Kiswahili ni lugha yenye vikwazo sana

Kiswahili ni lugha yenye vikwazo sana

Najua wengi wenu hapa ni wazalendo hivyo itakua ngumu kwenu kukubali hili ntakalosema.

Kiswahili ni lugha limiting sana. Ndio, katika maisha yakawaida ya kila siku, haina shida. Leta maji, leta kikombe, nenda pale, nipe hiyo. Hapo hakuna shida, na ni vizuri nchi nzima inaongea kwa kiswahili.

ila ikija kwenye mambo ya ki-intellectual, hakuna kitu. Kila nnapojaribu kuandika mada ya maana ya kiakili kwa kutumia kiswahili, napata shida. Maneno hakuna. Tofautisha na lugha kama English ambayo ina maneno ya kuelezea chochote kile kwa kutumia maneno ambayo yanafahamika na kutumika katika maisha ya kawaida.

Huwezi ukafundisha sayansi, computer, au topic yoyote ya maana kwa kiswahili. Hata utafsiri kila kitu.

Naamini hii imechangia sana kwa Tanzania kua nyuma katika mambo ya kielimu, teknolojia, na sayansi. Angalia majirani zetu Kenya. English wanajua kwa ufasaha zaidi. Na kweli ukiangalia, wakenya wengi wapo nje katika vyuo vya maana, taasisisi za maana, profession za maana, na wanashinda tuzo mbali mbali za kielimu, teknolojia, na sayansi. Hata innovation pia wako mstari wa mbele. Ukienda wall street, utakuta wakenya.

Sasa sisi tumebaki hapa tunasema kiswahili ni uzalendo. Ni lugha nzuri kweli sikatai, ila intellectual value yake ni almost zero.

Hii post yenyewe imenitumia muda kuandika nikisaka maneno. Na mimi ni mtanzania asili, sasa sijui wakuhamia itakuaje.

Ukitaka ujue, angalia viongozi wetu, ma manager, na watu mbali mbali wanaoheshimika. Wakihutubia kwa kiswahili, wanazunguka mbuyu, wanasaka maneno ya kuelezea jambo ambalo kwa lugha nyingine, sentensi moja ingetoshea. Na mwisho wa siku, hua hawafanikiwi.

kwa wale walioelimika na wenye akili pana. Hebu jaribu kutafsiri topic ya sayansi, teknolojia, au philosophy kwa ajili ya ufundishaji, uone uzito wake.
We sema hujui kiswahili
 
Mzee kwa stahili hii bora kuendelea na kiingereza tu.Kwa nini tusitengeneze au kutohoa maneno kutoka English yakawa tu kiswahili mfano badala ya kusema Nywila kwa nini tusiseme tu PASIWADI....
Hayo maneno yanakuwa magumu bora kutumia English tu sasa
Wewe ni mkenya,na hujui nimejuaje kuwa wewe ni mkenya
 
Mtoa mada umeeleweka vizur sana, msingi wa lugha ni kurahisisha mawasiliano, wengi wetu hatujui maneno ya kiswahili kwa ufasaha ingawa tumezaliwa na waswahili na kukulia kwenye jamii ya kiswahili.

Kuna baadhi ya maneno ya kiswahili ukiyasikia utashangaa hata kama hilo neno lipo na unaweza dhani ni neno la kabila flani labda, ila ndio kiswahili fasaha hicho.

Hii yote ni kwasababu mashuleni kuanzia vidudu mpaka Advance walimu wanao fundisha lugha nao hawakijui kiswahili fasaha vile vile pamoja na jamii zetu mitaani.
 
ila wewe kitu unashindwa kuelewa ni kwamba, haya maneno hayafahamiki karibu na kila mtu
Serikali ikirasimisha hayo maneno yatafahamika ndani ya muda mfupi sana sababu yatakua kwenye matumizi
wewe ni wangapi tanzania hii utawaambia "kitengo kikuu cha uchakataji" au "kiwambo", alafu wakakuelewa? Hapo ndo failure ilipo. Maana point ya language ni kuwasiliana na watu wengi, sio mmoja au wawilli, inabidi kila mtu akuelewe.
Itaeleweka tu, ndio maana nimekwambia lugha ya kitaaamu sio ya wote ni wale wanaofanyia eneo husika, kuna watu wengi wanatumia computer kwenye ila hawajui hata hizo CPU au pointer ila wale waliosoome computer ndio wanajua hayo
Alafu angalia sasa, ikija kwenye fursa za nje, ambapo sayansi, teknolojia, na elimu ndo wanaongoza, kiswahili hakitumiki. Na ndo nkakupa mfano wa wakenya ambao wengi huenda nje na kuadapt kirahis
Mbona wachina wanasoma kwa lugha yao na wapo dunia nzima mpaka huku kwetu umeshaona wanakwama wapi?na mitambo wanatumia kama kawaida.
hata ukafahamu perfect swahili ukawa na neno la kila kitu. Ni wangapi watakuelewa hapa hapa Tanzania? je Huko nje ambapo mitambo halisi ndo ipo?
Mitambo ni kuijua kwa vitendo tu, simu hata itoke leo ukampelekea mtu wa kijijini atajua tu namna ya kutumia ndio maana nikakupa mfano wa wachina.
 
English ingewekwa tu kuwa lugha ya taifa sema tumesha chelewa sana.
Kwenye hizi fursa za kimataifa watanzania tuna dhalilika sana. Uwezo upo lakini lugha inakuwa kikwazo.
Mbaya zaidi ni kenya tu ndio tunaweza kujumuika nayo mataifa yote Africa yaliyobaki Hawajui kabisa kuongea kiswahili.
Yaan hii lugha kwa kias fulan pia inachangia umasikin bongo
 
Huu ugumu unasababishwa na serikali kushindwa kurasimisha kiswahili kama lugha ya kufundisha ila haimaanishi hakuna maneno hayo.

Kila kitu kina wataalamu wake, haiwezekani ukaamka tu unataka kufundisha sayansi kwa kiswahili bila wewe kujua lugha ya kufundisha sayansi au computer

Kumbuka lugha ya kawaida ya kuongea ni tofauti na lugha ya taaluma fulani na hii ni hata katika kiingereza chenyewe mfano ukisema 'superwoman' katika lugha ya kawaida ni mwanamke shupavu lakini kwenye medical field ni mwanamke mwenye extra x chromosome ambazo zinaleta changamoto kwenye uzazi wake.
Au ukisema link kwenye Internet mtu anajua atakutana na https nk lakini link kwenye mechanic ni kifaa fulani chini ya gari kwenye tairi huko kwahio usichanganye mambo.

Kama unataka kufundisha somo mahsusi kwa Kiswahili tafuta maarifa kwanza na ukiweza wasiliana na BAKITA au BAKIZA au tumia kamusi.

Kiswahili ni tajiri sana labda wewe tu huna istilahi za kutosha kwahio ulizia kwanza kwa mfano kwenye computer:
Computer-Tarakilishi
Keybord-baobonye au charazio
Password-Nywila
Browse-Rambaza
Softcopy-nakala tepe
Link-kiunganishi
Screen-kiwambo
Mouse-Kiteuzi/kipanya
CPU-Kitengo kikuu cha uchakataji(KIU)au Kichakati
Cursor-kishale elekezi

Kwenye simu:
Sms-Arafa

Missed call- simu fifi
Nk.





Maneno yapo, misamiati ipo istilahi zipo pia tafuta au uliza.

Subalaheri.
Hallo, Boss samahani Kwa kuchelewa, nimeona "simu fifi"
Oya unaweza kukosa kazi 🤣
 
Back
Top Bottom