Mwana wa Mungu
JF-Expert Member
- Aug 14, 2008
- 1,003
- 83
wewe unaesema kiswahili cha zanzibar au mombasa ndo kizuri, hahaha, unatisha mzee, mbona kina mlegezo kama wanakula mlenda...duh. mimi nafikiri kiswahili kizuri ni kiswahili cha Dar es salaam. ninyi mnasemaje?
Hapa nionacho ni swala la watu kutokuwa makini na matamshi yao.Kiswahili cha Dar Arusha wanasema Alusha
Kariakoo wanasema Kaliakoo
Kimara wanasema Kimala
Afadhali cha wachaga na wameru japokua wana strong accent lakini wanatofautisha r na l kuliko kiswahili cha Dar.
Mwana wa mungu hawasemi mlenda bali mrenda.
Kwangu mimi kiswahili kizuri ni mtu anayeweza kuzitamka alfabet zote za kiswahili, ukisikiliza kiswahili cha dar herufi R hawaitumii kabisa.
Kiswahili cha Dar Arusha wanasema Alusha
Kariakoo wanasema Kaliakoo
Kimara wanasema Kimala
Afadhali cha wachaga na wameru japokua wana strong accent lakini wanatofautisha r na l kuliko kiswahili cha Dar.
Mwana wa mungu hawasemi mlenda bali mrenda.
Kwangu mimi kiswahili kizuri ni mtu anayeweza kuzitamka alfabet zote za kiswahili, ukisikiliza kiswahili cha dar herufi R hawaitumii kabisa.
kiswahili kizuri ni cha majita-Musoma.
Inashangaza,kuona tuna jadiri kitu ambacho tunakijua (kadiri nionavyo mimi),Kumbukumbu zangu kama ziko sawa,nilipo ingia kidato cha kwanza tu (ingawa miaka mingi iliyopita) Mwl. wangu wa kiswahili alinifundisha asili ya Lugha/Kiswahili.
Kwenye asili ndio hasa utajua kwanini kiswahili au lugha nyingine inatofautia kutokana na maeneo(kanda),nafasi ya kiuchumi(matabaka) na kadhalika.
Siwezi kujua watu kwanini watu hapa barazani,hasa watu wazima tunao waheshimu wenye michango mizuri kwenye mambo makubwa makubwa yahusio Uchumi ,Jamii ,kimataifa na mengineyo tunashindwa kukumbuka jambo hili dogo tu linaluhusu lugha tena Lugha yetu adhimu.?kiasi hata cha kuchanganyikiwa na kujichanganya.
Napata shaka kwamba haya ndio hasa matunda ya kuto sikiliza madarasani,Kununua mitihani na Kukariri ili kujibu tu maswari ya Mitihani,hii ndio mfumo mbaya wa elimu yetu unapotufikisha.
Sipati shaka kufikiri kwamba iko siku tutakuja kufundishwa hii lugha na wazungu kwani hatuijui.

Hakuna kitu kama "Kiswahili cha Dar" kuna cha Zanzibar, Mrima, Ngazija (Singadzija, Shikomor, Shindzuani, Shimaore), Kimgao, Kipemba, Kimvita, Kiamu, Chimwinii (Barawa)
Hao watu wa Dar wanaoweka "l" kwenye "r" na wengine "r" kwenye "l" ni influence za makabila.
Mimi nimekulia Dar na siwezi kuweka "l" kwenye "r" wala "r" kwenye "l".
Mara nyingi nimekutawa nakutana na maneno yanayonitia kichefuchefu hasa kwenye magazeti yetu mengi tena kwa bahati mbaya zaidi hata yale magazeti yanayoaminika hapa nchini,
utasoma habari nzuri ila huwezi kuimaliza kwa sababu tu lugha iliyotumika inasumbua.
mfano wa maneno hayo kwa uchache sana ni haya:-
alafu - akimaanisha Halafu
taharifa - taarifa
hajali - ajali
udhahifu -udhaifu
bahadae - baadae/baadaye
hadidhi - hadithi
ayupo - hayupo
kuna mengi yanamakosa ila leo nimeanza na haya machache
nawaalika/nawaalikeni badala ya nakualika/nakualikeni
kiswahili kinaraha sana kukitalii ukiwa mweledi na mahiri wa kupitia tahariri.
Kiswahili kilizaliwa Zanzibar, kikakulia Mrima-, kikazeekea Kenya na kujikongojea Uganda.
Kiswahili kina lahaja tofauti, lakini Wataalamu wengi wanakitambua Kiswahili cha Unguja kuwa ndiye chenyewe.