Kiswahili halisi ni kipi?je, cha Tz, cha Kenya, Congo au Zanzibar? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiswahili halisi ni kipi?je, cha Tz, cha Kenya, Congo au Zanzibar?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Mwana wa Mungu, Oct 7, 2008.

 1. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2008
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  jamanieee, hivi tuseme kuwa, kiswahili halisi na cha kufuatwa kama ndo mfano wa kiswahili halisi na kizuri ni cha wapi? mfano, nikianza kama nchi, ukienda kenya, kiswahili chao kimegonjwa, ukienda congo ndo kimekukufa, ukienda zenji ni cha mlegezo debwedebwe.

  ukija hapa bara, wachaga wanaongea lafudhi ya kikwao, wahaya ndo kabisaa, wahehe ndo kama kwenye maigizo ya luninga, wazaramo ndo watoto wa mjini hata kama ni mzee,watu wa tanga wanaongea kama hawataki,watu wa mtwara wakiongea watakutemea mate kwa cheche..eg.che mkapa, wamasai kwa kina Lowasa ndo kimelala na mama yeyo kabisa, sasa, kipi kiswahili halisi? na ninani wa kumcheka mwenzake?mfano wazungumza kiswahili wote africa tukikutana pamoja, au tz tukikutana pamoja kima mmoja akawa anaongea, icho kichekesho nani ataibuka kumcheka mwenzie?,manake ivyo vicheko havitaisha, kila mtu akigeukia huku anacheka, yule anayemcheka mwenzie naye anachekwa nk. duh!
   
 2. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2008
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Binafsi nafikiri kuna haja ya kuwekwa misingi ya kiswahili na si kila mtu kufanya anavyotaka au kufikiri ni sawa.Ingawa inaonekana ni vigumu kiswahili kutokuathiliwa na lafudhi,lakini inaweza kusaidia kupunguza tofauti ya kiswahili kulingana na maeneo.Kwa sababu utakuta hata matumizi ya maneno yana tofautiana kulingana na maeneo kitu ambacho sidhani kama ni kizuri.Lakini ikiwekwa misingi,tofauti zitakuwepo lakini si kubwa kwa kiasi hiki kinachoonekana.
   
 3. D

  Darwin JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kitu cha msingi nikuelewana kwenye hio lugha, hayo mengine nimajikombo tu. hta kiingereza kinatofautiana pia, mreno wa brazil na mreno wa portugal wanatofautiana pia baadhi ya maneno.
  Mfaransa wa Ufaransa anatofautiana pia na mzungumzaji kifaransa wa Canada.

  Na hizi tofauti ndio zinazoleta utamu.
   
 4. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2008
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mhhh! hivi ni kweli?
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Naomba nichangie kidogo kama ifuatavyo:
  Mwisho wa siku , lugha yeyote inapaswa irahisishe mawasiliano. Watu wanapoelewana basi mengine ni ziada hata kama lafudhi zinachekesha au kustaajabisha. Kiswahili kama lugha nyingine na kama walivyosema waliotangulia, hutofautiana kutegemea kinaongelewa wapi na kimepata athari au influence ya sehemu husika aidha kilahaja au hata kwenye istilahi na misamiati.
  Pamoja na kutofautiana huko.. kwenye kiswahili hua naona mara nyingi hasa matangazo ya kazi za kimataifa wanatofautisha kwa kusema kuwa lugha inayotakiwa ni kiswahili cha Congo.Hivyo basi usifikirie kuwa kwa vile unajua kiswahili basi una qualify kwenda kufanya kazi DRC na kiswahili chako cha Tanzania, Kenya au kwingineko!
  Vile vile kuna ile hulka ya wenzetu Ulaya hata Marekani kupenda kuona kuwa kiswahili cha pwani - mathalani Zanzibar au Mombasa ndio kiswahili kizuri. Hili tunaweza kulijadili zaidi.
   
 6. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2008
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  huwa wanasema hivyo kwa kazi zile ambazo mtu anatakiwa kufanya kazi UN kule congo, mtu anayeongea kiswahili cha kitz, watu wa congo hawawezi kumuelewa vizuri, kwasababu kiswahili yao ni mbofumbofu. hivyo wanahitaju mtu atakayeongea kiswahili kibovu kama cha kwao. kwahabari ya congo ni hivi, kazi nyingi huwa ni za kule kwenye nchi za kifaransa, so wanahitaji mtu atakaeongea kifaransa na kuongea kiswahili kama chao, ila so kwamba kiswahili cha congo ndo kizuri. na tatizo lingine ni kwamba, congo ndo kuna matatizo sana ndo maana unaona kazi nyingi hasa kule kwenye web ya UN ni za congo.

  wewe unaesema kiswahili cha zanzibar au mombasa ndo kizuri, hahaha, unatisha mzee, mbona kina mlegezo kama wanakula mlenda...duh. mimi nafikiri kiswahili kizuri ni kiswahili cha Dar es salaam. ninyi mnasemaje?
   
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ata English ni ivyo ivyo tuu,mnaigeria akiongea apa ni tofauti na mkenya au mganda.
  Hii inatokana na background za watu via vernacular language zao.
  Ila bongo tuko juu kwa kiswahili na sio kenya wala DRC na kwingineko ata wenyewe wanalijua ilo.
  Ila wazaramo nao ambao ndo pioneers wa lugha hii ninavyozani wanatuaribia sometimes ati (ati mvua uyo anakuja!!!!!!!!!!!!!)
   
 8. D

  Darwin JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kiswahili cha Dar Arusha wanasema Alusha
  Kariakoo wanasema Kaliakoo
  Kimara wanasema Kimala

  Afadhali cha wachaga na wameru japokua wana strong accent lakini wanatofautisha r na l kuliko kiswahili cha Dar.

