Kitabu gani ambacho kimewahi kubadilisha maisha yako na unatamani wengine tukisome?

Kuna vitabu vitatu ambavyo vimeshangia kubadili maisha yangu kwa kiwango kikubwa sana. Ningependekeza kila mtanzania avisome.
1. THINK AND GROW RICH
Hiki kimenisaidia kuweza kufikia uwezo mkubwa ulio ndani yangu na kuniwezesha kuona fursa nyingi zinazonizunguka.
2. RICH DAD, POOR DAD
Hiki kimenisaidia kuhusu utofauti kati ya elimu ya darasani na elimu halisi ya mtaani. Kimenisaidia kuona mambo ambayo nilifichwa darasani na ambayo ni ya msingi sana ili kufanikiwa.
3. THE RICHEST MAN IN BABYLON
Hiki kimenisaidia kuhusiana na maswala yote yanayohusuana na fedha kuanzia kuweka akiba mpaka kuwekeza. Kimeniwezesha kuweza kujilipa mimi mwenyewe hata kwa kipato kidogo sana na kuweza kujenga akiba iliyotosha kuanzia biashara.
Hivyo ni vitabu ambavyo natamani kila mtanzania avisome. Kama huna vitabu hivi nitumie email kwenye amakirita@gmail.com na nitakutumia vyote vitatu bure kabisa.
Au unaweza kutembelea AMKA MTANZANIA na ukajifunza mengi pamoja na uchambuzi wa vitabu hivi.

Wote mlionitumia emails nimeshawatumia vitabu hivyo vitatu.
 
Vitabu vinauwezo wa
kubadili kabisa maisha ya mtu yeyote yule. Baada ya vita vya pili ya
dunia wajapan walikuja na nadhalia iitwayo KAIZEN (Continuous improve),
yaani angalau kila siku uongeze kitu kipya kichwani chenye kukuza uelewa
wako na kuboresha maisha yako kwa njia yeyote ile.

hapa tujadili nguvu ya vitabu katika maisha ya mtu. yawezekana ulisoma
wewe au umewahi kukisikia kwa watu tushirikishane.

Kuna wengi tumebadilishwa au kuboreshwa maishani mwetu kiafya, kijamii,
kibiashara, kitaaruma,kimitazamo, kiimani, kimwili, mausihano nk kupitia
vitabu.

Kitabu gani ambacho kiligusa maisha yako au kukubadilisha na unatamani
wanajf wenzako tujifunze pia. unaweza kueleza kimekusaidiaje kwa ufupi
kama hutojali.
BIBLIA ni kitabu pekee kilichnbadili na kinaendelea kubadili maisha yangu kila ningpoendelea kukisoma. Jaribu na wewe.
 
The book tittled "THINK BIG" by Ben Carson (MD&Professor of neurosurgery)
Hiki ni mwanzo mwisho, kama unataka kubadili maisha yako kitafute na ukisome
 
Hiki hapa!! U never get bored at all.
 

Attachments

  • 1398615795806.jpg
    1398615795806.jpg
    49.8 KB · Views: 446
Jinsi ya kukamata mzunguko wa pesa.
Nguvu ya maombi ya rehema.
Vitabu hivi vimenibadilisha sana na hata uchumi wangu.
Mwandishi ni NABII BG MALISA
 
Animal Farm cha George Orwell! Kinaweka bayana songombingo za siasa katika jamii vile ambavyo watu wanaweza kuw na mtazamo wa pamoja kuleta mabadiliko na hatimaye wakishamwondoa yule wanayeamini hafai basi wenyewe kwa wenyewe wanaanza kubaguana!
 
Back
Top Bottom