Mtu ni zaidi ya uzito, urefu, group ya damu, jinsia. He is a complex creature. Ndiyo maana kila mtu ni yeye tu (unique) hata kama atafanana kivipi na mwingine. Kuna vitu ambavyo ni vyake tu kati ya hivyo vinavyomuunda huyu mtu. Na kwa sababu ya upekee huo ambao haujirudii, ndiyo maana unakuta kwamba mwitikio wa huyu mtu kwa mazingira mbalimbali ikiwa ni pamoja na magonjwa unatofautiana kati yake na watu wengine. Vivyo hivyo katika kuitikia matibabu kutatofautiana kati ya mtu na mtu. Kwa hiyo sababu ni nyingi sana zikiwemo za kimwili, kimazingira, kisaikolojia, kiimani, nk. nk. nk.