Kiswahili halisi ni kipi?je, cha Tz, cha Kenya, Congo au Zanzibar?

Wengine waletao kichefuchefu ni hawa wasemao
Sintakwenda pahala pa Sitokwenda
Sintajiuzulu - Sitajiuzulu
Kimvuli - Kivuli
sioni sababu ya mtu kutojitahidi kukizungumza kiswahili vizuri na hasa waandishi wa habari na makala mbalimbali.
 
Kwa mujibu wa tafiti tofauti tofauti za chimbuko la kiswahili, kile cha tanga na mombasa ndio hasa chenyewe.
 
Kiswahili halisi ni kile kinachozungumzwa na Watanzania nikimaanisha kinazunguzwa Tanzania bara na Zanzibar.Nakubali kuna utofauti wa matamshi ya maneno mbalimbali ya kiswahili kwa wazungumzaji ndani ya Tanzania.Utofauti huu wa matamshi unatokana na lugha za asili za makabila mbalimbali ya Kitanzania.Wakenya,Wakongo na wengine wanajifunza Kiswahili kupitia kwa Watanzania.
 
kiswahili kinaangaliwa kihistoria ktk ukuaji wa kiswahili hvyo ktk mtazamo wangu kiswahili ni kile kile tu ila tofauti ni nani katamuka vipi?lakini kama ni ujumbe utakuwa uleule mana kwa mzungu aliyesoma kiswahili tanzania atajaribu kuongea kama watz na kama amejifunzia kenya ataongea kama wakenya nk
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom