Kitambue chombo VOYAGER 1

Kitambue chombo VOYAGER 1

kurudi chini kwenda wapi? au hujui hakuna sayari iliyojuu wala chini
Mkuu umeanza kuelewa kwanza ukajibu au umesoma tu kwa ajili ya kujibu...sijazungumzia suala la sayari hata kidogo ila nilichohoji ni hiyo voyager pindi chanzo cha nishati kitakapoisha kwa maana hakitokuwa na uwezo tena wa kujioperate so what next...haitokuwa tena na escape velocity hvyo itazidiwa nguvu na kitaanza kudondoka so from this point of falling where it will be dumped?


acha kabisa
 
Huto to thrusters hatutaweza kuzuia gravitation pull ya chochote! Lakini pia spidi yake itapungua baada ya hapo hizo transponders zitazimika,baridi huko ni kaaali saana haijulikani baada ya hapo.
 
Mkuu umeanza kuelewa kwanza ukajibu au umesoma tu kwa ajili ya kujibu...sijazungumzia suala la sayari hata kidogo ila nilichohoji ni hiyo voyager pindi chanzo cha nishati kitakapoisha kwa maana hakitokuwa na uwezo tena wa kujioperate so what next...haitokuwa tena na escape velocity hvyo itazidiwa nguvu na kitaanza kudondoka so from this point of falling where it will be dumped?


acha kabisa
Mkuu kikiishiwa hiyo nguvu kitabaki kinaelea kuhusu kuvutwa kitavutwa endapo kutakuwa na gravit yoyote inayoweza kukivuta lkn kama kitakuwa karibu na huo mvutano wa hiyo nguvu,kwasasa kipo mbali mno na dunia pamoja na solar system yetu hivyo kuvutwa huku kwetu mmmmmhh! ni shughuli getegete..
 
Mimi kwa ukubwa wa dunia hii najiona kama "bacteria" na mimea naiona kama "algae"
hio ndio sababu ya mafundisho yote haya kwamba watu wote ajione wadogo na hawana thamani ili wawe rahisi kuongoza,kama ingekuwa watu wanajiona kuwa wapo katika centre of everything na kila kitu kilicho hapa kimefanywa kwa ajili yetu tungekuwa na thamani kubwa sana na ingekuwa tabu kumtawala mtu

jinsi ya kuendesha jamii kubwa ya watu ni lazima uwaingie akilini na kuwaaminisha mambo ya kusadikika,maana yake ni kuwa ikiwa tutajiona kama bacteria na dunia yetu ni kama punje ya mchanga inapeperuka kwenye infinity space kwenye trilion za nyota nyengine na matokeo ya sisi kuwepo hapa duniani ni bahati tu na sio kwa makusudi basi thamani yetu inapungua na tunabakia kuwa ni watu tusiojali kitu
 
hio ndio sababu ya mafundisho yote haya kwamba watu wote ajione wadogo na hawana thamani ili wawe rahisi kuongoza,
Hapana wala sikuwa na maana hiyo.nilikuwa namaanisha udogo wangu na ukubwa wa sayari niliyomo thats it.
 
sisi kuwepo hapa duniani ni bahati tu na sio kwa makusudi basi thamani yetu inapungua na tunabakia kuwa ni watu tusiojali kitu
Mimi naamini kuwa tumeumbwa na mungu,ila tumewekwa hapa kwenye hili "tufe"kwa lengo fulani.
 
1977-2020....Mzungu si mtu wa mchezo mchezo aisee
 
mkuu ntajaribu kukujibu kwa kadri ya uwezo wangu lakini nakusihi ufanye research kwa umakini

kwanza hakuna picha ya ukweli ya dunia ikiwa flat au duara,hizo picha zote za duara zote sio za kweli kila kitu ni photoshop kuna picha moja tu ambayo wanadai kuwa ni ya kweli ambayo waliipiga wakati wanakwenda mwezini,kama unafatilia vya kutosha utagundua kuwa hakuna mtu aliyewahi kwenda mwezini hizo video zao za kwenda mwezini zote za uzushi. kwa hio hio picha ni propaganda tu sio ya kweli. miezi kadhaa nyuma wamesema wanafanya reseach ili watu waweze kupita kwenye van allen belt ambayo ina radiation kubwa sana na madhara makubwa kwa watu lakini wakati huo huo 1969 wanasema watu walipita hapo kwenda mwezini na hawakudhurika kwa sababu walikuwa hawajui kuwa pana radiation,kwa hio kutokujua ndio kumewanusuru watu 1969 kuto kuathirika.

