi. Kwa namna hiyo wataweza kuwa chachu ya kupata Katiba Mpya itakayowezesha kubadili mazingira ya kikatiba na kisheria katika uchaguzi ujao.?
Ameonyesha ukomavu wa kisiasa na ameongea kama msomi na mpenda amani. shida iko kwa wana UKAWA hawatamuelewa zaidi ya kumtusi na kumpa majina mengi ya ajabu ajabu but ameongea ukweli mchungu. wanaojua ukweli wa kilichokuwa kwenye mabox ya kura ni mawakala, waliobaki wanaendeshwa na hisia na kuburuzwa na utashi wa waliotegemea urais.
 
Yaani very coward....
anaitetea CCM kwa price hata ya kuipuuza ACT
sasa unashangaa...
Mara mtafiti..mara mchambuzi mara mwanasiasa....

Huwezi kuvaa kofia zote hizi. Ni lazima utaharibu. Sasa mtu kama huyu alikuwa sehemu ya "utafiti" wa Twaweza. Very subjective. Anachofanya Kitila kimenikumbusha kitabu cha Roger Pielke kiitwacho The Honest Broker. Kitila is not a honest broker.
 
Huyo Kitila hana lolote pamoja na usomi wa chuo nilitegemea unaweza kutusaidia kimawazo. Unachuki za kike yaani kwakua mgombea ni wa CHADEMA kuhujumiwa kwake ndio furaha kwako hata point unazotoa haziendani kuhusu CCM kupata wabunge wengi. unataka kuniambia kungekuwa na mgombea binafsi itakuwa hawezi kupata kura.Kwanza hapo tu mnaonesha ACT ni tawi la CCM
 
Huwezi kuvaa kofia zote hizi. Ni lazima utaharibu. Sasa mtu kama huyu alikuwa sehemu ya "utafiti" wa Twaweza. Very subjective. Anachofanya Kitila kimenikumbusha kitabu cha Roger Pielke kiitwacho The Honest Broker. Kitila is not a honest broker.

Yaani anajipa kazi ya kuitete TWAWEZA
as if hajui kuwa utafiti ulikuwa magumashi
sasa anajipa kazi ya kuiuza ACT huku maneno yake kama mtafiti yanaiua hiyo ACT
 
Namsupport Kitila. lowas na kingunge waliipinga rasimu ya jajibWarioba, leo hii imekuja kuwachinja hao hao na iwe fundisho kwa wanasiasa wengine wote.
 
Dar es Salaam. Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Kitila Mkumbo amesema aliyekuwa mgombea wa urais wa Chadema, Edward Lowassa, hana budi kukubali matokeo licha ya kupoteza nafasi hiyo.
Pia Profesa Mkumbo alisema mgombea huyo kisheria, hakuwa na haki ya kujitangaza mshindi wa nafasi ya urais katika uchaguzi wa mwaka huu.
Juzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilitangaza matokeo ya kura za urais zilipopingwa Jumapili, Oktoba 25 mwaka huu na kumtangaza mgombea wa

tatizo ni kwamba tofauti ya kura alizopata ni KUUUUBWA sana, kama ingekuwa laki mbili, tatu hata mimi ningeongea tofauti.

Ni kama mtaka yote hivi. Anafuata upepo unakoelekea na hiyo inamuondolea credibility hata wakati mwingine huwa na question mienendo yake.

Mfano niliwah kukutana naye Mlimani city akisoma gazeti la Tanzania daima enzi zile Lowassa kaingia Chadema akasema anamuunga mkono kwa asilimia zote na anaamini anafaa kuwa Rais.

Today is different story na huenda akakana kabisa maneno yake yale.

