KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 26,213
- 56,849
Ni chombo cha kisayansi kilichorushwa na shirika la maswala ya anga NASA mwaka 1977,kusudi la kurushwa chombo hiki ni kwaajili ya kupeleleza anga ndani na nje ya mfumo wetu wa jua.
Voyager 1 mpaka sasa kiko umbali wa kilometa billion 18.35 kutoka duniani,mwaka 2012 chombo hicho kilipita mzingo wa pluto ambapo ndo kunaaminika ndio mwisho wa mfumo wa solar system yetu,kwamaana hiyo kipo nje ya mfumo wa jua letu!
Pia mwanga wa jua unahitaji zaidi ya masaa 17 kufikia chombo hicho ambapo umbali toka jua mpaka ilipo voyager ni km billion 19 na kitu.
Kifaa hiki kinatumia madini ya uranium kujizalishia umeme ili kiweze kujiendesha na itakapofika mwaka 2020 madini hayo yanatarajiwa kuisha hivyo kitastop na itakuwa ndo mwisho wake wa kufanya kazi!
Lakini pia kifaa hicho kimeekewa DNA za binadamu endapo ikitokea viumbe wengine kukipata wanaweza gundua kuwa kuna viumbe wengine mahala fulani.
hiyo ndo voyager 1 unaweza ongezea