Kisima cha kutunzia maji ya mvua

Futi20 mil9 we jamaa utapigwa danya makes u hYa mambo madogo tumieni mafundi wa hapo kijijini n wewe mweneyewe tumia common skills comon skills matofali ,safruji ,nondo, mchanga kokoto lZima ujue bei na kiwango idadi
Wapi kaandika futi 20 mil 9?
 
Mkitengeneza barabara dsm na dodoma
Ndo mnasema nchi imekua kiuchimi
Ndio.

TUNATEKELEZA
JamiiForums-879927817_641x534.jpg
 
Maji ya mvua yana vumbi sana. Aidha, huwa yananuka sana yakikaa muda mrefu. Hivyo, ushauri wangu ni kuchimba kisima.
Hayawezi kuwa na vumbi,ni Kama tumeyatumia mara nyingi,isitoshe tutaweka dawa. Japo sawa hayawezi kuwa sawa na ya kisima kwa ubora. Tuna compare na gharama pia. Asante kwa maoni pia sister.
 
Hakuna tatizo, utapunguza gharama kubwa sana. 20' deep, 15' diameter gharama inaweza kufika 4m au zaidi kutegemeana na eneo husika.

Muhimu tu utumie tofali imara, usiwe bahili wa cement, ukiweza weka wire mesh ili kuimarisha kuta, chini weka ile nailoni nyeusi ili kuzuia maji kupotea, jenga msalaba ili kuimarisha kuta na hakikisha unalifunika ili mwanga wa jua usipenye ndani. Ukifanya hivi hata hizo water guard utaweka kwa utashi tu ilà haitakuwa lazima.

Utaokoa gharama nyingi kununua maji.
Daah...! Umeua kamanda,asante sana. Hilo la cement yupo mtaalam atasimamia. Isitoshe kuhusu tofali kaniambia tutatumia hizi za kuchoma ila atazipanga kama unavyojengwa msingi ili kuufanya huo ukuta wake usipungue futi moja upana wake,hiyo ni kuanzia chini mpaka juu. Zaidi umeongezea kitu ambacho yeye hakusema kuhusu hiyo karatasi la nailoni nyeusi kwa chini. Asante sana mkuu
 
Lita 60,000 ni sawa na ndoo za maji 3,000 (ndoo 1 ni lt 20)
3,000÷12=250 ie ndoo 250 kwa mwezi au ndoo 9 kwa siku. Fanya tathmini hapo kwako unatumia ndoo ngapi kwa siku, then utakua na jibu.
Duuh...! Asante sana mkuu,kunileta huku ambako sikufikiria kabisa kuhusu calculation ya namna ya matumizi pia. Lakini nafikiri hapo mkuu tufanye 3000÷6 ksbb ile miezi ya kuanzia wa 11 mpaka wa 4,5 hapo ni sawa na kwamba tutakuwa hatutumii maji yetu ya kisima,japo tutakuwa tunatumia,lakini yanarudishiwa zaidi kwa mvua zitakazokuwa zinaendelea kwa kipindi cha miezi hiyo. Kwa hiyo maji ya akiba zaidi tutaanza hesabu nayo mwezi 5,6,7,8,9,10 ambayo kutakuwa hakuna mvua
 
Miaka 10? Ni bora uyafungulie ukinge mengine.
Sio kwamba miaka 10 anatumia hayo hayo yaliyomo kwenye kisima. Anamaanisha ametumia maji ya mvua kwa miaka 10 bila athari yoyote. Hata hivyo kukujibia hilo,kila mwanzo wa mvua,mfano kila mwisho wa mwezi 10 kila mwaka nafikiri kisima kinasafishwa
 
Futi20 mil9 we jamaa utapigwa danya makes u hYa mambo madogo tumieni mafundi wa hapo kijijini n wewe mweneyewe tumia common skills comon skills matofali ,safruji ,nondo, mchanga kokoto lZima ujue bei na kiwango idadi
Sawa mkuu,nalo neno. Kuna Eli79 amesema ni kama milioni 4 hivi. Au wewe unaona gharama inaweza kuwa sawa na milioni 9 mkuu?
 
Back
Top Bottom