Kiswahili hiki ni sahihi?

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,244
4,258
Hamjambo wanaJF wote? Leo naomba wale wadau/wakereketwa wa lugha ya kiswahili mnisaidie hili. Kuna tangazo moja la biashara linanipa shida sana. Tangazo hilo linatolewa kwa kiingereza, halafu tafsiri yake kwa kiswahili inafuata.Kwa kiingereza, tangazo lasema hivi: 'How to loosen up when you are bored. (maneno niliyoweka bold ndio chanzo cha shida yangu.) Tafsiri yao kwa kiswahili yasema hivi: 'Jinsi ya kuburudika ukiboreka' Katika tafsir ya kiswahili utaona wazi kwamba to be bored imetafsiriwa kuboreka. Sasa nawauliza waungwana wenye ujuzi wa kiswahili, ni lini katika kiswahili tumekuwa na neno ku-boreka lenye maana ya to be bored? Nijuavyo mimi kuboreka ni neno la kiswahili lenye maana ya: kuwa bora zaidi, kuimarika nk. Naomba mlizungumzie hili nipate uhakika. Asanteni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom