Karibu kwenye klabu ya kusoma vitabu mtandaoni (online book club)

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,781
3,072
Rafiki yangu mpendwa,

Ukiniuliza ni kitu gani ambacho mtu yeyote akikifanya anaweza kubadili kabisa maisha yake na yakawa bora, sitafikiria mara mbili.
Nitakujibu mara moja kwamba ni USOMAJI WA VITABU.

Ninaamini mno kwenye usomaji wa vitabu, vimebadili mno maisha yangu na kila ambaye nimemshauri asome vitabu na akafanya hivyo, ameweza kuona matokeo mazuri kwenye maisha yake.

Ndiyo maana nimekuwa nashauri mno kila mtu asome vitabu. Kama mtu hasomi vitabu, huwa naamini kabisa kwamba anajinyima fursa nzuri ya kuyabadili maisha yake na kuwa bora.

online_book_club__with_devices_.jpg
Tangu mwaka 2012 nimekuwa na harakati mbalimbali za kuwashawishi na kuwahamasisha watu kusoma vitabu. Hii ni baada ya mimi binafsi kuweza kuyageuza maisha yangu kupitia vitabu vitatu nilivyosoma na kuanza kufanyia kazi mwaka huo.

Nilianza kwa kuwatumia mtu mmoja mmoja mmoja vitabu hivyo vitatu kwenye email yake. Niliweza kuwatumia watu wengi na baadaye nikatengeneza mfumo rahisi wa mtu kupata vitabu hivyo.

Baadaye tulianzisha kundi la Telegram linaloitwa Tanzania Voracious Readers ambapo lengo lilikuwa kusoma vitabu 2 kila wiki ili kufikisha vitabu 100 kila mwaka. Kwa miaka mitatu ambapo kundi hilo lilikuwa hai, tuliweza kushirikishana vitabu visivyopungua 300.

Nikaja kuanzisha programu ya KURASA KUMI ZA KITABU KILA SIKU. Lengo la programu hii ilikuwa kumsaidia yule ambaye bado hajawa na tabia ya usomaji basi aweze kuijenga kwa kusoma kurasa 10 tu za kitabu kila siku. Wengi walinufaika na programu hii na kujijengea tabia ya usomaji.

Kwa sasa tupo na programu ya SOMA VITABU TANZANIA, hii ni channel ambayo ipo kwenye mtandao wa Telegram ambapo mtu anapata vitabu na chambuzi zake. Lengo kuu la channel hii ni kuondoa kikwazo cha lugha kwa wengi, ambao wanashindwa kusoma vitabu vizuri ambavyo vipo kwa lugha ya kiingereza. Ndani ya channel hiyo, mtu anapata uchambuzi wa kina wa vitabu vizuri na kuweza kujifunza na kuboresha maisha yake.

soma-vitabu-logo.jpg

Katika hatua zote ambazo nimekuwa nachukua kuwasaidia watu kujenga tabia ya usomaji, nimejifunza mambo gani yanafanya kazi na yapi hayafanyi kazi vizuri katika kuwasaidia watu kujenga tabia ya usomaji.

Leo ninayo furaha ya kuleta kwako kitu kipya, kitu ambacho hakijawahi kuwepo kwenye usomaji wa vitabu hapa Tanzania.
Kitu hicho ni klabu ya usomaji wa vitabu ya mtandaoni (online book club).
Yapo makundi mbalimbali ya usomaji na ambayo huendesha mijadala ya vitabu, lakini sasa tunakuja na kitu cha tofauti.

Kitu cha tofauti kwenye klabu hii mpya ni kila wiki tunakuwa na mjadala wa moja kwa moja (live) ambapo kila mtu anapata nafasi ya kuongea ambapo anashirikisha yale aliyojifunza kwenye kitabu cha wiki husika.

Kwa sasa teknolojia imekua sana na inatoa nafasi ya watu kushiriki mijadala ya moja kwa moja wakiwa popote duniani.
Kupitia channel ya SOMA VITABU TANZANIA, tutakuwa na klabu ya usomaji vitabu na kuwa na mjadala wa vitabu kila wiki.

Mijadala ya klabu ya soma vitabu itakuwa kila siku ya jumamosi, kuanzia saa mbili kamili usiku mpaka saa nne kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Katika mjadala huo kwa pamoja tunajadiliana yale tuliyojifunza kwenye kitabu na hatua ambazo kila mmoja wetu anakwenda kuchukua kwenye maisha yake.