la pili ni hapo uliposema kwanini nchi hizi nyengine kubwa zote zitudanganye?
mkuu hapa lazma uwe unafahamu jinsi ya dunia inavyoendeshwa kwamba usione hizi nchi zikifanya maonesho kuwa wao ni maadui na hawaelewani ,marekani na china na urusi na nchi zote zenye elimu ya juu na mamlaka yenye kufahamu mambo makubwa kama haya wanafanya kila kitu kwa pamoja na zinaendeshwa entity moja kwa ajili ya kuendelea kudanganya uuma ili maisha ya watu duniani yawe in peace,huwezi kujua labda kama tutakuja kuoneshwa kiukweli jinsi ilivyo hii dunia na space pengine sote tutachanyanyikiwa ndio maana kwa mitazamo yao uongo bado unahitajika uendelee na pesa nyingi sana zinatumika kuendeleza propaganda hizi,saivi nchi za uchina,urusi,japan,uk nk zote zina space agencies kama ya nasa kwa ajili ya kuendelea kufanya maonyesho haya na sio space exploration

tatu ukiangalia video za watu na maparachuti unaona duara hii sio kweli kuona duara kutokana na camera hata usiwe na parachuti unaweza kuona duara hapa hapa chini kuna kwa camera ambazi zina fish-eye lens
ndege zinaruka juu zaidi na hazioni duara la dunia seuze mtu na parachuti

mimi nnachoamini ni kuwa shepu ya dunia iliyo halisi haijawahi kuonekana na watu wa kama kama sisi,kwa hio hatuwezi kujua,lakini nna uhakika sio duara kama chungwa na dunia hairuki kwa masafa na speed wanazosema wala haina motion ya aina yeyote,tetemeko la ardhi ndio motion pekee na hio ikitokea watu wanaihisi kiukweli sio hizi speed za miujiza ambazo hatuwezi kuzihisi

jaribu kuitia akilini speed na rotation za dunia
rotation on its axis ni 1674 km per hr
speed ya dunia kuzunguka jua ni 110,000 km per hr
speed ya rotation ya solar system 828,000 km per hr
na milkyway galaxy ina-travel kwa speed hii 3.6mil km per hr
speed zote hizi na rotation zinakwenda kwa wakati mmoja na mielekeo tafauti kila speed inaelekea kwake, haziingii akilini na hatuna uwezo kuzifahamu tukafananisha na kitu chochote ili tukaona ukweli utakavyokuwa

speed ambayo tumewahi kupata idea ni za gari zinapifika 140km/hr na hapo tunaogopa sana wakati speed za dunia ndio kama hizo nazo tunaambiwa ni constant hazibadiliki lakini usiku na mchana masaa yanabadilika mara nyengine usiku unakuwa mkubwa kidogo na/au mchana unakuwa mdogo,kama speed za dunia ni constant kwanini usiku na mchana masaa yasiwe constant kwa sababu rotation iliyo constant ndio inayosababisha usiku na mchana,uhalisi tunaoona ni kuwa usiku unakuwa mdogo na au mchana unakuwa mkubwa baadhi ya time.

pamoja na speed hizi zote ambazo zinakwenda zig-zag kwa wakati mmoja bado unaweza kwenda kwenye ziwa na ukakuta maji yametuwama tulii na dunia na bahari zipo shwarii na sisi hatuoni kizunguzungu wala hizi speed hazitukeri kabisa, ukiuliza kwanini utaambiwa ni law of gravity ndio inayoiwezeshwa dunia kuwa shwari na sisi kuganda hapa
force of gravity inaituliza na kuzuia bahari na maziwa ya maji mazito sana ili yasiganduke kwenye uso wa dunia lakini ndege wanaachiwa waruke na vikaratasi ambavyo ni vyepesi sana na mabofu yanaachiwa yapeperuke ovyo ovyo kwanini hii force ya gravity inachagua cha kuzuia na kuachia na ina nguvu kubwa ya kuzuia bahari lakini ishindwe kuzuia bofu lisruke ambalo ni jepesi sana
ukiuliza kwanini unaambiwa ni law of relativity ambayo inatowa jawabu za mahusiano baina ya vitu hivi na vyengine kwa nini hiki kinaweza na kile hakiwezi

