Kishindo Mkutano Mkuu CHADEMA ; Mabalozi na Taasisi za Kimataifa wathibitisha kushiriki!

Itakuwa historia.Ndivyo tunavyoweza kusema kwani mkutano mkuu wa CHADEMA Desemba 18 utahudhuriwa na taasisi na mashirika makubwa ya ndani na nje ya nchi pengine kwa mara ya kwanza katika historia ya mikutano mikuu ya vyama.

Chanzo kimoja cha Taarifa kutoka ndani ya chama hicho chenye wanachama milioni 6 ni kwamba tayari mabalozi 14 wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wamethibitisha kushiriki mkutano huo wakiwemo mabalozi wa mataifa makubwa duniani.

Pia inadaiwa Taasisi na mashirika mbalimbali zaidi ya 19 tayari yamethibitisha kushiriki katika mkutano mkuu huo ambao umekuwa gumzo ndani na nje ya nchi kwa Takribani mwezi mmoja sasa.Mojawapo ya Taasisi kubwa duniani inayotarajiwa kutuma wawakilishi wake ni Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International

Pia wanazuoni,viongozi wa dini,wafanyabiashara wakubwa,vyama vya siasa na watu kadhaa mashuhuri wamepewa mialiko kuhudhuria mkutano mkuu huo.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe anatarajiwa kulihutubia Taifa kupitia mkutano mkuu katika hotuba inayotarajiwa kuchukua saa mbili.Katika hotuba hiyo Mbowe anatarajiwa kuhitimisha utawala wake wa miaka mitano na kutoa mwelekeo wa chama hicho kwa miaka ijayo.

Katika kuelekea mkutano mkuu wa Desemba 18 ulinzi umeimarishwa katika maeneo yote ya Mlimani City ulipo ukumbi utakaotumika huku askari waliovalia kiraia na wenye sare wakionekana kurandaranda wakiwemo vijana wa ulinzi wa chama hicho Red Brigade.

Kabla ya Mkutano Mkuu Jumatano Desemba 18 siku ya Jumatatu Kamati Kuu ya Chama hicho itakutana hapo hapo Mlimani City huku Baraza Kuu likikutana siku ya Jumanne ikiwa ni siku moja kabla ya Mkutano Mkuu.Vikao hivi vya Kamati Kuu na Baraza kuu vitapitisha majina ya wagombea nafasi za Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

HUKU KUNAITWA KUUPAMBA UCHAFU
 
Asante sana kwa kuuona ukweli
Kwa Chadema hii ni ''missed opportunity''. Fursa ilijitokeza wameshindwa kuitumia
Ilikuwa ni muda mzuri wa kuonyesha kutamalaki kwa Demokrasia.

Baada ya mgogoro wa muda mrefu wa NCCR,James Mbatia aliitisha uchaguzi ulioonyeshwa 'live'
Taratibu nzima za uchaguzi zilikidhi viwango kiasi kwamba NCCR ilikuwa mfano wa kuigwa.

Kwa yaliojitokeza Chadema, sitegemei jipya!

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Kwanini mnafanyia mkutano maeneo ya kifahari ili hali wapiga kura wenu ni maskini

Inaboa sana kwa kweli
watanzania siyo maskini kivile maana umasikini wao hautokani na chama cha siasa bali mipango na utendaji wa serikali yao kufuatana na umuhimu wa vipau mbele vyake!!!!!!!!!!!!!
 
Kwa Chadema hii ni ''missed opportunity''. Fursa ilijitokeza wameshindwa kuitumia
Ilikuwa ni muda mzuri wa kuonyesha kutamalaki kwa Demokrasia.

Baada ya mgogoro wa muda mrefu wa NCCR,James Mbatia aliitisha uchaguzi ulioonyeshwa 'live'
Taratibu nzima za uchaguzi zilikidhi viwango kiasi kwamba NCCR ilikuwa mfano wa kuigwa.

Kwa yaliojitokeza Chadema, sitegemei jipya!

JokaKuu Pascal Mayalla

..mkutano wa bawacha.



..ratiba ya vikao vitakavyopelekea kupatikana kwa viongozi wa kitaifa wa cdm.

 
..mkutano wa bawacha.
..ratiba ya vikao vitakavyopelekea kupatikana kwa viongozi wa kitaifa wa cdm.
Mkuu hayo yanayoendelea ni ya kuwataki kheri
Kuna kitu kimoja kimetia doa sana suala zima na ndiyo maana nikasema hiyo ni ''missed opportunity''. Uchaguzi mzima umegubikwa na mambo yasiyo na majibu kwa wanaofuatilia

SUMAYE;
Niweke wazi kwamba ameshindwa uchaguzi katika sanduku la kura.

Hata hivyo kushindwa kwake kuna acha maswali mengi sana kwa kuangalia historia ya CDM
Imesemwa mara nyingi ukitaka kukutana na mkono wa chuma, zungumzia uenyekiti

Hayo yaionekana kama maneno na uzushi, lakini kwa hali ilivyo kuna sababu za kujiuliza.

Sumaye alijiunga na CDM kama akina Lowassa. Tofauti na wenzake yeye alianza siasa za chama ngazi za mitaani. CCM walimtania kuwa alicheza ''ligi za mchangani''

Hii ni baada ya kuwa mwenyekiti wa kanda ya Pwani.
Katika kipindi chote hatuskusikia malalamiko kuhusu uongozi wake katika kanda hiyo.

Sumaye akachukua fomu za kuwania uenyekiti wa kanda.
Alikuwa mgombea peke, na bila shaka wanachama wengine waliona ni maji marefu.
Hakuna aliyejitokeza kupambana naye

Katika kura Sumaye akashindwa na kivuli.
Yaani akashindwa kuchaguliwa licha ya kuwa m/kiti wa kanda na mgombea pekee.

Halikutokea kwa bahati mbaya, kulikuwa na sababu na mikono ya watu nyuma yake

Hilo ni baada ya kuchukua fomu za Uenyekiti wa Taifa.

Kwa dhalili aliyokumbana nayo, akajitoa katika chama. Ukimsikiliza Prof Safari kwa umakini kuna kitu kinachozungumziwa.

Ule ushindani uliotarajiwa na ambao ungekijenga chama chao, kukifanya kiwe tofauti umekufa.

Swali la kujiuliza, kampeni ya kumwangusha Sumaye imefanywa na nani na kwa lengo gani?
Narudia tena hilo halikutokea kwa bahati, ilikuwa ni ''calculated move''

Pili, Mwenyekiti Mbowe akiwa na miaka takribani 15 hakuwa na sababu za kuanza kampeni kwa kutumia kundi la ''mwaba tuvushe''. Alitakiwa achukue fomu kawaida ili kuleta uwanja sawa

Haya ni maoni yangu, lakini nasimama nayo kwa kusema ''kuna kitu hakipo sawa''

Pascal Mayalla
 
Back
Top Bottom