Wakuu,
Hivi kuna mtu anaweza kunipa idea wapi nitapata kitabu cha zamani cha katuni za Mganga "Panga la Shaba"?
Natanguliza shurani.
Kuna mtu mmoja yupo Tanga, alikuwa mtendaji kipindi kile
kwenye jarida la Sani na anacho, nilikiona kwake wakati
tukijadili mambo fulani. Ngoja nitaongea naye kisha nitakujulisha
kama unaweza kukipata, japo ukatoa copy...

Aisee utakuwa umenisaidia sana. Actually, hata kama ningekipata kwa mtu mwingine.. mpango wa kukutafuta wewe binafsi ninao. Ningependa tuzungumze mambo kadhaa juu ya filamu za Tanzania na duniani kwa ujumla. Watu wa Sani wana hazina ya vitabu. Nadhani kitabu hicho kilichorwa na John M. Kaduma ambaye alikuwa mchoraji mkuu wa Sani wakati huo (Ameinfluence sana uchoraji wangu). Kuna kitabu kingine cha watu wa Sani kilikuwa kinaitwa "Usiku wa balaa" .. ni version fulani ya stori za akina Mzee Ole. Kilikuwa kizuri.. nilikisoma utotoni. Kikipatikana hiki pia itakuwa poa. Natanguliza shukrani.
Hivi vitabu huyu mtu anavyo, alinionesha wakati akitafuta
moja ya hadithi ambayo alitaka nimuandikie script ya filamu
ili aangalie uwezekano wa kutengeneza movie...
Dah!panga la shaba nakumbuka ila sikumbuki ilikuwa inahusu nini!bab kubwa
Panga la shaba alikuwa anakula totoz nzuri sana baada ya kuziroga. kipindi ile ilikuwa kama kweli vile hadi mtu unaskia huzuni yani.
Actually, kusudio langu la kukitaka kitabu hicho ni kuona ikiwa kina uzito ule ule nilioupata nilipokisoma utotoni (nadhani nilisomewa maana kwa wakati huo very likely nilikuwa sijui kusoma... sina kumbukumbu nzuri). Kama stori yake itakuwa ina uzito huo nakusudia kutengenezea sinema hasa kama imagination na level nayoikusudia inaweza kutekelezeka (kutengenezeka) hapa Tanzania.
Kuna baadhi ya hadithi na simulizi za Tanzania ambazo ni excellent kwa kutengeneza sinema kuliko kuwa na themes zile zile ambazo kwa sasa zinalalamikiwa sana. Asante Bishop.
Panga la shaba alikuwa anakula totoz nzuri sana baada ya kuziroga. kipindi ile ilikuwa kama kweli vile hadi mtu unaskia huzuni yani.
Kuna mtu mmoja yupo Tanga, alikuwa mtendaji kipindi kile
kwenye jarida la Sani na anacho, nilikiona kwake wakati
tukijadili mambo fulani. Ngoja nitaongea naye kisha nitakujulisha
kama unaweza kukipata, japo ukatoa copy...
MIMI NAVITAFUTA SANA VITABU VYA WILLY GAMBA VYOTE ANZIA NJAMA,KIKOSI CHA KISASI,HOFU....VILITUNGWA MUSIBBA,NITAVIPATA WAPI KWA GHARAMA YEYOTE ILE WADAU,NI E MAIL hapa ruttajunior@yahoo.com
Mgalanjuka,
Sikutegemea kama bado tuna watu wana kumbukumbu ya kiwango hiki,
maana siku hizi Wa-tz wamekuwa wavivu hadi kwenye kufikiri. Hongera
sana mkuu...