Kitendawili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitendawili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kiby, Jul 24, 2010.

 1. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Nimeulizwa swali ambalo nimeshindwa kulitolea majibu. Hivyo nikaonelea nililete hapa JF, na kwa kua naamini hapa jamvini pana vichwa vilivyojaa hekima kwa kila nyanja jibu litapatikana. Swali lenyewe ni hili: inakuwa je watu wawili wenye status zinazo fanana kwa kila kitu ikiwa ni pamoja na uzito, urefu, group ya damu na hata jinsia, wanaugua malaria iliyofikia level moja mfano wa malaria tatu. Wanapewa dozi ya tiba ya uzito sawa, mmoja anapona na wa pili yake anafariki? Wataalamu wa jf tusaidiane kwa hili.
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mtu ni zaidi ya uzito, urefu, group ya damu, jinsia. He is a complex creature. Ndiyo maana kila mtu ni yeye tu (unique) hata kama atafanana kivipi na mwingine. Kuna vitu ambavyo ni vyake tu kati ya hivyo vinavyomuunda huyu mtu. Na kwa sababu ya upekee huo ambao haujirudii, ndiyo maana unakuta kwamba mwitikio wa huyu mtu kwa mazingira mbalimbali ikiwa ni pamoja na magonjwa unatofautiana kati yake na watu wengine. Vivyo hivyo katika kuitikia matibabu kutatofautiana kati ya mtu na mtu. Kwa hiyo sababu ni nyingi sana zikiwemo za kimwili, kimazingira, kisaikolojia, kiimani, nk. nk. nk.
   
 3. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  .
  Ahsante mkuu. Sasa kama ni hivi kuna jitihada zozote kwa wataalamu wa tiba kutengeneza dozi ya kipekee kwa kila mtu maana kila mmoja hafanani na mwingine? Ukizingatia pia kuna ni ukweli usiopingika wa hizi tofauti. Hata dole gumba hakuna linalofanana na mwingine yeyote duniani.
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Jul 25, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Kama vipimo vya kitabibu vote vinafananana, inategemea na jinsi miili yao inavyoyeyusha dawa ile na kuiruhusu kuanza kufanya kazi, na uimara wa mifumo yao vingine vya mwilini kama nervous system, na circulation system. Ndiyo maana watu hao wanaweza kunywa pombe pamoja lakini mmoja wao akalewa mapema sana wakati yule mwingine bado anadai kabisa.
   
 5. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  .
  Basi kumbe ni vema na sii kosa kwa ile tabia ya watu kutanguliza neno 'nikijaliwa na Mungu nitapona' bila kuwa na uhakika wa asilimia mia kwamba baada ya kumaliza dozi husika nimepona. Pili kumbe tiba ni probabilities. Na ndio maana hospitali zote zina mortuary ambazo hazipo tu kwa ajili ya wale waliocheleweshewa huduma ya tiba bali pia kwa wale dozi husuka imeshindwa kufanya kazi.
   
Loading...