Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo kasi (UDART) Robert Kisena na wenzake watatu wamesomewa mashtaka 33 katika kesi mbili tofauti kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikiwemo Utakatishaji wa fedha na kuongoza genge la uhalifu.
Kwenye kesi namba 21 ya mwaka 2022 inawahusu Kisena na wenzake wawili ambapo ni Charles Newe na Tumaini Kulwa wanadaiwa kujipatia kwa njia ya udanganyifu kaisi cha cha Shilingi 4.5 Bilioni huku wakituhumiwa kutakatisha na kusababisha hasara serikali kiasi hicho hicho.
Katika kesi namba 20 ya mwaka 2022 Kisena na washtakiwa wanne akiwemo Newe, Kulwa na Jonhn Samangu wanadaiwa kutakatisha kiasi cha Shilingi Milioni 750 ambazo zinadaiwa kuwa ni zao la kughushi na kulaghai.
Washtakiwa hawakuwa na haki ya kujibu chochote kwa Mahakama hiyo kwani haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo kisheria.
Watuhumiwa wamerejeshwa mahabusu ya magereza mpaka tarehe 23 Mei 2022 shauri hilo litakapotajwa.
Wote Wamekosa dhamana.
=====
UPDATES;
======
Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Usafirishaji wa Mabasi yaendayo haraka, maarufu mwendokasi (Udart), Robert Kisena na wenzake watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 33 yakiwemo ya kutakatisha fedha, kuongoza genge la uhalifu na kuisababishia hasara Serikali ya Sh 5.2 bilioni.
Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo leo Jumatatu Mei 9, 2022 na kusomewa kesi mbili tofauti za uhujumu uchumi mbele ya mahakimu wawili tofauti ambao ni Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Isaya.
Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao na jopo la mawakili watano wandaamizi wa Serikali wakiongozwa na Pius Hilla akisaidiana na Jackline Nyatori, Ester Martin, Iman Mitumemingi na Upendo Temu.
Mbali na Kisena, washtakiwa wengine ni Charles Newe (48) Mkurugenzi wa Udart, mfanyabiashara John Samangu (66) na Mtunza fedha Tumaini Kulwa (44).
Septemba 13, 2019 Mkurugenzi wa Mashtaka nchini ( DPP) aliwafutia mashtaka manne ya utakatishaji fedha washtakiwa hao na hivyo kubaki mashtaka 15 kati 19.
Kati ya mashtaka hayo 15 yaliyokuwa yanawakabili washtakiwa hao, yapo mashtaka manne ya kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo; manne ya wizi; moja kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na moja ni kusababisha hasara UDART.
Mengine ni kuongoza genge la uhalifu, kujenga kituo cha mafuta ya petroli bila kibali kutoka Ewura na kuiba.
Chanzo: Mwananchi