Kitabu cha Mwanzo katika Bible ndio msingi wa mambo matatu duniani! Intelijensia, Sayansi na Uchawi

@bazazi
Moja ya sababu kwa nini ni mfuasi wako ktk mada chonganishi na fikirishi. Majibu Kuntu toka kwa swali la mtu mjinga asiye na weledi. Mtu anayedhani dini yake ndio ya Mungu na zingine ni za kubumba. Hajiulizi ikiwa ni ya Mungu kwanini hazifuti na kuiacha yake tu.

Bazazi

Sent using Jamii Forums mobile app

Jr
 
@zitto junior big up sana... Uko deep kwenye maandiko pamoja na historia yake.... Natamani siku moja tuonane ana kwa ana.... Nataka niachane kabisa na ulozi nikipata mtu wa kumkabidhi mfuko
@Mshana Jr

Jinga sana wewe!
Umenifanya ncheke
Ncheke kwa sauti
Yani! kama kichaa
Watu hawanielewi
Nacheka nini hasa
Kumbe jibu hovyo
Ndio toka kwako

Bazazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi Genesis inatokna na lugha gani ni kiebrania au? na je ni kweli ina maana ya "mwanzo"?
1588830931729.png
 
Jina huathiri muktadha, asili, chanzo na uhalisia wa kitu..... Kitabu cha MWANZO katika Biblia takatifu ndicho kitabu msingi kinachosomwa zaidi duniani... Tena na imani na dini zote...
Nukuu na rejea nyingi kwenye malumbano mijadala, tafiti za kisayansi, tafiti za kilozi na kishirikina, ulimwengu wa nguvu ya 'supernatunal powers (nguvu zisizomithilika) na hata maandiko mbalimbali yahusuyo asili na chanzo cha ulimwengu... Huwezi kuacha kutaja kitabu hiki....
Masomo ya sayansi, fizikia, baiolojia, historia, kemia historia, filosofia uchawi na ulozi.. Yote haya katika ujumla wake unayapata katika kitabu hiki cha MWANZO....
Unaposoma... MUNGU AKATAMKA NA IKAWA... hii ni aina ya ushirikina, imani katika nguvu za asili na uwezo wa kuumba na kuunda kwa matamshi tu... Sayansi iwayo yote haina uwezo huu... Mambo hayo kwasasa ni ya manabii mitume na wachawi(wanga na washirikina)
Mungu anapotamka kuwa kaumba viumbe vyote... VINAVYOONEKANA NA VISIVYOONEKANA... mpaka leo hii sayansi imeshindwa kutoa jibu sahihi juu ya hivyo VISIVYOONEKANA!
Hapa ndipo inabidi turudi kwenye rejea ya kitabu cha MWANZO na kuona nini kilisemwa na kikawa halafu kikawaje! Na ndipo tunapata ufunuo wa ajabu na ugunduzi kwamba hii tunayoita SAYANSI YA ITHIBATI si chochote bali ni njia tu ya mwanadamu kujaribu kutafsiri kwa njia yake kile ambacho kilishaandikwa na kufanyika kwenye kitabu cha MWANZO
Hakuna kipya chini ya anga na kwa hakika bado hatujaweza kuvumbua kila kilichomo na kilichoandikwa kwenye zile kurasa chache za kitabu cha MWANZO
World encyclopedia, volumes kwa volumes za sutras, misahafu kwa misahafu, maandiko na mavitabu makubwa ya wanafilosofia maarufu kuwahi kutokea duniani... SUMMARY yao iko kwenye kitabu cha MWANZO

Kuna wenzetu wenye mawazo mbadala kuhusu Bible na kitabu cha mwanzo.. Ukiwa mwepezi wa tafakuri wanaweza kwa HAKIKA kabisa kukuteka na hoja zao mahiri kabisa lakini zisizo na hakika.. Ni wajenzi wazuri wa hoja zinazoteteresha kama wewe ni legelege lakini ukitulia na kutafakari hawana mwendelezo na hawaendi zaidi ya kilipokomea kitabu cha mwanzo...
Wataandika na kuchagiza kwa maneno mengi na misamiati huku wakiweka nukuu za wengine ambazo nazo zinaishia kwenye kuakisi kile kilichomo kwenye kitabu hicho cha mwanzo....
Tukirudi hapa JF hata jukwaa hili la intelligence kwa sehemu kubwa linatawaliwa na maandiko toka kitabu cha mwanzo...
Ni kwa Muktadha huu kitabu hiki cha MWANZO kinabaki kuwa chanzo kikuu, msingi, chimbuko na asili ya kila kitu katika maisha yetu ya kila siku... Iwe sayansi uchawi imani ama intelijensia....!!!
na pia mkuu,wakati moses anaandika kitabu cha mwanzo,alichukua reference kutoka katika kitabu cha kale zaidi na ndio maana tunapata habari za adam na hawa,abraham,nuhu japo kwa uchache ambao waliishi maelfu ya miaka nyuma kabla ya moses,hiyo inaonesha maandiko yana mambo mengi sana kiasi kama tungeandikiwa yote kama yalivyo naona hata robo tungekuwa hatujamaliza
 
In fact Bible ilikuja ku summarize ili iweze kusomeka kwa urahisi na kueleweka na wengi
 
Tukirudi hapa JF hata jukwaa hili la intelligence kwa sehemu kubwa linatawaliwa na maandiko toka kitabu cha mwanzo...
Ni kwa Muktadha huu kitabu hiki cha MWANZO kinabaki kuwa chanzo kikuu, msingi, chimbuko na asili ya kila kitu katika maisha yetu ya kila siku... Iwe sayansi uchawi imani ama intelijensia....!!!
 
Hongera somo zuri sana hili mchawi mstaafu. Unajitahidi sana. Mwaka huu tutaandamana kama JF hawatakupa tuzo, acknowldement na appreciation kwa kile ufanyacho.
 
Hongera somo zuri sana hili mchawi mstaafu. Unajitahidi sana. Mwaka huu tutaandamana kama JF hawatakupa tuzo, acknowldement na appreciation kwa kile ufanyacho.
Tusiandamane bali tuzidi kuombeana afya njema na uhai.. Wakipata wengine tumepata sisi pia kwakuwa sote tu familia moja kubwa
 
Tukirudi hapa JF hata jukwaa hili la intelligence kwa sehemu kubwa linatawaliwa na maandiko toka kitabu cha mwanzo...
Ni kwa Muktadha huu kitabu hiki cha MWANZO kinabaki kuwa chanzo kikuu, msingi, chimbuko na asili ya kila kitu katika maisha yetu ya kila siku... Iwe sayansi uchawi imani ama intelijensia....!!!
Ukisoma kitabu cha "The bill of Jubilee " kinaeleza vizuri namna gani Musa aliandika kitabu cha Mwanzo. Musa akiwa Mlimani kwa siku 40 ndipo Mungu kwa kupitia Malaika wake alimfunulia kuhusu toka uumbaji hadi Wana wa Israel kwenda Misri utumwani na kumwambia aandike hayo mafunuo.
 
Back
Top Bottom