Nimesema CHADEMA ina influence Zanzibar au nimesemaCHADEMA ina influential gani Zanzibar ?
Zanzibar wana maamuzi yao hata wangekuwa CHADEMA, hakuna wa kuwazuia kufanya yao.
Ishtoshe Mbowe hana utakatifu huo wa kukataa nafasi kama hizo labda kama umezaliwa jana.
CHADEMA ilishakuwa strong, asingeweza kuiburuza kama anavyoweza kuiburuza ACT kadri atakavyo!! CHADEMA tayari ilishakuwa na misingi imara ya uongozi na viongozi wake walikuwa very influential unlike ACT ambayo ilikuwa ukimtoa Zitto, hamna kinachobaki!!!
NI kwamba huoni, ama sometimes huwa unapata taabu kusoma kwa usahihi au huelewi?!
Kwamba eti Zanzibar wana maamuzi yao, hivi unajua unachokiongea kweli wewe?!
Ina maana chama kimoja kinakuwa na katiba mbili, inayo-operate Bara na Zanzibar hata useme wana maamuzi yao?!
Au ukumbushwe kama kujuzwa kwa mara ya kwanza kwamba Maalim Seif alipoingia ACT, aliingia na kundi lake, na wengi wao wakalamba uongozi ACT na kuwa kwenye kamati mbalimbali za maamuzi?! Hivi kwa akili yako opportunity kama hiyo pale CHADEMA wangeipata kirahisi wakati tayari chama kilishakuwa na uongozi wake top down?
Na suala la Mbowe linatoka wapi? Kwamba "oh, hana utakatifu huo", nani amezungumzia utakatifu au ubora wa Mbowe hapa?! Ameingijiaje ingiaje?!