Ndugu wawili kunyongwa kwa mauaji ya kikatili

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
430
998
Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Kigoma, imewahukumu adhabu ya kifo, wakazi wawili wa kijiji cha Msebei katika Wilaya ya Uvinza baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumuua kikatili mkata kuni kijijini hapo kwa kutumia shoka.

Mtuhumiwa mkuu wa mauaji hayo, Hamis Nzovu ambaye alimkata marehemu kwa shoka na kuondoka na mikono miwili, uume na korodani kwa maelezo kuwa anakwenda kuzibanika nyumbani kwake, hajakamatwa hadi sasa.

Baada ya mauaji hayo, Lucas Charles aliyekuwa mshtakiwa namba moja na mshtakiwa namba mbili Emanuel Charles, walishirikiana na Nzovu kumfunga jiwe ili asielee na kuuzamisha mwili kwenye mto Ruchugi.

Kiini cha mauaji hayo kulingana na ushahidi uliotolewa Mahakamani yakiwamo maelezo ya onyo ya Lucas na Emmanuel ya kukiri kosa, ni wivu wa mapenzi ambapo Nzovu alimshuku marehemu Yamungu kuwa uhusiano na mkewe.

Yamungu aliyefahamika kwa jina hilo moja tu, aliuawa kikatili siku isiyofahamika Februari 2022 na mwili wake kupatikana Februari 14, 2022 ukielea katika mto Ruchugi na uligunduliwa siku hiyo usiku na wavuvi.
Hukumu hiyo ilitolewa Julai 13,2023 na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma, Lameck Mlacha na nakala yake kupatikana jana katika tovuti ya Mahakama, mahsusi kuchapisha maamuzi, sheria na kanuni bure mtandaoni.

Jaji Mlacha katika hukumu yake alisema baada ya kupitia maelezo hayo washtakiwa ya kukiri kutenda kosa hilo na kushawishika kuwa maelezo hayo hayajabeba kitu kingine zaidi ya ukweli, anaona washtakiwa wana hatia.

“Kuna adhabu moja tu ya kuua kwa kukusudia nayo ni kunyongwa hadi kufa. Binafsi siipendi adhabu hii lakini mikono yangu imefungwa na sheria na kiapo cha kutenda haki. Nawahukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa,” alisema Jaji.

Hata hivyo, aliyekuwa mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyo, Juma Mgararizi aliachiwa mapema baada ya upande wa mashtaka kufunga kesi yao na kuonekana hakuwa na kesi ya kujibu hivyo mahakama kuamuachia huru.

Upande wa mashtaka ulioongozwa na wakili wa Serikali mwandamizi, Amina Mawoko aliyesaidiana na wakili, Edna Makala, uliita mashahidi saba na kuwasilisha vielelezo yakiwamo maelezo ya ungamo ya Lucas na Emmanuel ambao ni ndugu.

Jaji alisema baada ya kukamilika kwa kesi ya upande wa mashtaka, mahakama iliona hakukuwa na ushahidi unaoonyesha mshtakiwa wa tatu, Mgaririzi alifanya uhalifu huo hivyo kumuachia huru kwa kuwa hakuna na kesi ya kujibu.

Maelezo ya kukiri kosa yalivyo
Katika maelezo yao ya onyo waliyoyaandika polisi, Lucas Charles na Emmanuel Charles ambao walikuwa ni marafiki na mtuhumiwa Hamis Nzovu ambaye hajapatikana, wameeleza kinagaubaga ushiriki wao katika mauaji hayo.

“Baadae akakata (sehemu za siri), kwa kutumia shoka hilo. Wakati hayo yanafanyika mimi nilikuwa nimemshika

CREDIT: MWANANCHI
 
Mtu anajiita Mgararizi?maana yake ni mtu alieshindikana kwa ujeuri na tabia zote mbovu.kazi ipo kwa vijana.nyie marijali,mke wa mtu sumu jamani achaneni nao.mbona masingo ni wengi tu na mmeongezewa mpaka machoko.tafuteni wa kwenu

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
So sad, ila nimependa vile kesi imeenda kwa haraka sana haijachukua muda mrefu, mahakimu wajifunze kwa hili
 
Safi sana muda mfupi wa kesi pia waliohukumiwa nami nafata wake zao nijilipe wakiwa kifungoni
 
Back
Top Bottom