Kitambue chombo VOYAGER 1

Kitambue chombo VOYAGER 1

Zenjibaria sorry kwa ile comment#55 sorry bro.
 
Mkuu zenj unajua chochote kuhusu radio calls, walkie talkies, one way radios
 
Zenjibaria sorry kwa ile comment#55 sorry bro.

haina shida mi nachukulia criticism kama changamoto tu hazinikeri kabisa,asante.

jaribu kupitia posts nlizoweka kwenye uzi huu zote pengine unaweza kupata aidia japo ndogo ya kujenga maswali
 
Kuna comment yako ya nyumaa nliona umeandika hakuna mwezi ni myth ....tena sasa hv unasema kuna mwezi na jua....

sijawahi kusema hakuna mwezi mkuu,mwezi ni kitu kila mtu anakiona,labda hukunisoma vizuri nimesema mwezini hakuna ardhi kama ilivyo hapa duniani, kwa hio hakuna mazingira ya watu kwenda wakatua spaceships,zipitie vizuri comments zangu
 
hakuna voyager wala hakuna space exploration hizi zote ni propanganda za uongo mtupu,yote haya ni makatuni ya kuchora,picha zote za space sio za kweli na picha za dunia zote zilizo online zote ni uongo mtupu zote za kuchora hakuna picha ya dunia iliyo kweli,tunavyosomeshwa ni propaganda tu hali halisi ya dunia ilivyo haijasemwa ndio maana tunaaminishwa hizi fantasy
Bangi sio nzuri.
Hapo hapo hio internet unayotumia ikizingua unawalaumu tigo 4 G yao inasumbua?
Kama sio bangi ni nini?
 
nimefikia viwango vizuri vya shule na madrassa pia ila fanya utafiti kidogo utajinea mwenyewe

kama unakwenda shule uliza maswali haya
proof of gravity
proof of earth spinning(usiku na mchana sio proof) ulizia kama kuna aina ya kipimo kilowahi kuthibitisha spin
proof sun is 93mil miles
ni wapi imewahi kutokea maji yakawa na mpindo(yaani ukitia maji kama kwenye glass yakawa na uvimbe wa juu kuonesha mpindo

maswali yapo mengi ulizia hayo tu kwanza
aiseee,kuna watu wa hivi bado?!!
 
mkuu ntajaribu kukujibu kwa kadri ya uwezo wangu lakini nakusihi ufanye research kwa umakini

kwanza hakuna picha ya ukweli ya dunia ikiwa flat au duara,hizo picha zote za duara zote sio za kweli kila kitu ni photoshop kuna picha moja tu ambayo wanadai kuwa ni ya kweli ambayo waliipiga wakati wanakwenda mwezini,kama unafatilia vya kutosha utagundua kuwa hakuna mtu aliyewahi kwenda mwezini hizo video zao za kwenda mwezini zote za uzushi. kwa hio hio picha ni propaganda tu sio ya kweli. miezi kadhaa nyuma wamesema wanafanya reseach ili watu waweze kupita kwenye van allen belt ambayo ina radiation kubwa sana na madhara makubwa kwa watu lakini wakati huo huo 1969 wanasema watu walipita hapo kwenda mwezini na hawakudhurika kwa sababu walikuwa hawajui kuwa pana radiation,kwa hio kutokujua ndio kumewanusuru watu 1969 kuto kuathirika.

la pili ni hapo uliposema kwanini nchi hizi nyengine kubwa zote zitudanganye?
mkuu hapa lazma uwe unafahamu jinsi ya dunia inavyoendeshwa kwamba usione hizi nchi zikifanya maonesho kuwa wao ni maadui na hawaelewani ,marekani na china na urusi na nchi zote zenye elimu ya juu na mamlaka yenye kufahamu mambo makubwa kama haya wanafanya kila kitu kwa pamoja na zinaendeshwa entity moja kwa ajili ya kuendelea kudanganya uuma ili maisha ya watu duniani yawe in peace,huwezi kujua labda kama tutakuja kuoneshwa kiukweli jinsi ilivyo hii dunia na space pengine sote tutachanyanyikiwa ndio maana kwa mitazamo yao uongo bado unahitajika uendelee na pesa nyingi sana zinatumika kuendeleza propaganda hizi,saivi nchi za uchina,urusi,japan,uk nk zote zina space agencies kama ya nasa kwa ajili ya kuendelea kufanya maonyesho haya na sio space exploration

