Kisichoeleweka kwa wadau kuhusu mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood

Jul 11, 2020
64
139
Jana Magufuli amemponda sana Mbunge Aziz Abood kwa kuua viwanda lakini kuna kauli haijaeleweka na wadau wa Morogoro wamekuwa kimya kuhusu baadhi ya kauli. Ninalazimika kuandika kuhusu kauli hizo na sababu ya CCM kumsimamisha kama mbunge huku wakijua ameua viwanda

Abood amesimamishwa kwa mara nyingine kama mbunge kwa kuwa tangu zamani amekuwa akitoa magari yake bure kusaidia shughuli za msiba za raia yeyote ndani ya manispaa, Hivyo wadau wanasema Abood anazika watu kwa maana hiyo. Hili jambo pia amesifiwa na Magufuli wakati anazindua Soko la Kingaru Morogoro Mjini.

Morogoro imechukuliwa na Mbunge Abood baada ya Dr. Mzeru kushindwa kufanya kitu, tangu wakati huo viwanda tayari vilikuwa vimeshakufa. Lakini kifupi ni kuwa raia wanamkubali mtu wao kwa sababu hiyo ya kuwazika hivyo hata kwa CCM inakuwa ngumu kumleta mwingine, wakati watu wanamjua Abood

Halafu kama mnavyojua jinsi raia walivyo rahisi kudanganyika, Kuzikwa kuwa wazi zaidi kwao kuliko viwanda ambavyo vingeweza kuwa saidia. Mwaka 2018 Abood aliita watu kuandikisha kama anataka kufufua kiwanda cha MOPROCO raia wakaenda kutuma maomba na kuacha CV ila hadi leo kimya. Anyway sio ishu

So, kuna watu walielewa kuwa kuwazika ni kuwa kuna wafanyakazi walikuwa wanakufa viwandani halafu wanazikwa kwa siri, hapana! Angefanya mambo hayo maana yake ingekuwa ni suala la ajabu serikali ijue halafu ikae kimya, point ni kuwa anawazika raia wote ambao wengine angeweza kuwaajiri kwa kufufua viwanda.

Pia, kwa hili suala limemshushia sana Abood na viongozi wa CCM, Manispaa ya Morogoro so inawezekana akakaa pembeni 2025 ili mwingine achukue, kwa kuwa sidhani kama ataweza kufufua viwanda viwili ndani ya miaka mitano iliyobaki wakati yeye amejiwekeza zaidi kwenye Redio na Usafirishaji.

Kwa vijana wanaotaka kuingia kujaribu bahati yao Morogoro, tutafutane kupeana mikakati kuanzia sasa ili kufikia lengo la kuchukua jimbo na kufanya maajabu, maana Morogoro ina shida nyingi sana. Mikakati inabidi ianze sasa.

Mathematical Equation
 
Mkoa wa Morogoro kuna watu wamuufanya shamba la bibi. Rais akiwa Kilosa pia alichukizwa kuhusu mashamba. Morogoro inahitajika uongozi imara kuliko mikoa mwingine kuanzia mkuu wa mkoa,wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa Halmashauri, wakuu wa idara zote ndani ya Halmashauri.

Pia mkoa wa Morogoro unaonyesha hauna vipaumbele vya mkoa wako, kama vipio ni nadharia tu. Morogoro kuna kila kitu ila wananchi wake ni maskini sababu hazijulikani.
 
Ukiona watu wanapata shida, waangalie pita zako tu, wanayataka wenyewe, sasa hao wanashangilia na kumkubali mtu anayetoa magari kwenda kuzika ndugu zao ila amechukua viwanda amekopa pesa na kununua mabasi. ila ameacha viwanda ambavyo vingewapa hao wananchi pesa.
 
Nilichokiona mimi kwa nchi ya Morogoro, wale watu wanapendwa sana kuzikwa hivyo Azizi atabaki kuwa mbunge wa maisha labda ije neema nyingne na pia katika ile nchi Azizi ameshika si jimbo au wilaya bali mkoa mzima wote unasujudu kwake
Anamapapeti kila mtaa ukimzungumzia tu anapata taarifa zako. Na ni lazima upotezwe kisiasa..
Mimi kama mtoto wa mchungaji nilichokiona ni kama kuna matumizi makubwa yaliyopitiliza ya nguvu za kupuliza kwani utaweza shangaa mwenyewe na hata mleta mada ameshingwa kunyooka haelewi.