kila kitu kina law lakini ukweli tu ndio unaofichwa hapa, ndio maana tunafata law za uongo law za kutengeneza ili kujenga hoja za uongo ili tusiziamini hisia zetu

hisia zinazoonsha kuwa
hatuwezi kuihisi mizunguko ya dunia kwa kwa sababu dunia haizunguki wao wanasema wanajua dunia inazunguka
hatuwezi kuuona mpindo wa dunia ilivyo duara wao wanasema upo lakini hatuna uwezo wa kuuona
uhalisi ni kwamba dunia haizunguki na hakuna mpindo wa duara ndio mana hatuhisi mizunguko na hatuoni mipindo ya duara la dunia
Mkuu kama naanza kukuelewa Sasa japo kwa mbaaali....
 
Mmi nakuelewa sana usiambiwe kitu tu duniani ukakubali mungu ametupa akili binaadam ya kufikiri unaweza akaambiwa jambo kumbe anaekwambia lile jambo anamaana yake tofauti na unavyofikilia wewe
 
golden_record_cover_sm.jpg

The golden record
hiki ni ki plate maalum ambacho kipo kwenye voyager ndio kina taarifa juu ya uwepo wetu means kina show direction ya wapi sisi tupo,nini kinafanyika duniani na kina sauti mbalimbali za wanyama,upepo n.k pia kina picha na maelekezo ya namna ya kuplay hizo sauti na salamu za lugha zipatazo 55 za zamani na sasa ktk maeneo tofauti tofauti.
ukitaka kujua mengi google utajua kuhusu kifaa hicho hapa me nimedodosadodosa tu.
Duh wenzetu wametushinda mbal sana
 
Mkuu ZENJIBARIA naomba nikuulize hii kitu Nina rafiki yangu yeye ni baharia aliwahi kuniambia kuna sehemu ya dunia hii wakipita na meli miezi fulani kunakuwa hakuna jua kabisa ni baridi au kuna kipindi wanaliona jua Kwa mbali na kupotelea huko huko na kuna kipindi jua linakuwepo kama kawaida japo na linakuwa sio kama la huku Kwa maana ya masaa yanakuwa tofauti ya mchana na usiku,
Je hauoni hiyo ni prove kwamba dunia inalizinguka jua na sio jua lipo juu ya uso wa dunia?
 
Mtu mweusi alilaaniwa tangu enzi acha tushughilike na matumbo maana ndo uwezo wetu ulipofikia
 
Ni anga mkuuu sio dunia, dunia ni hii tunayoishi sisi viumbe hai, lakini ukisha toka nakupaa juu zaidi hadi panaitwa space yaani anga
kila pahali ni space mkuu space ina sifa hizi actions can happen and things can exist so hata hapa duniani kuna space humo geto unapolala ni space... sio kwamba inaanzia huko juu
 
kila pahali ni space mkuu space ina sifa hizi actions can happen and things can exist so hata hapa duniani kuna space humo geto unapolala ni space... sio kwamba inaanzia huko juu
Ni sawa, ila kwakile kilichozungumziwa ndio kilikuwa hakihusu dunia , bali space mzee
 
nawe umeona hilo mkuu ukimsoma vizuri ni kama ulivyosema huenda anajaribu kuona kama ananguvu ya ushawishi...
ki ukweli nia yangu sio kumshawishi mtu kama mimi sikushawishiwana mtu na naaamini kila mmoja wetu atakuwa na wakati wake wa kufahamu kwa viwango tafauti vya uelewa,nlikuwa kutoa maoni yangu tu,sina chama kuwa nnatafuta wafuasi,yangu ni maoni tu
 
ki ukweli nia yangu sio kumshawishi mtu kama mimi sikushawishiwana mtu na naaamini kila mmoja wetu atakuwa na wakati wake wa kufahamu kwa viwango tafauti vya uelewa,nlikuwa kutoa maoni yangu tu,sina chama kuwa nnatafuta wafuasi,yangu ni maoni tu
vyema...
 
Back
Top Bottom