Kitabu cha Panga la Shaba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitabu cha Panga la Shaba

Discussion in 'Entertainment' started by 3D., Jan 4, 2012.

 1. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2012
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wakuu,

  Hivi kuna mtu anaweza kunipa idea wapi nitapata kitabu cha zamani cha katuni za Mganga "Panga la Shaba"?

  Natanguliza shurani.
   
 2. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #2
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Kuna mtu mmoja yupo Tanga, alikuwa mtendaji kipindi kile
  kwenye jarida la Sani na anacho, nilikiona kwake wakati
  tukijadili mambo fulani. Ngoja nitaongea naye kisha nitakujulisha
  kama unaweza kukipata, japo ukatoa copy...
   
 3. ram

  ram JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,203
  Likes Received: 905
  Trophy Points: 280
  Aise Bishop ukikipata, plz toa copy mbili, mi pia nakihitaji, halafu nisaidieni natafuta kitabu cha KULI, tulikitumia sekondari ktk somo la kiswahili, ukivipata ni-pm mkuu
  Barikiwa hadi ushangae Bishop!

   
 4. Relief

  Relief JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  na mimi nataka copy mkuu
   
 5. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2012
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Aisee utakuwa umenisaidia sana. Actually, hata kama ningekipata kwa mtu mwingine.. mpango wa kukutafuta wewe binafsi ninao. Ningependa tuzungumze mambo kadhaa juu ya filamu za Tanzania na duniani kwa ujumla. Watu wa Sani wana hazina ya vitabu. Nadhani kitabu hicho kilichorwa na John M. Kaduma ambaye alikuwa mchoraji mkuu wa Sani wakati huo (Ameinfluence sana uchoraji wangu). Kuna kitabu kingine cha watu wa Sani kilikuwa kinaitwa "Usiku wa balaa" .. ni version fulani ya stori za akina Mzee Ole. Kilikuwa kizuri.. nilikisoma utotoni. Kikipatikana hiki pia itakuwa poa. Natanguliza shukrani.
   
 6. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #6
  Jan 12, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Hivi vitabu huyu mtu anavyo, alinionesha wakati akitafuta
  moja ya hadithi ambayo alitaka nimuandikie script ya filamu
  ili aangalie uwezekano wa kutengeneza movie...
   
 7. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #7
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Actually, kusudio langu la kukitaka kitabu hicho ni kuona ikiwa kina uzito ule ule nilioupata nilipokisoma utotoni (nadhani nilisomewa maana kwa wakati huo very likely nilikuwa sijui kusoma... sina kumbukumbu nzuri). Kama stori yake itakuwa ina uzito huo nakusudia kutengenezea sinema hasa kama imagination na level nayoikusudia inaweza kutekelezeka (kutengenezeka) hapa Tanzania.

  Kuna baadhi ya hadithi na simulizi za Tanzania ambazo ni excellent kwa kutengeneza sinema kuliko kuwa na themes zile zile ambazo kwa sasa zinalalamikiwa sana. Asante Bishop.
   
 8. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Ikibidi utuwekee kabisa hapa jf tu-download na kuprint wenyewe mana naona wahitaji wanaongezeka.
   
 9. Muuza Sura

  Muuza Sura JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,990
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Dah!panga la shaba nakumbuka ila sikumbuki ilikuwa inahusu nini!bab kubwa
   
 10. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Nenda bakita utapata vyote.
   
 11. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #11
  Jan 19, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Panga la shaba alikuwa anakula totoz nzuri sana baada ya kuziroga. kipindi ile ilikuwa kama kweli vile hadi mtu unaskia huzuni yani.
   
 12. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,998
  Likes Received: 2,653
  Trophy Points: 280
  Panga la shaba alikuwa ni mganga wa kienyeji, alikuwa anapenda sana kusafiri na mtoto wake aliyekuwa anitwa ufudu,aisee kale kajarida kalikuwa kazuzi sana.
   
 13. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #13
  Jan 19, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,998
  Likes Received: 2,653
  Trophy Points: 280
  Alafu siku moja akiwa kwenye ungo na ufudu,wanapepea kuelekea makaburini ufudu akaona ndege inapita akamuuliza baba na yetu iko kama ile?yaani kama kweli vile.
   
 14. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #14
  Jan 22, 2012
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Asante kwa taarifa mkuu. Ila BAKITA wanauza vitabu ama kuna alternative wanatoa?
   
 15. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #15
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  wazo zuri mkuu.
  Usisahau mrabaha wa hao wenye wazo chanzi katika filamu yako.
  Au sio?
   
