falamangaa,
Siyo kweli mkuu kwamba watu wote wametoka Africa, yawezekana Maisha ya binadamu yameanzia Africa lakini sio kweli kwamba Watu wote duniani asili yao ni Africa. Siyo kweli kwa sababu huwezi kusema watu wa asili ya misitu ya Anazoni (in the interior dense forest of Amazon who have never seen the outside world) kwamba walitoka Africa.
Huwezi kusema watu wanaoishi juu kabisa ya milima ya Himalaya ambao maisha yao yote ni huko huko juu na wala hawajaona outside world uniambie eti hao walitokea Africa huwezi kunishawishi kwamba Wenyeji wa ndani kabisa wa Mongolia wanaoishi huku na tamaduni zao za asili bila kuchangamana na tamaduni zingine useme kwamba walitoka Africa.
Huwezi kunishawishi kwamba Sinhalese walioko katika visiwa vya india (Isolated islands in indian ocean), watu wenye lugha za kipekee na tamaduni za kipekee, watu ambao have never seen outside world uniambie kwamba karne kadha zilizopita walitoka Africa wakasafiri kwenda huko!!!, kwasababu ipi na kwa usafiri gani??.
Katika zama ambapo Mungu alianza uumbaji wa Wanyama na baadaye Watu -billion/millions of years ago- , uso wa dunia ulizungukwa na "Biotic soup" ni zama hizo za Biotic soup ndipo dunia ilipo chipusha viumbe hai (sprouting living organism), ni chemistry iliyokuwa Catalysed na direct sun light (cosmic rays), ndiyo maana ninakuambia siyo lazima kwamba Papua new guineans na Aborigines kwamba walitoka Africa.
Hao walichipuka hapo hapo jinsi sisi Waafrika tulivyochipuka hapa hapa Afrika, yaani Mazingira ya sisi waafrika kuchipuka hapa Afrika ni mazingira ya aina hiyo hiyo yaliyokuwepo sehemu mbalimbali za dunia na ndipo wakachipuka watu wa aina mbalimbali wenye rangi mbalimbali, lugha na tamaduni na mila mbalimbali, hii ilitokana na utofauti wa Biotic soup za mahali mbalimbali.
Chukua mfano huu, huwezi kusema kwamba Ng'ombe kutoka Afrika ndiye aliyeenda kuzaa ng'ombe wote wa duniani, kadhalika huwezi sema jambo hilo kwa kuku, Bata, Mbuzi nk kutoka Afrika ndio waliozaa mbuzi ,Bata, kuku nk wa dunia nzima, ni kwa mfano huo pia huwezi kusema kwsmba Aborigines wa Australia wenye historia ya maelfu ya Miaka huko kwamba walitoka Afrika, Aborigines feature zao ni tofauti sana na Black Africans, wao rangi ya ngozi yao, nywele zao, nyuso zao na stature zao hazifanani kabisa na Sisi black African, sasa huwezi kushikilia theory za wanasayansi kwamba hawa jamaa walitoka Afrika.
Kumbuka theory ni kitu cha kujadiliwa ili kupata ukweli, theory zinaweza kuwa Uongo.