Mila na desturi: Matumizi ya mikono

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,638
697,929
Kuliwahi kutokea mabishano hapa jukwaani toka kwa Wakenya na wabongo juu ya matumizi ya mikono kwenye mambo mbalimbali

Kila taifa lina tamaduni zake kwenye kila kitu na tamaduni moja ya kuheshimika inaweza kuwa tamaduni ya kudharaulika kwa wengine

Twende moja kwa moja kwenye point juu ya matumizi ya mikono kwenye maisha yetu ya kila siku..
Matumizi ya mkono wa kulia yanaheshimika kwenye kila kitu kwa yale mataifa ambayo hutumia maji kujisafisha/kutawadha mara baada ya kujisaidia, na hapo kinachotumika ni mkono wa kushoto
Kinyesi huchukuliwa ni uchafu mkubwa kiasi kwamba hata mtu ikitokea akakikanyaga lazima achechemee si kwa maumivu bali kwa hisia za kukanyaga uchafu
Hivyo kwa mataifa yenye utamaduni wa kutumia maji kujitawadha basi mkono wa kushoto hauwezi kutumika kwenye mambo haya
Kulia chakula
Kusalimiana
Kushukuru
Kupungia
Kuasa/kuonya
Kutoa ishara njema
Kuelekeza nk
Kwa waamini kwenye hizi desturi wakizaa mtoto anatumia mkono wa kushoto huona hilo ni tatizo na kuwalazimisha kutumia mkono wa kulia.. Mkono wa kheri!

Kwa mataifa yanayotumia karatasi laini kujisafisha baada ya kujisaidia haja kubwa kwao wao kutumia mkono wa kulia kwenye mambo mengi kuna ukakasi kidogo kwakuwa wao mkono wa kulia ndio husafisha mabaki ya uchafu baada ya kujisaidia
Hivyo kwao kukusalimia kwa mkono wa kushoto kwao ni sawa tu maana ni mkono usiogusa choo.. Na ndio maana kwenye taratibu zao za kula zinazoitwa table manners.. Mkono wa kushoto ndio unaohusika na kupeleka chakula kinywani
Na hata kwenye mambo mengi ya kimapokeo na mila hutumia mkono wa kushoto..
Sasa hapa ndipo penye mkanganyiko kuhusu matumizi ya mikono yetu na dhana nzima ya heshima.. Hasa mtu wa tamaduni fulani anapotumia mikono yake tofauti na mazoea ya kimapokeo kulinangana na muktdha mzima wa matumizi husika
Screenshots_2023-08-26-11-36-49.jpg
 
upinzani wakijinga ukizidi ni vyema mkono wa chuma utumike ili kusonga mbele walahi
 
Ombaomba huwa anashikwa Kwa mkono wowote ule.....MATONYA alinyanyasika Kwa kila namna kipindi kile cha mkapa na alikuwa mpole tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom