Kisbo imepitwa hapa mapema tu!

Sexer

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2014
Posts
8,505
Reaction score
8,256
Jamani nilishauriwa humuhumu JF ili nifike Dar kutoka Mwanza kwa siku moja nipande basi la Kisbo, wanaJF wakasisitiza hakuna basi linalokimbia kama Kisbo, nami kweli nikakata tiketi ya hilo basi.

Sasa ajabu leo tumetoka Nyegezi stand tumevuka tu Buhongwa Kisbo ikapitwa basi fulani linaitwa Master, sasa nimeanza kupata wasiwasi kama kweli nitafika leo manake uongo umeanza kudhihirika.
 
Huyo jamaa aliyeipita kisbo hapo buhongwa, kwa uzoefu wangu, hata toboa shinyanga bila ya kukutwa na kupitwa.
Uzuri wa kisbo hailali kituoni, kula ni dk 4 hadi 5, ukizembea utaachwa. Kuns kamsemo chao wale madereva na mautingo "kisbo haimuachi abiria, bali abilia ndo anaiacha kisbo"
 
Kisbo inatoboa,
 
mwanza wanakaa kabila gani, wasukuma?!
 
Mfate dereva MPE 10 ya maji hakika utaona matokeo yake. Kwenye speed 30 anaweka 80.SAA 12:01 jion utakuwa dar
 
Mkuu kama utasikia mabasi yote ya nwanza yamelala Moro isipokuwa gari moja, basi hiyo gari moja itakuwa Kisbo. Wewe tulia mtoke shinyanga hakuna uchwara itawaona hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…