tatu ukiangalia video za watu na maparachuti unaona duara hii sio kweli kuona duara kutokana na camera hata usiwe na parachuti unaweza kuona duara hapa hapa chini kuna kwa camera ambazi zina fish-eye lens
ndege zinaruka juu zaidi na hazioni duara la dunia seuze mtu na parachuti

mimi nnachoamini ni kuwa shepu ya dunia iliyo halisi haijawahi kuonekana na watu wa kama kama sisi,kwa hio hatuwezi kujua,lakini nna uhakika sio duara kama chungwa na dunia hairuki kwa masafa na speed wanazosema wala haina motion ya aina yeyote,tetemeko la ardhi ndio motion pekee na hio ikitokea watu wanaihisi kiukweli sio hizi speed za miujiza ambazo hatuwezi kuzihisi

jaribu kuitia akilini speed na rotation za dunia
rotation on its axis ni 1674 km per hr
speed ya dunia kuzunguka jua ni 110,000 km per hr
speed ya rotation ya solar system 828,000 km per hr
na milkyway galaxy ina-travel kwa speed hii 3.6mil km per hr
speed zote hizi na rotation zinakwenda kwa wakati mmoja na mielekeo tafauti kila speed inaelekea kwake, haziingii akilini na hatuna uwezo kuzifahamu tukafananisha na kitu chochote ili tukaona ukweli utakavyokuwa

speed ambayo tumewahi kupata idea ni za gari zinapifika 140km/hr na hapo tunaogopa sana wakati speed za dunia ndio kama hizo nazo tunaambiwa ni constant hazibadiliki lakini usiku na mchana masaa yanabadilika mara nyengine usiku unakuwa mkubwa kidogo na/au mchana unakuwa mdogo,kama speed za dunia ni constant kwanini usiku na mchana masaa yasiwe constant kwa sababu rotation iliyo constant ndio inayosababisha usiku na mchana,uhalisi tunaoona ni kuwa usiku unakuwa mdogo na au mchana unakuwa mkubwa baadhi ya time.

pamoja na speed hizi zote ambazo zinakwenda zig-zag kwa wakati mmoja bado unaweza kwenda kwenye ziwa na ukakuta maji yametuwama tulii na dunia na bahari zipo shwarii na sisi hatuoni kizunguzungu wala hizi speed hazitukeri kabisa, ukiuliza kwanini utaambiwa ni law of gravity ndio inayoiwezeshwa dunia kuwa shwari na sisi kuganda hapa
force of gravity inaituliza na kuzuia bahari na maziwa ya maji mazito sana ili yasiganduke kwenye uso wa dunia lakini ndege wanaachiwa waruke na vikaratasi ambavyo ni vyepesi sana na mabofu yanaachiwa yapeperuke ovyo ovyo kwanini hii force ya gravity inachagua cha kuzuia na kuachia na ina nguvu kubwa ya kuzuia bahari lakini ishindwe kuzuia bofu lisruke ambalo ni jepesi sana
ukiuliza kwanini unaambiwa ni law of relativity ambayo inatowa jawabu za mahusiano baina ya vitu hivi na vyengine kwa nini hiki kinaweza na kile hakiwezi

kila kitu kina law lakini ukweli tu ndio unaofichwa hapa, ndio maana tunafata law za uongo law za kutengeneza ili kujenga hoja za uongo ili tusiziamini hisia zetu

hisia zinazoonsha kuwa
hatuwezi kuihisi mizunguko ya dunia kwa kwa sababu dunia haizunguki wao wanasema wanajua dunia inazunguka
hatuwezi kuuona mpindo wa dunia ilivyo duara wao wanasema upo lakini hatuna uwezo wa kuuona
uhalisi ni kwamba dunia haizunguki na hakuna mpindo wa duara ndio mana hatuhisi mizunguko na hatuoni mipindo ya duara la dunia
Ninakuelewa sana
 
kila kitu kinachohusu space sio kweli pamoja na hio space yenyewe yote,picha zote za sayari zote,rover,satelites kila kitu ni photoshop,kwa mitazamo ya haraka haraka sio rahisi kufahamu lakini chungunza kila kitu unnaweza kuona kuwa hakuna proof ya mambo yote hayo,proof kubwa iliyopo ni kwenye mifumo yetu ya elimu tumefundishwa hivo na matangazo ya kwenye vyombo vya habari wanatangazia bas na sisi tunasikia na kuamini kila kitu
Tehe mkuu unatumia dose ipi??
 
kuna mambo mengi sana ya kuangalia ambayo yatakuonesha kuwa elimu yote ya space na uhalisi wa dunia ilivyo ni uongo

