Hivi Mkuu una uelewa wa namna gani? mbona hata maswali yako hayana mshiko? Unauliza lugha yenye mchango mkubwa katika maendeleo kati ya Kiswahili na Kiingereza bila ya kutaja mchango wa maendeleo gani na nchi gani, unatarajia ujibiwe vipi? Unataka useme maendeleo yaliyoko uchina, Ujerumani, Urusi, Italia, Ufaransa, na nchi kibao zisizozungumza hicho kiingereza unachokiabudu yaliletwa kwa kuzungumza Kiingereza? Ni viongozi wenye mawazo kama yako ndiyo walioididimiza lugha hii kuwa kama ilivyo, wameshindwa kuchukua hatua thabiti kuiimarisha. Inashangaza lugha inayozungumzwa na watu zaidi ya milioni 100 waliosambaa katika mataifa zaidi ya kumi wewe unasema si lugha ya kimataifa! Nasisitiza tena ukikiona Kiingereza ni kipana, kirefu au kinapendeza ujue nyuma ya pazia wapo watu wanaokifanya kionekane hivyo.Naomba nikuulize maswali yafuatayo:
Je, ni lugha gani kati ya kiingereza na kiswahili, inamchango mkubwa katika maendeleo ? na ni kwa nini?
ndugu yangu!haya unayozungumza umefanyia utafiti kweli?hivi lugha ndio kikwazo cha sisi kuto tambulika au kuto kuwa na maendeleo?naomba nitofautiane na wewe kwa hilo.mimi na amini fikra sahihi huja kwa lugha sahihi inayoeleweka kwa jamii husika.nilisha wahi fika china,kwakweli wale jamaa ni kichina kwa kwenda mbele unaweza shindwa nunua kitu dukani au kwenda mahali fulani kwa kuwa mmeshindwa kuelewena kwa lugha lakini hebu angalia walivyopiga hatua kimaendeleo kwa kila nyanja!hivyo basi usitukuze lugha za kigeni na kuacha za kwako kisa eti hatutaendelea,jaribu kuja na mbinu mbadala ya sisi wapi tumekosea ila hili la lugha hapana!
Mkuu kwanza hongera kwa bahati (au jitihada) ya kipekee kuishi nje ya Tanzania. Pili, sidhani kama kiingereza kinapuuzwa hapa Tanzania na ndio maana kwanza kinafundishwa kama somo ngazi za awali na ndio lugha rasmi ya kufundishia ngazi ya sekondari na kuendelea.
Pili kulegalega kwa kiingereza isichukuliwe ni kutokana na kupuuzwa kwake kwani hata hicho kiswahili chenyewe wala hakina au hakifundishwi kwa ubora unaotakiwa.
So, generally, tatizo halipo kwenye kiingereza bali tuna tatizo zaidi ya lugha. Ni almost kila kitu hatukiwezi karibu kila nyanja ya maisha. Kwa mfano, hivi hata kuweka mazingira yetu safi ili tusisumbuliwe na kipindupindu kila wakati tunahitaji kiingereza? Hivi kondakta wa daladala anahitaji kujua kiingereza ili asimnyanyase mwanafunzi? Hivi tunahitaji kujua kiingereza ili tusijisaidie ovyo mitaani? Hivi tunahitaji kujua kiingereza ili tusikwepe kodi au kuiba mali ya umma, ufisadi, n.k?
Tatizo sio lugha bali mfumo. Na mfumo, nionavyo mimi, unahusisha tabia zetu, desturi zetu, siasa zetu, mila zetu (imani za kishirikina, n.k.), mahusiano yetu, na hata dini zetu. Kama wachina waliweza kwa lugha yao na "sasa hivi" ndio wanajifunza lugha za kigeni kwa nini sisi tushindwe? Ni maoni yangu.
it might not be knowledge but it forms the basis for knowledge!!Mkuu language is not knowledge.
usiwe mwepesi kuropoka!!!, soma mada, elewa, tafakari, jibu.Nimepita haraka haraka kwenye tovuti ya Benki ya Dunia, miongoni mwa mataifa maskini 20 duniani zimo Haiti, Niger, Sierra Leone, Zimbabwe, Malawi, Togo, Liberia na Uganda, nchi ambazo ni wazungumzaji wa Kiingereza tokea mwanzo.
Mtoa mada nahisi umevurugwa...
anza kwa kuchapisha kitabu cha chemistry kwa kiswahili. no! kwanza tafuta hilo somo kwa kiswahili linaitwaje, na usiseme 'kemia'. kemia sio kiswahiliTena kama tungejitahidi tukatumia kiswahili hata mpaka chuo kikuu elimu yetu ingekuwa ya uelewa zaidi kuliko sasa hivi ambapo tunatumia kiingereza kucram vitu tusivyovielewa kwa kiingereza
Nchi haiwezi kuendelea na kuwa na amani Kwa kutumia lugha za kigeni.Huo ni ujinga ambao ni mwafrika tu anayeutukuza.
anza kwa kuchapisha kitabu cha chemistry kwa kiswahili. no! kwanza tafuta hilo somo kwa kiswahili linaitwaje, na usiseme 'kemia'. kemia sio kiswahili
Hata chemisty sio Kiingereza, ni Kilatini.
ndugu yangu!haya unayozungumza umefanyia utafiti kweli?hivi lugha ndio kikwazo cha sisi kuto tambulika au kuto kuwa na maendeleo?naomba nitofautiane na wewe kwa hilo.mimi na amini fikra sahihi huja kwa lugha sahihi inayoeleweka kwa jamii husika.nilisha wahi fika china,kwakweli wale jamaa ni kichina kwa kwenda mbele unaweza shindwa nunua kitu dukani au kwenda mahali fulani kwa kuwa mmeshindwa kuelewena kwa lugha lakini hebu angalia walivyopiga hatua kimaendeleo kwa kila nyanja!hivyo basi usitukuze lugha za kigeni na kuacha za kwako kisa eti hatutaendelea,jaribu kuja na mbinu mbadala ya sisi wapi tumekosea ila hili la lugha hapana!
duh! Tipical!!
ok. lengo sio kujua chemistry ni kilatini/ kiingereza. tusiongee tu ili tuonekane kama si tuwazalendo sana au ndo tunapenda mila zetu kuzidi watu wote...... kutafsiri vitabu vinavyotumika secondary na vyuoni itachukua miaka mingapi na kutugharimu sisi walipa kodi shi'ngi ngapi? je tuko tayari kugharamika na kusubiri au ni maneno tu? maana yangu ilikua kwamba its imposible kufundisha hasa masomo ya sayansi kwa lugha ya kiswahili. na information ndio power ya maendeleo. so, Mphamvu nilitaka nikuonyeshe kwamba lugha yetu bado changa na sio kujua neno chemistry ni lugha gani, labda kwa kukufahamisha tu ni kwamba chemistry is greek origin not latin!