Kunawakati Mzee aliingia ghafla kwa kushitukiza pale mjini maeneo ya Msamvu standi alimpiga sana Mbunge na hoja yake hiyo hiyo na safari nyingine alikuwa katika wilaya za mkoa huo alikuwa anampigia huko. kuna siku alikuwa na ziara mkoani hapo cha ajabu alimsifia sana, kwani walimpokea wakampa maji ya kunywa na ya kuonga na chakula, unanielewa.

Juzi akiwa katika uzinduzi wa soko pia alimsifia sana tena sana na yale mapokezi yalijulikana kuwa ya siku moja tu sasa Mzee akaongeza siku za kukaa pale akiwa jukwaani yaani alibadirisha gia angani sasa hapa sisi watu wa mambo ya roho tunaelewa vizuri kuwa nini kilipungua. Na hiyo siku iliyoongezwa ndiyo iliyo muumiza mbunge kwani haikuwepo katika utaratibu wa kimwili au wa kiroho.
Ndiyo maana kesho yake akawa kama si yeye na kumpiga kama hamjui na kumgalagaza kwa hasira kwani hata yeye mzee anafika wakati haelewi alimsifiaje vile jana kwahiyo anashusha nyingi za uso mpaka shoo ya mbele uwezi kuitambua.

Wapendwa katika imani ipo haja ya kuiombea nchi ya Morogoro kwa ujumla hasa pale mjini kwani wale watu wa pale hawafanani na watanzania wengine kwa imani kuwa maiti zao zitaozea ndani kama Mhs. hakuleta masaada wa magali yake kwenda kuzika na hii pale inachukuliwa kuwa ni fadhila kubwa kuzidi chochote kilichofanywa hata kabla ya uumbaji na kuwa Mungu ndiyo amemleta Mbunge kwa kazi hiyo ya kuwazika.
Angalia Msh. Rais jinsi alivyo piga; anasema huyu jamaa ameuwa viwanda na wanamoro wamekosa kazi na pesa mwishowe wana kufa na yeye anawazika tu.
 
Kwani bila kutoa mabasi kwenda kuzika,
Wafu wasingezikwa?
Uchaguzi uliopita wananchi hawakumcagua Abood,Devota Minia ndiye alichaguliwa na wananchi wa Jimbo la Morogoro mjini
Ndiyo Ukweli Wenyewe
Huyu Abood Hakuchaguliwa Ni Ujanjaujanja Mwingi
 
Sishauri hilo, Afande kwa sasa kimsingi hana nguvu kivile, uliona 2015 alipokuwa ACT.
Hakuna anayempenda Abood acha uwongo, nadhani wewe ni chawa wake amekutuma. Ubunge anapata kwa kuiba kura na wala siyo kwa kupendwa na watu. Hata mbinu zake za kumteka Devota Minja ili apite bila kupingwa zilibuma vibaya sana. Hivi umeona wapi mbunge hata barabara ya kwenda ofisini na nyumbani kwake imemshinda na imejaa mashimo? Barabara ya kwenda chuo cha VETA Kihonda imemshinda kabisa. Yaani JPM kamuweza kweli kweli hafai hafai apishe wengine yeye aendelee na Bus zake maana viwanda hawezi bora wamempora.
 
Ukiona watu wanapata shida, waangalie pita zako tu, wanayataka wenyewe, sasa hao wanashangilia na kumkubali mtu anayetoa magari kwenda kuzika ndugu zao ila amechukua viwanda amekopa pesa na kununua mabasi. ila ameacha viwanda ambavyo vingewapa hao wananchi pesa.
Na asikudanganye mtu hivi Bus moja au mawili makuu kuu yanaweza kuzika wakazi wa manispaa nzima ambao wanakufa daily?? Sijaona hata akihamasisha ujenzi wa vituo vya afya, mfano Kihonda nzima hakuna kituo cha afya, watu inabidi waende mafiga hukooo... Haya ameshindwa hata kushirikisha wananchi kuamua stend mpya ya daladala iwe wapi matokeo yake wameihamishia porini huko Mafiga.

Yaani kama unaenda hospitali ya mkoa uende kushukia huko mafiga halafu upande bodaboda au bajaji kuja mjini tena. Ameshindwa kuchukua mawazo ya wananchi ili angalau stendi ihamie pale Fire (wawahamishe wauza mbao wote pale) waende huko Mafiga.
 
Hakuna kitu kama hicho, hilo Bus linazika watu manispaa nzima mkuu? Mamisiba kila siku hicho kibus kitaenda kote huko? Kwanza Bus lenyewe halibebi maiti ni wasindikizaji tuu, lazima mfiwa awe na usafiri wake wa maiti.
 
Back
Top Bottom