  Mwana wa mungu hawasemi mlenda bali mrenda.

  Kwangu mimi kiswahili kizuri ni mtu anayeweza kuzitamka alfabet zote za kiswahili, ukisikiliza kiswahili cha dar herufi R hawaitumii kabisa.
   
 9. S

  Sunshine OLD Member

  #9
  Oct 8, 2008
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapa nionacho ni swala la watu kutokuwa makini na matamshi yao.
  Hii ndiyo sababu ya instead of 'r' they put 'l' inakera si uongo.
   
 10. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kiswahili kilizaliwa Zanzibar, kikakulia Mrima-, kikazeekea Kenya na kujikongojea Uganda.

  Kiswahili kina lahaja tofauti, lakini Wataalamu wengi wanakitambua Kiswahili cha Unguja kuwa ndiye chenyewe.
   
 11. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #11
  Oct 8, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hakuna kitu kama "Kiswahili cha Dar" kuna cha Zanzibar, Mrima, Ngazija (Singadzija, Shikomor, Shindzuani, Shimaore), Kimgao, Kipemba, Kimvita, Kiamu, Chimwinii (Barawa)


  Hao watu wa Dar wanaoweka "l" kwenye "r" na wengine "r" kwenye "l" ni influence za makabila.

  Mimi nimekulia Dar na siwezi kuweka "l" kwenye "r" wala "r" kwenye "l".
   
 12. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  kiswahili kizuri ni cha majita-Musoma.
   
 13. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #13
  Oct 9, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Mmmmmh kuna mwingine atatuambia kiswahili kizuri cha Kanyigo - Kagera.
   
 14. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #14
  Oct 9, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Inashangaza,kuona tuna jadiri kitu ambacho tunakijua (kadiri nionavyo mimi),Kumbukumbu zangu kama ziko sawa,nilipo ingia kidato cha kwanza tu (ingawa miaka mingi iliyopita) Mwl. wangu wa kiswahili alinifundisha asili ya Lugha/Kiswahili.
  Kwenye asili ndio hasa utajua kwanini kiswahili au lugha nyingine inatofautia kutokana na maeneo(kanda),nafasi ya kiuchumi(matabaka) na kadhalika.
  Siwezi kujua watu kwanini watu hapa barazani,hasa watu wazima tunao waheshimu wenye michango mizuri kwenye mambo makubwa makubwa yahusio Uchumi ,Jamii ,kimataifa na mengineyo tunashindwa kukumbuka jambo hili dogo tu linaluhusu lugha tena Lugha yetu adhimu.?kiasi hata cha kuchanganyikiwa na kujichanganya.

  Napata shaka kwamba haya ndio hasa matunda ya kuto sikiliza madarasani,Kununua mitihani na Kukariri ili kujibu tu maswari ya Mitihani,hii ndio mfumo mbaya wa elimu yetu unapotufikisha.
  Sipati shaka kufikiri kwamba iko siku tutakuja kufundishwa hii lugha na wazungu kwani hatuijui.
   
 15. D

  Darwin JF-Expert Member

  #15
  Oct 9, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hapa umeshateleza tayari.

  Watanga mjini, Waunguja, waarusha na wachaga sio rahisi kuteleza kirahisi.
   
 16. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #16
  Oct 9, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0


  Mkuu
  Mwalimu wako alikufundisha vibaya kutamka Jadiri badala ya JADILI na maswari badala ya MASWALI!
   
 17. D

  Darwin JF-Expert Member

  #17
  Oct 9, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Siwezi kuongea sana kuhusu kiswahili cha Dar, Labda watu wa Dar ni ile typical accent yao lakini kwenye lafudhi ngoja nisiongee sana. Bora nisikie kiswahili cha Nairobi japokua wanasema "kudja hapa" lakini wanazijua alfabet zote kuzitamka.

  Labda kiswahili cha dar kitabadilika kidogo kutokana na watangazaji wa redio na luninga kuzungumza vizuri, lakini sijui kama itasaidia sana kwani mtoto anajifunzia lugha nyumbani na mitaani.
   
 18. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #18
  Oct 9, 2008
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 922
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 60
  Mara nyingi nimekutawa nakutana na maneno yanayonitia kichefuchefu hasa kwenye magazeti yetu mengi tena kwa bahati mbaya zaidi hata yale magazeti yanayoaminika hapa nchini,
  utasoma habari nzuri ila huwezi kuimaliza kwa sababu tu lugha iliyotumika inasumbua.
  mfano wa maneno hayo kwa uchache sana ni haya:-
  alafu - akimaanisha Halafu
  taharifa - taarifa
  hajali - ajali
  udhahifu -udhaifu
  bahadae - baadae/baadaye
  hadidhi - hadithi
  ayupo - hayupo
  kuna mengi yanamakosa ila leo nimeanza na haya machache
  nawaalika/nawaalikeni badala ya nakualika/nakualikeni
  kiswahili kinaraha sana kukitalii ukiwa mweledi na mahiri wa kupitia tahariri.
   
 19. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #19
  Oct 9, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Bora kusoma utaweza kudhani ni typo error... inapokuwa ni kusikiliza redio au TV hapo ndio inachefua zaidi kuona au kusikia Mtanzania akisoma kiswahili kisichoeleweka.Hivi hawa watu wanafanyiwa usahili kwa maana ya usahili wa kutamka?
   
 20. M

  Mwanaluguma Member

  #20
  Oct 9, 2008
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ni kweli nakuunga mkono moja kwa moja,kiswahili rasmi ni cha unguja na hiyo ni kwa mujibu wa historia kama ilivyoandikwa kwenye vitabu mbalimbali juu ya lugha hiyo.
   
Loading...