Kitasa gani cha mlango ni bora?

Kuna kitasa kinaitwa spider sh. 3000/= kizuri tu kwa maisha ya kijamaa ila muda wowote unaweza kujifungua ndani na kisifunguke hadi jirani aje na jiwe maarufu Fatuma.
hahahahahahaha au unaweza kushindwa kuingia kwako jioni ukaanza kuhangaika na fatuma.
 
Ukiwa na muda pita DIY kama unaenda mikocheni coca cola karibu na geti la majembe utakuta hivyo vitu na vingine viingi kwa shughuli yako
 
Union Ni vizuri na imara ILA tatizo lake nikisoma namba ya kwenye funguo nakwenda kwa wachonga funguo nawatajia namba wananipa funguo ile ile kama yako, tulifunga guest wateja walikuwa wanaibiwa Sana.
 
Tushauri Mkuu baada ya kugundua tatizo hilo ulifanyeje? Manake nimeangalia ufunguo wangu hapa nilienda kuchanga ni kweli No zinafanana na ufungue mwingine uliokuwa umebaki.
 
Mambo yote ni HAFELE , HUTAJUTIA FEDHA YAKO, ANGALIA SAMPLE KWENYE MILANGO YOTE YA OFFICE ZA NMB KILA TAWI
 
Tushauri Mkuu baada ya kugundua tatizo hilo ulifanyeje? Manake nimeangalia ufunguo wangu hapa nilienda kuchanga ni kweli No zinafanana na ufungue mwingine uliokuwa umebaki.

sisi tulibadilisha vitasa, tukafunga vitasa vinavyo tumia sleeve ambavyo, hata funguo zikipotea unaenda dukani kununua sleeve unapata na funguo zake
 
Hii ni bei ya jumla?
Aiseee na hivi ninavyoambiwa na mafundi wa milango kwamba vinaenda mpaka 150,000/= vitasa vya Union Original kwa milango ya nje! Hii bei iko sawa au mafundi wanataka kunipiga??
Pia nimeambiwa kuna vingine vinaitwa Icon navyo vinauzwa 80,000/= vya milango ya nje.
 
Back
Top Bottom