Hii ni fursa ya kipekee sana ambayo msomaji yeyote wa vitabu au anayetaka kuwa msomaji hapaswi kuikosa.

Kuna faida nyingi za kuwa kwenye klabu hii ya mtandaoni ya kusoma vitabu, kubwa kabisa ni hizi;

1. Haijalishi uko eneo gani, unaweza kushiriki. Ukishakuwa tu na mtandao wa intaneti, unaweza kuwa kwenye klabu. Huhitaji kuacha mambo yako ili kwenda kuhudhuria mikutano ya klabu ya usomaji vitabu, ni wewe kutenga muda na kushiriki ukiwa popote.

2. Inakupa msukumo wa kusoma vitabu. Pale unapojua unakwenda kushiriki mjadala wa moja kwa moja wa kitabu, lazima ufanye maandalizi, usome kitabu au uchambuzi wake ili uwe na cha kuchangia. Hilo linakusukuma ujenge tabia ya kusoma.

3. Unapata nafasi ya kujifunza kutoka kwa wengine. Watu wawili wanaweza kusoma kitabu kimoja, ila kila mmoja akaondoka na mafunzo tofauti kabisa, kutokana na mtazamo alionao na uzoefu wake pia.
Unaposhiriki mjadala wa moja kwa moja, unapata nafasi ya kujifunza kutoka kwa wengine, kwa namna walivyoelewa wao kitabu husika.

4. Inakusukuma ujifunze kwa kina na uondoke na kitu cha kwenda kufanyia kazi. Unaposoma kitabu peke yako, ni rahisi kukimbilia kukimaliza na ukatoka hujajifunza chochote. Lakini unapokuwa kwenye klabu, unajua unapaswa kushirikisha ulichosoma na hatua unazokwenda kuchukua, hilo linakusukuma ujifunze kwa kina.
Hutamaliza tu kusoma vitabu, bali pia utajifunza vitu vya kufanyia kazi.

5. Unajijenga kuwa muwasilishaji mzuri. Kwa kujua unakwenda kushirikisha wengine kwenye mjadala, unajenga hoja zako vizuri kitu ambacho kinakufanya uwe muwasilishaji mzuri.

Rafiki, kwa faida hizo na nyingine nyingi, nakukaribisha sana kwenye klabu ya kusoma vitabu ya SOMA VITABU TANZANIA. Kujiunga na klabu hii tuma ujumbe kwa telegram kwenda namba 0717 396 253 ukieleza unataka kuwa mwanachama wa klabu ya SOMA VITABU.

images.jpeg-30.jpg

Kitabu cha wiki ya 27 2021.
Mjadala wa wiki hii ya 27 ya mwaka 2021 ambao utakuwa siku ya jumamosi tarehe 11/07/2021 ni wa kitabu cha LIMITLESS kilichoandikwa na Jim Kwik.
Kitabu hicho kinaeleza maeneo matatu ya kuondoa ukomo kwenye maisha yako ili uweze kupata chochote unachotaka.
Kitabu tayari nimekichambua kwa kina na uchambuzi uko kwenye channel.
Pata muda usome uchambuzi huo ili siku ya mjadala ushirikishe yale uliyojifunza na hatua unazokwenda kuchukua ili kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi.

Karibu sana kwenye SOMA VITABU BOOK CLUB ili ushiriki mijadala ya vitabu ya moja kwa moja kila jumamosi kuanzia saa 2 usiku mpaka saa 4 usiku saa za Afrika Mashariki.
Kujiunga kwenye klabu tuma ujumbe sasa kwa telegram kwenda namba 0717 396 253 wenye maneno KLABU YA SOMA VITABU na utaunganishwa.

Njia rahisi na ya uhakika ya wewe kuyabadili maisha yako ili yawe bora sana ni kupitia usomaji wa vitabu.
Karibu twende pamoja kupitia SOMA VITABU BOOK CLUB.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.
 
Umesema lengo kuu ni kuondoa kikwazo cha lugha kwa wasiojua lugha ya kiingereza kwa kuwa vitabu vingi vimeandikwa kwa lugha hiyo.
Naomba kujua huyu mwenye tatizo la lugha utamsaidiaje ili naye awe ni msomaji wa vitabu katika channel yako
 
Karibu mkuu,
Vitabu navichambua kwa kina kwa lugha rahisi kabisa ya Kiswahili hivyo mtu anapata nafasi ya kuelewa kilicho kwenye kitabu na hatua anazoweza kuchukua.
Hapa naambatanisha uchambuzi wa kitabu cha LIMITLESS tutakachojadiliana wiki hii, uone mfano wa uchambuzi ninaofanya unavyorahisisha.
Fungua attachment.
 
