mkuu ntajaribu kukujibu kwa kadri ya uwezo wangu lakini nakusihi ufanye research kwa umakini
kwanza hakuna picha ya ukweli ya dunia ikiwa flat au duara,hizo picha zote za duara zote sio za kweli kila kitu ni photoshop kuna picha moja tu ambayo wanadai kuwa ni ya kweli ambayo waliipiga wakati wanakwenda mwezini,kama unafatilia vya kutosha utagundua kuwa hakuna mtu aliyewahi kwenda mwezini hizo video zao za kwenda mwezini zote za uzushi. kwa hio hio picha ni propaganda tu sio ya kweli. miezi kadhaa nyuma wamesema wanafanya reseach ili watu waweze kupita kwenye van allen belt ambayo ina radiation kubwa sana na madhara makubwa kwa watu lakini wakati huo huo 1969 wanasema watu walipita hapo kwenda mwezini na hawakudhurika kwa sababu walikuwa hawajui kuwa pana radiation,kwa hio kutokujua ndio kumewanusuru watu 1969 kuto kuathirika.
la pili ni hapo uliposema kwanini nchi hizi nyengine kubwa zote zitudanganye?
mkuu hapa lazma uwe unafahamu jinsi ya dunia inavyoendeshwa kwamba usione hizi nchi zikifanya maonesho kuwa wao ni maadui na hawaelewani ,marekani na china na urusi na nchi zote zenye elimu ya juu na mamlaka yenye kufahamu mambo makubwa kama haya wanafanya kila kitu kwa pamoja na zinaendeshwa entity moja kwa ajili ya kuendelea kudanganya uuma ili maisha ya watu duniani yawe in peace,huwezi kujua labda kama tutakuja kuoneshwa kiukweli jinsi ilivyo hii dunia na space pengine sote tutachanyanyikiwa ndio maana kwa mitazamo yao uongo bado unahitajika uendelee na pesa nyingi sana zinatumika kuendeleza propaganda hizi,saivi nchi za uchina,urusi,japan,uk nk zote zina space agencies kama ya nasa kwa ajili ya kuendelea kufanya maonyesho haya na sio space exploration
tatu ukiangalia video za watu na maparachuti unaona duara hii sio kweli kuona duara kutokana na camera hata usiwe na parachuti unaweza kuona duara hapa hapa chini kuna kwa camera ambazi zina fish-eye lens
ndege zinaruka juu zaidi na hazioni duara la dunia seuze mtu na parachuti
mimi nnachoamini ni kuwa shepu ya dunia iliyo halisi haijawahi kuonekana na watu wa kama kama sisi,kwa hio hatuwezi kujua,lakini nna uhakika sio duara kama chungwa na dunia hairuki kwa masafa na speed wanazosema wala haina motion ya aina yeyote,tetemeko la ardhi ndio motion pekee na hio ikitokea watu wanaihisi kiukweli sio hizi speed za miujiza ambazo hatuwezi kuzihisi
jaribu kuitia akilini speed na rotation za dunia
rotation on its axis ni 1674 km per hr
speed ya dunia kuzunguka jua ni 110,000 km per hr
speed ya rotation ya solar system 828,000 km per hr
na milkyway galaxy ina-travel kwa speed hii 3.6mil km per hr
speed zote hizi na rotation zinakwenda kwa wakati mmoja na mielekeo tafauti kila speed inaelekea kwake, haziingii akilini na hatuna uwezo kuzifahamu tukafananisha na kitu chochote ili tukaona ukweli utakavyokuwa
speed ambayo tumewahi kupata idea ni za gari zinapifika 140km/hr na hapo tunaogopa sana wakati speed za dunia ndio kama hizo nazo tunaambiwa ni constant hazibadiliki lakini usiku na mchana masaa yanabadilika mara nyengine usiku unakuwa mkubwa kidogo na/au mchana unakuwa mdogo,kama speed za dunia ni constant kwanini usiku na mchana masaa yasiwe constant kwa sababu rotation iliyo constant ndio inayosababisha usiku na mchana,uhalisi tunaoona ni kuwa usiku unakuwa mdogo na au mchana unakuwa mkubwa baadhi ya time.
pamoja na speed hizi zote ambazo zinakwenda zig-zag kwa wakati mmoja bado unaweza kwenda kwenye ziwa na ukakuta maji yametuwama tulii na dunia na bahari zipo shwarii na sisi hatuoni kizunguzungu wala hizi speed hazitukeri kabisa, ukiuliza kwanini utaambiwa ni law of gravity ndio inayoiwezeshwa dunia kuwa shwari na sisi kuganda hapa
force of gravity inaituliza na kuzuia bahari na maziwa ya maji mazito sana ili yasiganduke kwenye uso wa dunia lakini ndege wanaachiwa waruke na vikaratasi ambavyo ni vyepesi sana na mabofu yanaachiwa yapeperuke ovyo ovyo kwanini hii force ya gravity inachagua cha kuzuia na kuachia na ina nguvu kubwa ya kuzuia bahari lakini ishindwe kuzuia bofu lisruke ambalo ni jepesi sana
ukiuliza kwanini unaambiwa ni law of relativity ambayo inatowa jawabu za mahusiano baina ya vitu hivi na vyengine kwa nini hiki kinaweza na kile hakiwezi
kila kitu kina law lakini ukweli tu ndio unaofichwa hapa, ndio maana tunafata law za uongo law za kutengeneza ili kujenga hoja za uongo ili tusiziamini hisia zetu
hisia zinazoonsha kuwa
hatuwezi kuihisi mizunguko ya dunia kwa kwa sababu dunia haizunguki wao wanasema wanajua dunia inazunguka
hatuwezi kuuona mpindo wa dunia ilivyo duara wao wanasema upo lakini hatuna uwezo wa kuuona
uhalisi ni kwamba dunia haizunguki na hakuna mpindo wa duara ndio mana hatuhisi mizunguko na hatuoni mipindo ya duara la dunia