- wanasema dunia ipo duara kama chungwa lakini ndege zikiruka hazizunguki chungwa zinafika angani zinaweka cruising speed na zinakwenda straight hazilazi pua chini au juu kulizunguka chungwa ambayo ndio shepu ya dunia
-wanasema dunia ni shape ya chungwa kwa hio kila pahala patakuwa na mpindo ili kupara shepu ya chungwa kwa maana hio ukiwa dar zanzibar huwezi kuiona popote kwa maana itakuwa upande wa pili wa mpindo wa dunia na hii zipo formula zake ambayo kwa masafa ya dar to znz ni kama 44km mpindo wa maji ulikuwa uwe kama ulikuwa uwe atleast 60m
-pia hivi majuzi wamesema wanajiandaa ili waweze kutoka kwenye low-earth orbit na waweze kupeleka watu outer sapce wakati mwanzo wamesema washapeleka watu kwenye mwezi ambayo upo beyond low earth orbit.

-sifa moja kuu ya maji popote yalipo ni lazima yawe level,maji hayawezi kupinda kufanya duara,kwa hio hilo duara la dunia maji yanapinda vipi kuweka shepu ya duara,maji ni lazima yatafute level kwa namna yeyote ile,

gravity ni uzushi ,kama gravity ndio inayozuia vitu hapa duniani iweje ndege iliyo ndogo na nyepesi iweze kuishinda gravity na iruke wakati bahari iliyo kubwa sana nzito kuliko kitu chochote hapa duniani isiweze kuishinda gravity'
au kwanini gravity iruhusu mabofu yende ngani wakati vitu vizito zaidi vipeshikwa na gravity


ki uhalisia hakuna aliyewahi kufika mwezini na mwezi haupo na ardhi kama ilivyo hapa duniani,sayari zote picha tunazoziona online sio halisi ni michoro tu, picha halisi hazipo clear kama wanavyoonesha hio michoro

mambo ni mengi sana ntarudia tena mengine
Word! Sema wengi washalewa na hii elimu yao ya binadamu Ni nyani.
 
Mkuu zenjibaria,ukitaka kujua umbali ingia kwenye universe,kuna sehemu umbali wake unapimwa kwa spidi ya mwanga, kwenye solar system ni yetu ni karibu sana.
 
Milk way galaxy hata usiku inaonekana kwa kiasi kikubwa,ukitumia telescope za kawida tu unaiona hata andromeda,alafu tusiijue dunia tunayoishi.
 
Aingie hubble telescope website,au anunue telescope ndogo zinauzwa madukani akirudi zanzbar usiku anazima taa anakaa uwani ana enjoy kwa macho yake.hatutaki mrejesho.ndio atashuhudia uumbaji wa mungu na ukubwaaaaaaaaaaaaaaaaaaa wa universe.good luck zenjibar.
Sijui Imani yako but naona umesema uumbaji wa Mungu so unaamini kuna Mungu.
Then kamsome Joshua jinsi alivyosimamisha jua ndio utajua kipi kinazunguka kati ya jua/mwezi na hii dunia...
 
hakuna voyager wala hakuna space exploration hizi zote ni propanganda za uongo mtupu,yote haya ni makatuni ya kuchora,picha zote za space sio za kweli na picha za dunia zote zilizo online zote ni uongo mtupu zote za kuchora hakuna picha ya dunia iliyo kweli,tunavyosomeshwa ni propaganda tu hali halisi ya dunia ilivyo haijasemwa ndio maana tunaaminishwa hizi fantasy
tatizo ccm mkuu siyo lako!!
 
Bado tunajadili kuhusu matundu ya choo...mamaee
ha ha! mkuu kila jambo lina uzuri wake na ubaya wake... kitendo cha kuwekwa golden record kwenye voyager 1 ambacho kina taarifa zetu na mahala tunapopatikana kwenye galaxy kiliibua mjadala wa vipi ikiwa taarifa hizo zikaangukia kwa viumbe wabaya..? i mean viumbe ambao wanaweza kuja kuleta madhara duniani! hili nalo linatakiwa kuangaliwa maana tunaweza kuingia matatizoni kwelikweli ama tukapigwa cha chembe na baadhi wa watu kuwa kuna viumbe vimekuja kwa ubaya baada ya kupata zile information!
na ikiwa kama ni kweli kama tutashindwa kupambana navyo kuna kuharibiwa kwa dunia ama kutawaliwa!.
 
Back
Top Bottom