Tatizo lenu hamtaki kuambiwa ukweli Prof Kitila amesema ukweli mliingia kwenye uchaguzi wakati mkijua kuwa tume ya taifa ya uchaguzi ndiyo yenye mamlaka ya kumtangaza mshindi kuanzia ngazi ya udiwani, ubunge na urais mbona ubunge mmekubali wakati iliyotangaza ni tume hiyohiyo? CCM wana viti 188 na wanywa viroba 76 ushindi wenu uko wapi majuha nyie acheni kuleta upumbavu wenu hapa mnapoteza muda wetu kuhbiri ujinga hivi hata kama una matope kichwani kama ya EL unaweza kudai ushindi wakati una viti 76 na mwenzako 188? Vitu vingine mnatia aibu kila siku mnaonewa mwaka 2010 mlisema mmeonewa na Rais hamkumtambua sasa ilikuwaje mkakubali kuingia kwenye uchaguzi wakati hamna imani na tume? Na kama ni tume mbovu kwa mujibu wa ujinga wenu kataeni hata hivyo viti vya ubunge navyo siyo halali kwakuwa imetangaza tume hiyohiyo mnayichukia. Tumechoka kumsikiliza Lowasa ngonjera zake atuache tufanye kazi za kuendeleza familia zetu yeye ana mabilioni ya kuchezea sisi anatutia umasikini kutokana na malalamiko yake.

Ametoka CCM analalama eti kaonewa utadhani yeye ana hati milki ya kuteuliwa kuwa mgombea Urais amekwenda kununua CHADEMA nako akadhani atashinda kwa kununua Urais, lakini bahati haikuwa yake nako amenoa analalamika, tena mwambieni ajitazame upya ana kasoro gani kila aendako hakubaliki?

ASIWE MTU WA KULALAMIKA TOKA 1995 DEAL LA URAIS LILIGOMA AKALALAMIKA NYERERE KAMUONEA AKAPEWA UWAZIRI MKUU NA AKAFUKUZWA KAZI KWA MUDA MFUPI TU NAKO AKALIA BUNGENI AMEONEWA, IKAJA UTEUZI WA MGOMBEA WA CCM AKAKATWA NAKO AKALIA AMEONEWA AKAKIMBILIA CHADEMA, NAKO TUME IMEMUONEA, HUYU HAFAI KUWA RAIS NA AKILAZIMISHA YATAMKUTA MKUBWA KWANI HANA NYOTA YA UTAWALA ASILAZIMISHE MAISHA BILA URAIS YANAWEZEKANA.

UONGOZI HUTOKA KWA MUNGU N SIYO KWA PESA KAMA ANAVYODHANI . ICC KINA TUNDU LISU WANAKWENDA KUUZA SURA KWAKUWA WANA MKAKATI WA KUHAKIKISHA ILE PESA YA RICMOND WANAKOMBA YOTE NA KISHA WAMWACHE KWENYE MATAA MALI YA MJINGA HULIWA NA WAJANJA ALIZOMPA MBOWE HAJAKTA TAMAA TU WACHA NA KINA LISU NAO WALE ZAO.

Dr Magufuli aliwaambia kuwa hajawahi kugombea uongozi akashindwa kabla hata kampeni hazijaanza na matokeo mumeyaona huyo kilaza wenu anababaika mara huku mara kule hajijui tu ana nyota ya mkasi kila aendako atakatwa tu hakuna namna.
 
Ameonyesha ukomavu wa kisiasa na ameongea kama msomi na mpenda amani. shida iko kwa wana UKAWA hawatamuelewa zaidi ya kumtusi na kumpa majina mengi ya ajabu ajabu but ameongea ukweli mchungu. wanaojua ukweli wa kilichokuwa kwenye mabox ya kura ni mawakala, waliobaki wanaendeshwa na hisia na kuburuzwa na utashi wa waliotegemea urais.
Tusubiri ila ninavyojua Prof Mkumbo ni mtaalam wa mambo ya elimu kuliko siasa na sheria!
 
