Kisiasa, Zitto Kabwe yupo wapi?

Ni vigumu sana kuamini kwamba Zitto Kabwe ambaye wiki chache zilizopita alikuwa mshirika wa Chadema leo ni mshirika wa CCM. Nadhani maneno yangu hayatakuwa na nguvu kama hii picha. Najiuliza maswali mengi kama watanzania wengine, ila majibu sipati.

Zitto atawaambia nini watanzania kuanzia sasa? Hata watatetezi wake wanamchukuliaje?

Mwenye majibu atuambie kwamba Zitto Kabwe ni mpinzani au ni mtu wa haina gani maana kisiasa hajawahi kuaminika.

Zitto hana cha kuwambia Watanzania, hilo ndiyo jibu lako. Sasa hivi anawinda political asylum Canada.
 
Siamini kama Zitto amehusika au amependelea suala la ACT kujiunga na Serikali ya Kitaifa kule Zanzibar!!

Mistake aliyofanya Zitto ni kumkaribisha Maalim Seif ndani ya ACT ambae nae alikuja na Wafuasi wake!!

Wafuasi wa Seif kutoka CUF walikuwa wengi na more influential kule Zanzibar kuliko Wafuasi wa ACT Asili!!

Matokeo yake, Zitto na ACT Asili hawana ubavu wa kufurukuta kule Zanzibar mbele ya ACT Makirikiri, kwahiyo akina Zitto watake au wasitake, lazima wataburuzwa tu na ACT Zanzibar!!

Na hii ndiyo sababu inayonifanya nisiamini ikiwa kweli Maalim Seif aliomba kujiunga CHADEMA kwa sababu kwavile CHADEMA ilishakuwa strong, asingeweza kuiburuza kama anavyoweza kuiburuza ACT kadri atakavyo!! CHADEMA tayari ilishakuwa na misingi imara ya uongozi na viongozi wake walikuwa very influential unlike ACT ambayo ilikuwa ukimtoa Zitto, hamna kinachobaki!!!

Ambacho alifanya Maalim Seif ni kama alichokuwa amefanya Mrema alipoondoka NCCR!!! Ingawaje wakati ule CUF ilikuwa na nguvu lakini ali-opt kenda TLP kwa sababu alijua angewaburuza atakavyo, na kwali, hadi kesho anaendelea kuwaburuza, fursa ambayo pale CUF asingeipata!!!
Good argument,the best JF argument of the month.
 
Back
Top Bottom