Attachments

  • UCHAMBUZI;_LIMITLESS;_Upgrade_Your_Brain,_Learn_Anything_Faster.PDF
    123.5 KB · Views: 142
Inapendeza sana, tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Rafiki yangu mpendwa,

Ukiniuliza ni kitu gani ambacho mtu yeyote akikifanya anaweza kubadili kabisa maisha yake na yakawa bora, sitafikiria mara mbili.
Nitakujibu mara moja kwamba ni USOMAJI WA VITABU.

Ninaamini mno kwenye usomaji wa vitabu, vimebadili mno maisha yangu na kila ambaye nimemshauri asome vitabu na akafanya hivyo, ameweza kuona matokeo mazuri kwenye maisha yake.

Ndiyo maana nimekuwa nashauri mno kila mtu asome vitabu. Kama mtu hasomi vitabu, huwa naamini kabisa kwamba anajinyima fursa nzuri ya kuyabadili maisha yake na kuwa bora.

online_book_club__with_devices_.jpg
Tangu mwaka 2012 nimekuwa na harakati mbalimbali za kuwashawishi na kuwahamasisha watu kusoma vitabu. Hii ni baada ya mimi binafsi kuweza kuyageuza maisha yangu kupitia vitabu vitatu nilivyosoma na kuanza kufanyia kazi mwaka huo.

Nilianza kwa kuwatumia mtu mmoja mmoja mmoja vitabu hivyo vitatu kwenye email yake. Niliweza kuwatumia watu wengi na baadaye nikatengeneza mfumo rahisi wa mtu kupata vitabu hivyo.

Baadaye tulianzisha kundi la Telegram linaloitwa Tanzania Voracious Readers ambapo lengo lilikuwa kusoma vitabu 2 kila wiki ili kufikisha vitabu 100 kila mwaka. Kwa miaka mitatu ambapo kundi hilo lilikuwa hai, tuliweza kushirikishana vitabu visivyopungua 300.

Nikaja kuanzisha programu ya KURASA KUMI ZA KITABU KILA SIKU. Lengo la programu hii ilikuwa kumsaidia yule ambaye bado hajawa na tabia ya usomaji basi aweze kuijenga kwa kusoma kurasa 10 tu za kitabu kila siku. Wengi walinufaika na programu hii na kujijengea tabia ya usomaji.

Kwa sasa tupo na programu ya SOMA VITABU TANZANIA, hii ni channel ambayo ipo kwenye mtandao wa Telegram ambapo mtu anapata vitabu na chambuzi zake. Lengo kuu la channel hii ni kuondoa kikwazo cha lugha kwa wengi, ambao wanashindwa kusoma vitabu vizuri ambavyo vipo kwa lugha ya kiingereza. Ndani ya channel hiyo, mtu anapata uchambuzi wa kina wa vitabu vizuri na kuweza kujifunza na kuboresha maisha yake.

soma-vitabu-logo.jpg

Katika hatua zote ambazo nimekuwa nachukua kuwasaidia watu kujenga tabia ya usomaji, nimejifunza mambo gani yanafanya kazi na yapi hayafanyi kazi vizuri katika kuwasaidia watu kujenga tabia ya usomaji.

Leo ninayo furaha ya kuleta kwako kitu kipya, kitu ambacho hakijawahi kuwepo kwenye usomaji wa vitabu hapa Tanzania.
Kitu hicho ni klabu ya usomaji wa vitabu ya mtandaoni (online book club).
Yapo makundi mbalimbali ya usomaji na ambayo huendesha mijadala ya vitabu, lakini sasa tunakuja na kitu cha tofauti.

Kitu cha tofauti kwenye klabu hii mpya ni kila wiki tunakuwa na mjadala wa moja kwa moja (live) ambapo kila mtu anapata nafasi ya kuongea ambapo anashirikisha yale aliyojifunza kwenye kitabu cha wiki husika.

Kwa sasa teknolojia imekua sana na inatoa nafasi ya watu kushiriki mijadala ya moja kwa moja wakiwa popote duniani.
Kupitia channel ya SOMA VITABU TANZANIA, tutakuwa na klabu ya usomaji vitabu na kuwa na mjadala wa vitabu kila wiki.

