Kitila Mkumbo: Lowassa hana budi kukubali matokeo

Kitila Mkumbo: Lowassa hana budi kukubali matokeo

Paul Alex

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2012
Posts
4,346
Reaction score
9,846
Dar es Salaam. Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Kitila Mkumbo amesema aliyekuwa mgombea wa urais wa Chadema, Edward Lowassa, hana budi kukubali matokeo licha ya kupoteza nafasi hiyo.

Pia Profesa Mkumbo alisema mgombea huyo kisheria, hakuwa na haki ya kujitangaza mshindi wa nafasi ya urais katika uchaguzi wa mwaka huu.
Juzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilitangaza matokeo ya kura za urais zilipopingwa Jumapili, Oktoba 25 mwaka huu na kumtangaza mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli mshindi, lakini Lowassa siku hiyo pia alisema ameshinda katika uchaguzi kwa kura 10,268,795 sawa na asilimia 62 na kuitaka tume hiyo kumtangaza mshindi.

Profesa Mkumbo ambaye pia alipendekezwa na chama cha ACT- Wazalendo kugombea nafasi hiyo na kukataa, alisema Lowassa aliingia kwenye kinyang?anyoro hicho akifahamu kuwa tume ndiyo yenye mamlaka ya kumtangaza mshindi.

Alisema licha ya mchuano mkali kati yake na mgombea wa CCM anatakiwa kukubali matokeo.

?Hivyo Lowassa na wenzake wa Ukawa hawana msingi wowote wa kisheria au kisiasa kutangaza ushindi wenyewe. Walikubali kushiriki katika uchaguzi huu wakati wakifahamu kikamilifu kuwa NEC ndiyo yenye jukumu la kutangaza mshindi na mshindwa katika uchaguzi.?

Aliongeza: ?Zaidi ya hayo, takwimu za uchaguzi zinaeleza pia.?

Hata hivyo alisema katika uchaguzi huu ambao ni wa kihistoria kutokana na upinzania mkali kati ya CCM na upinzani tofauti na miaka ya nyuma, bado upinzani umepoteza nafasi ya ubunge licha ya kujinyakulia viti 76 huku CCM ikiwa na viti 188.

?Kupoteza viti hivyo ni ishara kwamba ushindi wa Lowassa haukuwa wa uhakika,?alisema Profesa Mkumbo na kuongeza;
?...nawashauri Ukawa kukubali kwamba Dk Magufuli ndiye rais mtaule wa awamu ya tano.

Wahakikishe wanashirikiana na kufanya kazi naye kazi kwa karibu katika kipindi chake cha miaka mitano ya uongozi.

Kwa namna hiyo wataweza kuwa chachu ya kupata Katiba Mpya itakayowezesha kubadili mazingira ya kikatiba na kisheria katika uchaguzi ujao.?
 
Wanywa virobo (kwa mujibu wa kilaza Kikwete) wanaweza kushiriki kwenye kujenga nchi?
 
Huwezi kujua uhalisia wa uhalali wa uchaguzi huu hadi uwe unajua kilichokuwa kinatendwa nyuma ya pazia!
 
Mimi huyu Kitila ananishangaza kwa mengi sana....
kinachonishangaza ni jinsi Zitto alivyo muamini huyu
 
Mimi huyu Kitila ananishangaza kwa mengi sana....
kinachonishangaza ni jinsi Zitto alivyo muamini huyu

Jamaa huwa ana sura mbili au zaid. Leo anaongea kama Kitila, kesho anaongea kama mtaalam mchambuzi, keshokutwa anaongea kama ACT.
Wakati mwingine huwa simuelewi mantiki ya hoja zake.
 
Jamaa huwa ana sura mbili au zaid. Leo anaongea kama Kitila, kesho anaongea kama mtaalam mchambuzi, keshokutwa anaongea kama ACT.
Wakati mwingine huwa simuelewi mantiki ya hoja zake.

Yaani very coward....
anaitetea CCM kwa price hata ya kuipuuza ACT
sasa unashangaa...
Mara mtafiti..mara mchambuzi mara mwanasiasa....
 
