Kitabu Kipya: "Waliopotezwa Tanzania " Mwandishi: Sheikh Ponda Issa Ponda

Mzee wangu Said, huchoki na ngonjera za wapigania Uhuru? John Okelo alishiriki mapinduzi kule Zanzibar, je, nae ni Mzanzibar? Swala hapa si kuasisi chama wala kupigania Uhuru, hisipokuwa ni kwamba kuna Watanzania wenye asili ya Wamanyema wa Kongo. Kuwa Mmanyema hakuwezi kukuondoleeni Utanzania wenu kama ilivyo kwa Wamasaai, wako Kenya na wengine Tz, Wamakonde, Wajaruo nk.

Issue kubwa hapa ni maudhui ya vitabu mnavyoviandika. Kama vinahubiri udini na chuki bora usitueleze hapa jf, kaelezaneni uko misikitini. Title tu ya kitabu chenyewe na aina ya uwasilishaji wa maelezo yako, vinatosha kujua nini kimeandikwa ndani ya hiki kitabu. Yaleyale.......kama kawaida yenu.
Mbussi,
Unasema sichoki na ''ngonjera,'' za wapigania uhuru.
Lakini naindikayo si ngonjera.

Laiti ningeliandika ngonjera kitabu changu kisingitiwa katika Cambridge Journal of African History.

Laiti ningeliandika ngonjera nisingekuwamo katika Dictionary of African History (DAB).

Wala kitabu hiki kisingebadili historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika na historia ya Julius Nyerere.

Umeghadhibika na unakihusisha kitabu changu na udini na msikiti.

Kitabu cha Abdul Sykes ni kitabu kinachoeleza historia ya uhuru wa Tanganyika hakihusiani na dini wala na msikiti isipokuwa kitabu kinaeleza mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nimeandika kitabu hiki baada ya kugundua kuwa historia ya kweli imefutwa kwa hofu ya hilo.

Bahati mbaya hasira zimekuvaa na hasira humpunguzia mtu uwezo wa fikra nzuri.

Iangalie video hii hapo chini kisha ukimaliza tafakari:

Father...
Wote hao ni Watanzania ingawa ni Wamanyema.

Wamanyema wana historia kubwa sana katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nitakuonjesha kidogo:

View attachment 2649364
Kulia ni Hamisi Taratibu Muasisi wa TANU Dodoma Central Province, (Mmanyema), Saadan Abdu Kandoro (Mmanyema) katika waasisi 17 wa TANU, Julius Nyerere (Mzanaki), Sheikh Mohamed Ramiyya (Mmanyema) kiongozi wa TAA na TANU Bagamoyo na Iddi Faiz Mafongo (Mmanyema) Mweka Hazina wa Kwanza wa TANU kati ya watu wasiozidi 20 waliohudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Ukumbi wa Arnautoglo na mkusanyaji wa fedha sasfari ya kwanza ya Nyerere UNO 1955.

Picha imepigwa Dodoma Railway Station mwaka wa 1955 wakati wa kuisambaza TANU majimboni na kupigania uhuru.
Hatakuelewa . Tuendelee mzee mohamed said
 
Mzee wangu Said, huchoki na ngonjera za wapigania Uhuru? John Okelo alishiriki mapinduzi kule Zanzibar, je, nae ni Mzanzibar? Swala hapa si kuasisi chama wala kupigania Uhuru, hisipokuwa ni kwamba kuna Watanzania wenye asili ya Wamanyema wa Kongo. Kuwa Mmanyema hakuwezi kukuondoleeni Utanzania wenu kama ilivyo kwa Wamasaai, wako Kenya na wengine Tz, Wamakonde, Wajaruo nk.

Issue kubwa hapa ni maudhui ya vitabu mnavyoviandika. Kama vinahubiri udini na chuki bora usitueleze hapa jf, kaelezaneni uko misikitini. Title tu ya kitabu chenyewe na aina ya uwasilishaji wa maelezo yako, vinatosha kujua nini kimeandikwa ndani ya hiki kitabu. Yaleyale.......kama kawaida yenu.
Huyu mzee wetu anauchukia sana
Ukrst.....huo ndiyo ukweli

Ova
 
Huyu mzee wetu anauchukia sana
Ukrst.....huo ndiyo ukweli

Ova
Mrangi...
Kuandika historia ya kweli na kueleza mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika ndiyo kuwa na chuki?

Ningekuwa na chuki ningekuwa Mwandushi Bora hapa JF Ukumbi wa Historia kwa miaka miwili mfululizo 2021 na 2022?

Ningekuwa na chuki ningekuwa natafutwa na vyombo vya habari kwa mahojiano kuhusu historia ya Tanganyika na historia ya Julius Nyerere?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom