Kitendo Cha Inteligensia ya Polisi kutoana viashiria vya ualifu kwenye Mikutano ya Chadema kinanifanya niamini nchi ipo salama

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Kwa miaka zaidi ya sita Intelligence ya Polisi ilikuwa ikipokea taarifa za kiusalama zilizoonyesha viashiria vya uvunjifu wa amani kwenye Mikutano ya Chadema na vyama vingine vya siasa na hivyo kupelekea ma OCD kusitisha kufanyika kwa mikutano hiyo.

Toka tarehe 17/03/2021 hali ya Usalama imeimarika sana nchini na Sasa hivi hakuna vishiria vya uvunjifu wa amani Jambo lililopelekea viongozi wa Chadema kuzunguka nchi nzima bila kudhibitiwa Wala kutokea kwa vizingiti na uvunjifu wa Amani.

Niwaombe Jeshi la Polisi waendeleeze hali hii ya ulinzi wa nchi yetu hasa kufanikisha kudhibiti viashiria vya uvunjifu wa amani katika mikutano ya Chadema Kama ambavyo waliweza kudhibiti kwenye Mikutano ya CCM kwa kipindi chote Cha uhai wa CCM.

Nitoe rai kwa umma wa Watanzania kuendelea kudumisha Amani. Lakini pia niwaombe Polisi watusaidie wananchi kujua waliokuwa wanaleta uvunjifu wa amani nchini wamekimbilia wapi au wamepata kazi nyingine zakufanya?
 
cc IGP
 
Kigoma huko Bus la Abiria limetekwa! Uzuri wa Amani huwa haina kulemba ikilega kila kiumbe hupoteana.
 

Kwamba?

"Nitoe rai kwa umma wa Watanzania kuendelea kudumisha Amani. Lakini pia niwaombe Polisi watusaidie wananchi kujua waliokuwa wanaleta uvunjifu wa amani nchini wamekimbilia wapi au wamepata kazi nyingine zakufanya?"

Watakuwa wamepumzika kwa amani mkoani Geita.
 
Kwa mtazamo wangu,hao ndio waliokuwa watu wasiojulikana.
 
Lini nchi haikua salama?
 
Sifa kubwa ya kuajiriwa kuwa polisi ni kuwa mrefu na mwenye mbio kushinda wengine.
Hakuna polisi mwenye akili hata yule IGP ni mpuuzi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…