Yaani very coward....
anaitetea CCM kwa price hata ya kuipuuza ACT
sasa unashangaa...
Mara mtafiti..mara mchambuzi mara mwanasiasa....

Sometimes huwa nawaza kuwa mabadiliko ya kweli yataletwa baada ya kizazi cha chama kimoja kutoweka. Kizazi cha vyama vingi kinaweza kuleta changamoto. Ni kama puppet wa kitengo ndani ya upinzan kwa ujumla.
 
Huyu jamaa ni miongoni mwa wasomi wengi leo walioamua kwa makusudi kabisa kufukia elimu zao kwenye kifusi cha usakatonge!!
 
Sometimes huwa nawaza kuwa mabadiliko ya kweli yataletwa baada ya kizazi cha chama kimoja kutoweka. Kizazi cha vyama vingi kinaweza kuleta changamoto. Ni kama puppet wa kitengo ndani ya upinzan kwa ujumla.

Shida ya Kitila ni kutaka yote
anataka abaki mkuu wa idara chuoni kwake
anataka kualikwa kama mchambuzi kwenye media
na still anataka opportunity za kisiasa kupitia ACT
 
Shida ya Kitila ni kutaka yote
anataka abaki mkuu wa idara chuoni kwake
anataka kualikwa kama mchambuzi kwenye media
na still anataka opportunity za kisiasa kupitia ACT

Ni kama mtaka yote hivi. Anafuata upepo unakoelekea na hiyo inamuondolea credibility hata wakati mwingine huwa na question mienendo yake.

Mfano niliwah kukutana naye Mlimani city akisoma gazeti la Tanzania daima enzi zile Lowassa kaingia Chadema akasema anamuunga mkono kwa asilimia zote na anaamini anafaa kuwa Rais.

Today is different story na huenda akakana kabisa maneno yake yale.
 
Ni kama mtaka yote hivi. Anafuata upepo unakoelekea na hiyo inamuondolea credibility hana wakati mwingine huwa na question mienendo yake.

Mfano niliwah kukutana naye Mlimani city akisoma gazeti la Tanzania daima enzi zile Lowassa kaingia Chadema akasema anamuunga mkono kwa asilimia zote na anaamini anafaa kuwa Rais.

Today is different story na huenda akakana kabisa maneno yake yale.

Anapenda kuaminika kotekote
naona ili aweze ku influence kitu...
binafsi naona huwezi kuwa 'mchambuzi huru' wa siasa za TZ
halfu ukawa mwanachama wa chama chako na kiongozi pia
 
Anapenda kuaminika kotekote
naona ili aweze ku influence kitu...
binafsi naona huwezi kuwa 'mchambuzi huru' wa siasa za TZ
halfu ukawa mwanachama wa chama chako na kiongozi pia

Haswaaa kitu ambacho ni kigumu sana kutokea. Huwez kuwa pande zote ukawa mkweli hata siku moja.

He is revealing his true colours once again. Angebaki na u hazili wake tu basi. Asije akapata matatizo na huko ACT pia. Maana wao wanasimamia the so called Misingi.
 
Kitila nimemdharau jana nilipomuona
'anausafisha uchaguzi huu' akiwa BBC..
nimemdharau sana.....eti anakuja kusema TWAWEZA hawakukosea utafiti wao
results imeenda sawa sawa na TWAWEZA walivyo predict
nilibaki mdomo wazi
 
Another day in time upepo ukibadilika utamuona tena anavyobadilika hadi unaweza kumdharau kabisa. Hata media zinazompa airtime nahisi huwa wanakuwa wamekosa wachambuzi makini.
 
Hivi mbona kitilla ni yeye tu ndio anajua kila jambo? Huko hamna maprofesa wengine vimbelembele ama ana shida gan
 
Another day in time upepo ukibadilika utamuona tena anavyobadilika hadi unaweza kumdharau kabisa. Hata media zinazompa airtime nahisi huwa wanakuwa wamekosa wachambuzi makini.

Nimejiuliza kama hata TV alikuwa anatazama
manake dosari zingine zilikuwa too much..
anajidharaulisha...alipaswa kutumia taaluma yake kutetea the weak
sio kutetea dola
 
Back
Top Bottom