Mkuu umehoji mambo ya msingi sn,lkn ombi langu kwako ni ungepost uzi mpya ili ipate uzito halis kulingana na hoja yako,otherwise hoja hii inamezwa humu.Ibara number 41 ya katiba ya JMT inazungumzia uchaguzi wa raisi. Ninaomba wanasheria mtusaidie kupata ufafanuzi kifungu cha saba.
(6) Mgombea yeyote wa kiti cha Rais atatangazwa kuwaamechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata kura nyingi zaidikuliko mgombea mwingine yeyote.
(7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzikwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basihakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka yakuchunguza kuchaguliwa kwake.
Ufafanuzi ninaoumba ni kama tangazo la tume juu ya raisi litakuwa na kinga ya kutokuchunguzwa na mahakama yoyote hata pale ambapo maamuzi ya tangazo hilo hayajazingatia matakwa ya Ibara hii ya 41 mfano kama kifungu cha 6 ama chochote kikiwa kimekiukwa.
Kifungu cha saba kinasema wazi "Iwapo mgombea ametangazwa na tume ya uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa raisi kwa mujibu wa ibara hii (ya 41)". Vipi kama kilichotangazwa hakiko kwa mujibu wa ibara hii? Bado tangazo hilo ni legal binding?
Swali lingine, ni chombo gani kinatakiwa kuhakiki compliace ya tume ( iliyopewa nguvu hiyo kwenye) ili kujiridhisha kwamba inachokitangaza kimefanyika inline with stipulations za ibara hii ya 41?
Vipi ikitokea msemaji wa tume, on insanity, corruption, Rebellion, conspiracy, au threat grounds akamtangaza mtu kuwa raisi bila taratibu na mahitaji ya ibara hii ya 41 kufuatwa, bado itakuwa ni lawful, binding and enforceable announcement?
NAOMBA TUJADILIANE NA KUELEIMISHANA KWA HOJA. Na ni vizuri tukiwa tunarejea mfano wa kifungu cha sita hapo juu
Mimi huyu Kitila ananishangaza kwa mengi sana....
kinachonishangaza ni jinsi Zitto alivyo muamini huyu
Dar es Salaam. Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Kitila Mkumbo amesema aliyekuwa mgombea wa urais wa Chadema, Edward Lowassa, hana budi kukubali matokeo licha ya kupoteza nafasi hiyo.
Pia Profesa Mkumbo alisema mgombea huyo kisheria, hakuwa na haki ya kujitangaza mshindi wa nafasi ya urais katika uchaguzi wa mwaka huu.
Juzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilitangaza matokeo ya kura za urais zilipopingwa Jumapili, Oktoba 25 mwaka huu na kumtangaza mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli mshindi, lakini Lowassa siku hiyo pia alisema ameshinda katika uchaguzi kwa kura 10,268,795 sawa na asilimia 62 na kuitaka tume hiyo kumtangaza mshindi.
Profesa Mkumbo ambaye pia alipendekezwa na chama cha ACT- Wazalendo kugombea nafasi hiyo na kukataa, alisema Lowassa aliingia kwenye kinyang?anyoro hicho akifahamu kuwa tume ndiyo yenye mamlaka ya kumtangaza mshindi.
Alisema licha ya mchuano mkali kati yake na mgombea wa CCM anatakiwa kukubali matokeo.
?Hivyo Lowassa na wenzake wa Ukawa hawana msingi wowote wa kisheria au kisiasa kutangaza ushindi wenyewe. Walikubali kushiriki katika uchaguzi huu wakati wakifahamu kikamilifu kuwa NEC ndiyo yenye jukumu la kutangaza mshindi na mshindwa katika uchaguzi.?
Aliongeza: ?Zaidi ya hayo, takwimu za uchaguzi zinaeleza pia.?
Hata hivyo alisema katika uchaguzi huu ambao ni wa kihistoria kutokana na upinzania mkali kati ya CCM na upinzani tofauti na miaka ya nyuma, bado upinzani umepoteza nafasi ya ubunge licha ya kujinyakulia viti 76 huku CCM ikiwa na viti 188.
?Kupoteza viti hivyo ni ishara kwamba ushindi wa Lowassa haukuwa wa uhakika,?alisema Profesa Mkumbo na kuongeza;
?...nawashauri Ukawa kukubali kwamba Dk Magufuli ndiye rais mtaule wa awamu ya tano. Wahakikishe wanashirikiana na kufanya kazi naye kazi kwa karibu katika kipindi chake cha miaka mitano ya uongozi. Kwa namna hiyo wataweza kuwa chachu ya kupata Katiba Mpya itakayowezesha kubadili mazingira ya kikatiba na kisheria katika uchaguzi ujao.?
Usitaraji kupata uchambuzi wenye afya kipindi hiki.watu wako na harakati za kujikomba waambulie nafasi kuramba viatu vya mzee.ukuu wa vitengo ndugu......!!
Mkuu Umenena vyema,WATU HAWAJAMSOMA HUYU PROF.KITILA UKWELI NI KUWA JAMAA ANATAFUTA UBUNGE WA KUTEULIWA...Obviously Known!!!
Unawezaje kuwa mchambuzi 'huru' na mshindani katika vyama wakati huo huo bila kuathiriwa na mapenzi ya chama chako au wafadhili wako? Kitila Mkumbo ni kada wa ACT lakini anajifanya mchambuzi huru. Mkumbo alishiriki katika mojawapo ya zile oipnion polls zilizomtabiria Magufuli ushindi wa kishindo akiwa amejipachika Twaweza. Kwa hiyo anawajibika kutetea matokeo. Chambuzi za Mkumbo mara nyingi zinalenga kuiponda Chadema (na kusifia CCM) kuliko hata kuijenga ACT yake. Kwa kawaida ya nchi hii mtu hawezi kuwa mpinzani na akaendelea kuwa mtumishi kwenye taasisi ta kiserikali. Lakini mpinzani Mkumbo bado yuko UDSM ukilinganisha na wenzake waliokuwa kwenye vyama nuksi. Kwa hiyo haishangazi hata mgombea urais wao wa ACT kaonyesha kuridhishwa na mchakato na matokeo ya uchaguzi. Hata kama angejua kuwa kura zake zimepunguzwa ili kujazia kwa upande mwengine ninahisi lisingekuwa tatizo. Huwezi kukata mkono unaokulisha. Kuna wapinzani na wapinzani wa CCM. Hao ni kama Lyatonga, mwenyekiti wa chama kilichosimamisha mgombea wa urais lakini yeye anawashawishi wapiga kura wampigie mgombea wa chama kingine. Mpizani?Hili la baadhi ya vyama vya upinzani aina ya ACT kupendwa sana na CCM haijaanza leo. Na ndio maana watu wenye akili kama Kitila na Zitto wanajihisi vizuri zaidi (feeling good) ku-compromise na watawala kuliko wapinzani wenzao.
Unaambiwa akili za kuambiwa changanya na zako, kwa hiyo usitarajie tofauti yoyote
hata wakitoka, atawaita ikulu kunywa juice, then yatakwisha!
Huwezi kujua uhalisia wa uhalali wa uchaguzi huu hadi uwe unajua kilichokuwa kinatendwa nyuma ya pazia!
Nakubaliana Na Kitila,
Maana Hata Waliposhinda Wabunge Wapinzani Maranyingi Na Madiwani Tumepata Sasa Iweje Wabunge Wawe Wachache Na Urais Apate Yeye?
Mm Nilimpigia Lowasa, Japo Iliniuma Kukosa Ila Nimekubali Tumeshindwa Japo Sijarizika.