Nimemfuatilia Profesa Kitila kwa muda mrefu, naona alikiwa kwenye mkakati wa kuhakikisha Magufuli anashinda
 
Tatizo lenu hamtaki kuambiwa ukweli Prof Kitila amesema ukweli mliingia kwenye uchaguzi wakati mkijua kuwa tume ya taifa ya uchaguzi ndiyo yenye mamlaka ya kumtangaza mshindi kuanzia ngazi ya udiwani, ubunge na urais mbona ubunge mmekubali wakati iliyotangaza ni tume hiyohiyo? CCM wana viti 188 na wanywa viroba 76 ushindi wenu uko wapi majuha nyie acheni kuleta upumbavu wenu hapa mnapoteza muda wetu kuhbiri ujinga hivi hata kama una matope kichwani kama ya EL unaweza kudai ushindi wakati una viti 76 na mwenzako 188? Vitu vingine mnatia aibu kila siku mnaonewa mwaka 2010 mlisema mmeonewa na Rais hamkumtambua sasa ilikuwaje mkakubali kuingia kwenye uchaguzi wakati hamna imani na tume? Na kama ni tume mbovu kwa mujibu wa ujinga wenu kataeni hata hivyo viti vya ubunge navyo siyo halali kwakuwa imetangaza tume hiyohiyo mnayichukia. Tumechoka kumsikiliza Lowasa ngonjera zake atuache tufanye kazi za kuendeleza familia zetu yeye ana mabilioni ya kuchezea sisi anatutia umasikini kutokana na malalamiko yake.

Ametoka CCM analalama eti kaonewa utadhani yeye ana hati milki ya kuteuliwa kuwa mgombea Urais amekwenda kununua CHADEMA nako akadhani atashinda kwa kununua Urais, lakini bahati haikuwa yake nako amenoa analalamika, tena mwambieni ajitazame upya ana kasoro gani kila aendako hakubaliki?

ASIWE MTU WA KULALAMIKA TOKA 1995 DEAL LA URAIS LILIGOMA AKALALAMIKA NYERERE KAMUONEA AKAPEWA UWAZIRI MKUU NA AKAFUKUZWA KAZI KWA MUDA MFUPI TU NAKO AKALIA BUNGENI AMEONEWA, IKAJA UTEUZI WA MGOMBEA WA CCM AKAKATWA NAKO AKALIA AMEONEWA AKAKIMBILIA CHADEMA, NAKO TUME IMEMUONEA, HUYU HAFAI KUWA RAIS NA AKILAZIMISHA YATAMKUTA MKUBWA KWANI HANA NYOTA YA UTAWALA ASILAZIMISHE MAISHA BILA URAIS YANAWEZEKANA.

UONGOZI HUTOKA KWA MUNGU N SIYO KWA PESA KAMA ANAVYODHANI . ICC KINA TUNDU LISU WANAKWENDA KUUZA SURA KWAKUWA WANA MKAKATI WA KUHAKIKISHA ILE PESA YA RICMOND WANAKOMBA YOTE NA KISHA WAMWACHE KWENYE MATAA MALI YA MJINGA HULIWA NA WAJANJA ALIZOMPA MBOWE HAJAKTA TAMAA TU WACHA NA KINA LISU NAO WALE ZAO.
Siamini kama una haja ya kuendelea kumsikiliza kwa kuwa anakucheleweshea maendeleo wewe na familia yako, la maana ni kuendelea tu, kama una duka lako amka asubuhi na mapema nenda kauze ukitaka hata vichwa vya habari vya magazeti usisikiliza...usimtuhumu kwa kulalama wakati nawe unalalama ndo ushauri wangu
 
Makelele ya siasa yanaathiri waliomo na wasiokuwemo hilo ndiyo tatizo ingekuwa niko kisiwani nisikochanganyika na watanzania wenzangu hilo unalosema lingefaa, lakini siwezi kujitenga na jamii na hilo ndiyo tatizo kubwa tumekuwa na mambo ya siasa zaidi ya miezi miwili lakini tena sasa hivi mnataka turudi kulekule kumbuka hata kusikiliza mikutano ya kampeni ilikuwa ni wajibu wa mpiga kura na hata ukibaki dukani peke yako bado huna utakachouza kwakuwa watu wote wako kwenye mikutano ya kampeni nadhani mpaka hapo umeelewa ubaya wa kelele za Lowasa na genge lake utakavyo athiri uchumi wa Taifa letu uchaguzi umeshakwisha tujenge nchi yetu upya na rais mpya makelele na kulalama hakutatusaidia lolote ng'ooooooooo.
 