Mijadala ya klabu ya soma vitabu itakuwa kila siku ya jumamosi, kuanzia saa mbili kamili usiku mpaka saa nne kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Katika mjadala huo kwa pamoja tunajadiliana yale tuliyojifunza kwenye kitabu na hatua ambazo kila mmoja wetu anakwenda kuchukua kwenye maisha yake.

Hii ni fursa ya kipekee sana ambayo msomaji yeyote wa vitabu au anayetaka kuwa msomaji hapaswi kuikosa.

Kuna faida nyingi za kuwa kwenye klabu hii ya mtandaoni ya kusoma vitabu, kubwa kabisa ni hizi;

1. Haijalishi uko eneo gani, unaweza kushiriki. Ukishakuwa tu na mtandao wa intaneti, unaweza kuwa kwenye klabu. Huhitaji kuacha mambo yako ili kwenda kuhudhuria mikutano ya klabu ya usomaji vitabu, ni wewe kutenga muda na kushiriki ukiwa popote.

2. Inakupa msukumo wa kusoma vitabu. Pale unapojua unakwenda kushiriki mjadala wa moja kwa moja wa kitabu, lazima ufanye maandalizi, usome kitabu au uchambuzi wake ili uwe na cha kuchangia. Hilo linakusukuma ujenge tabia ya kusoma.

3. Unapata nafasi ya kujifunza kutoka kwa wengine. Watu wawili wanaweza kusoma kitabu kimoja, ila kila mmoja akaondoka na mafunzo tofauti kabisa, kutokana na mtazamo alionao na uzoefu wake pia.
Unaposhiriki mjadala wa moja kwa moja, unapata nafasi ya kujifunza kutoka kwa wengine, kwa namna walivyoelewa wao kitabu husika.

4. Inakusukuma ujifunze kwa kina na uondoke na kitu cha kwenda kufanyia kazi. Unaposoma kitabu peke yako, ni rahisi kukimbilia kukimaliza na ukatoka hujajifunza chochote. Lakini unapokuwa kwenye klabu, unajua unapaswa kushirikisha ulichosoma na hatua unazokwenda kuchukua, hilo linakusukuma ujifunze kwa kina.
Hutamaliza tu kusoma vitabu, bali pia utajifunza vitu vya kufanyia kazi.

5. Unajijenga kuwa muwasilishaji mzuri. Kwa kujua unakwenda kushirikisha wengine kwenye mjadala, unajenga hoja zako vizuri kitu ambacho kinakufanya uwe muwasilishaji mzuri.

Rafiki, kwa faida hizo na nyingine nyingi, nakukaribisha sana kwenye klabu ya kusoma vitabu ya SOMA VITABU TANZANIA. Kujiunga na klabu hii tuma ujumbe kwa telegram kwenda namba 0717 396 253 ukieleza unataka kuwa mwanachama wa klabu ya SOMA VITABU.

images.jpeg-30.jpg

Kitabu cha wiki ya 27 2021.
Mjadala wa wiki hii ya 27 ya mwaka 2021 ambao utakuwa siku ya jumamosi tarehe 11/07/2021 ni wa kitabu cha LIMITLESS kilichoandikwa na Jim Kwik.
Kitabu hicho kinaeleza maeneo matatu ya kuondoa ukomo kwenye maisha yako ili uweze kupata chochote unachotaka.
Kitabu tayari nimekichambua kwa kina na uchambuzi uko kwenye channel.
Pata muda usome uchambuzi huo ili siku ya mjadala ushirikishe yale uliyojifunza na hatua unazokwenda kuchukua ili kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi.

Karibu sana kwenye SOMA VITABU BOOK CLUB ili ushiriki mijadala ya vitabu ya moja kwa moja kila jumamosi kuanzia saa 2 usiku mpaka saa 4 usiku saa za Afrika Mashariki.
Kujiunga kwenye klabu tuma ujumbe sasa kwa telegram kwenda namba 0717 396 253 wenye maneno KLABU YA SOMA VITABU na utaunganishwa.

Njia rahisi na ya uhakika ya wewe kuyabadili maisha yako ili yawe bora sana ni kupitia usomaji wa vitabu.
Karibu twende pamoja kupitia SOMA VITABU BOOK CLUB.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.
Safi Sana
 
“genocide and covert operations in Africa “.. naomba msaada wa kupata hiki kitabu mbinu ninazozifahamu imeshindikana…
 
Back
Top Bottom