Kiswanglish lugha inayopendwa na Watanzania

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,515
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari,

Pamoja na kuwa kiswahili ndio lugha ya Tanzania inayojulikana ila Kingereza ndio lugha ambayo inakubalika.

Hata hivyo kiswahili kimeendelea kuongelewa kwa kuchanganywa na lugha hii ya kigeni Kutoka huko Duniani.

Baadhi yao wanaongea kiswanglish huwa wanajiona kuwa wao ni wajanja sana.

Wakiwa wanaongea wanajiona kuwa wao ni wasomo sana.

Mara nyingi watu hawa wanaongea kiswanglish wanakuwa na maringo.

Sasa lugha hii inaanza kukipiku kiswahili maana ndio inatumika kwa wingi.

Sio kwa kuongea tu, hata kuandika kwenye mitandao kiswanglish kinatumika.

Baadhi yao ni wanawake ambao ndio kundi linalopenda sana kiswanglish.

Wanaume nao baadhi yao hawajaachwa nyuma nao wanakichapa kiswanglish sasa.

Kiswanglish kinapiku kiswahili.
 
Kiswahili hakina msamiati wa kutosha ili kuwezesha mawasiliano kuleta ile semantiki na kimantiki


Mimi huwa natumia lugha tatu kwa wakati mmoja
Kiswahili
Kihaya
Kingereza

Mfano nikienda kununua uji pale kwetu Bukoba natoa older yangu kwa mtindo huu.


"Ninshaba epoleji ya Mia"
👇
Naomba uji wa shilingi miamoja.
 
Uko sawa nafikiri ni kwa sababu ya mfumo pia wa hizi lugha mbili kuwa kama msingi wa watu wengi kwenye makuzi..Mfano Wanafunzi wa shule za msingi lugha kuu ya kufundishia(shule za seriksli) ni kiswahili ukichanganya ns kiingereza kwa uchache wakati huo pia wanapili wa sekondari lugha kuu ni kiingereza huku kiswahili ni kwa uchache.

Na hata ukizingatia muda wa hii mifumo ya lugha kutumika haipishani sana endapo Mtu ataishia kidato cha sita. Miaka saba msingi na miaka sita sekondari..Hili pia unaweza lielewa vizuri ikiwa unajamaa ambae kiswahili kwake sio lugha ya msingi ni rahisi sana kukuchanganyia kiswahili na lugha mama yake..

Lakini pia mfumo wa serikali yetu unatumia hizi lugha mbili kama lugha rasmi katika shughuli zake.

Kwaiyo ni suala lisilokwepeka sana labda tungekuwa na lugha moja tu mfano kama wachina, waarabu nk. Hivo tunakula matunda ya kile tulichopanda.
 
Shida kubwa ni ile kudhani mtu ukiongea kingereza kingi ndio utaonekana msomi, angalia hata bungeni na watawala wote kuanzia bibi yao hawawezi kuongea maneno 10 bila kuchomekea kakingereza ka uongo na kweli alafu wakati huo wanakua wanaongea na waswahili ambao wanaelewa kiswahili tuu, lakini cha ajabu mashuleni ukitoa hesabu kingereza ni somo lingine linalo ongoza kwa wanafunzi kufanya vibaya, lakini wakute mtaani sasa wanavyo jikuta wasomi na hicho kiswanglishi chao, kingereza hawajui kiswahili hawakipendi
 
Kuna mahali niliwahi kusikia kuwa ukiona unachanganya lugha mbili katika mawasiliano basi kuna uwezekano mkubwa kuwa hauna misamiati ya kutosha katika hizo lugha mbili kwa maneno mengine ni hauna uwezo wa kutosha kuzimudu lugha hizo.
hata kigugumizi kwenye interviewz, hususani za kiingereza ni kutokana na muhusika kukosa msamiati mahususi wa kukamilisha sentennsi yenye maana anayokusudia kuitoa.....

Hapo sasa unakuta..
You know you know kama zote vile...
Which which kibao kwenye sentence fupi tu ....
 
Back
Top Bottom