Dk Kitila, imefikia wakati iwapo huwezi kuchambua mambo kisomi ukae kimya na sio kudhalilisha uprofesa wako na kuonekana mtu wa njaa badala ya taaluma. Nimekuwa nakufuatilia hoja zako tangu utoke CHADEMA hoja zako dhidi ya chama kile ziko kinjaa zaidi ya kisomi ukijaribu kuibeza CHADEMA bila vigezo vya kisomi wala Critical Thinking bali kushabikia upande wa CCM au wowote ule ulio rival na CHADEMA

Nimesoma habari zako kwenye gazeti la Mwananchi ukibeza Lowassa kujitangaza ushindi siko katika Lowassa kujitangaza ushindi bali nipo kwenye uchambuzi wako uko mweupe hauna uhalisia kwa kuangalia matokea ya Tume kisha kumtaka Lowassa akubali kashindwa maana number zinakubaliana na ushindi wa Magufuli

Dk Kitila kumbuka kwamba uchaguzi huu haukuwa na Tume Huru kwahiyo anything possible chama tawala kucheza rafu na kujipa ushindi, rafu hizi huchezwa kitaalamu kuanzia chini kwa wabunge ili kwenye urais waweze kuhalalisha kuwa walishinda kihalali. Kwa kudispute kauli yako kutolea mfano wa wabunge naweza sema Mwakyembe(Kyela) Mabula (Mwanza), Sauli (Tukuyu) hawa ni moja ya wabunge ambao hawajashinda kihalali na namba kama hii ni kubwa zaidi ya 60, hii ni katika mbinu za chama tawala kujihalalisha kuwa kilishinda kihalali angalia matokeao ya awali yalivyoyangazwa kisha wakagomea na kujikuta washindi ukizingatia msimamizi mkuu wa uchaguzi majimboni ni Mkurungezi wa wilaya anayefanya kazi kwa niaba ya CCM.

Hata madikteta kama Hosni Mubarak walikuwa wakishinda kwa zaidi ya 85% kwenye chaguzi zao lakini baada ya kutolewa madarakani kwa mapinduzi vyama vyao havikufikisha 10% ya kura kwahiyo usijaribu kubeza wenzio kwa sababu nyepesinyepesi, nakuuliza swali iwapo uchaguzi ulikuwa wa Huru na Haki kwanini polisi walivamia KItuo cha CHADEMA cha kukusanyia kura? Jambo ambalo ni haki katika chaguzi huru? Kwanini polisi walivamia kituo cha Haki za Binadamu kilichokuwa kinakusanya kura kama NEC? Jibu ni kwamba chama tawala kiliogopa kuumbuliwa wizi wake wa waziwazi maana namba za Tume na wengine zisingefanana. Na ulizo la ziada kwanini CCM ilitumia nguvu nyingi kupinga Tume Huru ya Uchaguzi iwapo hushinda kihalali?

Mwisho hakujawahi kuwa na uchaguzi Tanzania wenye ushindani kama huu na matokea ya Tume hayaonyeshi uhalisia wa ushindani uliokuwepo nchini na kwa kukupa ushahidi tangu Magufuli atangzwe nchi iko kimya kama imepata msiba maana watu wanasense kuna kitu kilifanyika ambacho si halali. Miaka yote akitangazwa mshindi wa CCM wananchi huendelea na shughuli zao kama kawaida lakini si uchaguzi huu. Dk Kitila tumia zaidi taaluma na akili sio ushabiki usio na maana
 
Back
Top Bottom