 16. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #16
  Jan 24, 2012
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 135
  Hebu tuvute kumbukumbu ya ile issue kwa ufupi...

  Suzzy baada ya kutafuta cheo kazini kwa muda mrefu bila mafanikio anadokezwa na shoga yake juu ya mganga makini Panga la Shaba(PLS) ambae anaweza kumtatulia tatizo hilo. Suzzy akiwa na company ya rafiki yake wanafunga safari kwenda bush huku akimdanganya mumewe kuwa ana safari ya kikazi na kumwacha mwanae mdogo akiwa na babaye.

  Huko kujijini PLS anapatata ugeni na kama kawaida yake anaandaa mkakati wa kumpata mtoto Suzzy. Safari ya pili ya Suzzy kumuona mganga anaamua kwenda bila shoga yake na hapo ndipo PLB anaamua kuweka "limbwata" kali katika msosi hivyo kumfanya Sussy kusahau kila kitu na kujikuta akianza maisha mapya. Suzzy mwanamke mrembo mwenye maisha mazuri anachakaa (anafulia) kiasi cha kupoteza mvuto na mwonekano wa awali na anajifungua mtoto ambae ni "photocopy ya Panga la Shaba". Ufudu mtoto wa PLS, mwenye ujuzi wa kukamata panya ambao ndio kitoweo kikubwa katika familia ya PLS anakuwa kivutio kwa utundu wake na pilika za hapa na pale ikiwamo kujifunza uchawi wa mzee wake.

  Huko town baada ya miaka kadhaa ya kupotea kwa Suzzy mumewe anapata taarifa kutoka kwa rafikiye Suzzy juu ya uwezekano wa mganga tapeli Panga la Shaba kuwa ndo mwizi wao. Mumewe kwa kushirikiana na maafande "wenye hasira" pamoja na rafikiye Suzzy wanadondoka huko bush mafichoni kwa mzee PLS. Baada ya kuwasili "timbwili" kali linaibuka ambapo maafande wanatembeza kichapo kikali na kufanikiwa kumkamata mganga huyo fuska na tapeli na anafikishwa mahakamani.

  Katika hitimisho ambalo ni la kusikitisha sana Suzzy akiwa kachakaa na kuchoka vibaya (choka mbaya) anamkana mumewe na kumg'ang'ania mchawi Panga la shaba kuwa ndiye mumewe halali hivyo wanaachiwa huru na kurudi mafichoni huku mumewe akilia machozi. Katika safari yao ya kurudi bush Ufudu anaonyesha mbwembwe kwa kukimbiza panya vichakani huku fedhuli PLS akitabasamu tukio linaloashiria kwamba hakimu/jaji hakufanikiwa kufurukuta juu ya ndumba za mchawi huyo.

  Aisee mkuu 3D, ukitengeneza movie yake utakuwa umefanya jambo la maana.
   
 17. T

  THE WHITE ELEPHANT Member

  #17
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MIMI NAVITAFUTA SANA VITABU VYA WILLY GAMBA VYOTE ANZIA NJAMA,KIKOSI CHA KISASI,HOFU....VILITUNGWA MUSIBBA,NITAVIPATA WAPI KWA GHARAMA YEYOTE ILE WADAU,NI E MAIL hapa ruttajunior@yahoo.com
   
 18. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #18
  Jan 24, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Vipo kwa wauzaji wa vitabu... E. Musiba (Willy Gamba) na Ben Mtobwa (Joram Kiango)
  kabla ya umauti wao walishaanza kuvichapa upya vitabu vyao na kuviingiza tena kwenye soko.
  Naamini ukiwafuata wauzaji wa vitabu utavipata bila shaka, vinginevyo nitaulizia halafu nitakujulisha
  through email yako...
   
 19. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #19
  Jan 24, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Mgalanjuka,

  Sikutegemea kama bado tuna watu wana kumbukumbu ya kiwango hiki,
  maana siku hizi Wa-tz wamekuwa wavivu hadi kwenye kufikiri. Hongera
  sana mkuu...
   
 20. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #20
  Jan 24, 2012
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 135
  Asante mkuu Bishop, nadhani pia kwa kuwa kitabu chenyewe kilikuwa kwa style ya comics inachangia kumbukumbu kutofutika kirahisi. Unakuwa na mental picture ya characters wote mpaka wale maafande wawili mmoja mfupiii na kofia yake inayofunika nusu ya uso.
   
Loading...