KISARAWE: Mkurugenzi awataka watumishi wote kuhamia wilayani

balibabambonahi

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
15,383
13,773
Mkurugenzi amewatwanga barua wakuu wa Idara zote za serikali wahakikishe watumishi wote wanahamia Wilayani Kisarawe ndani ya siku kumi na nne(14). Atakayekaidi kuchukuliwa hatua kali. Hii inahusisha kada zote za waajiriwa wa serikali.

Nimeongea na mdau wangu Mkuu wa Shule moja anasema yeye ana walimu 45 ila nyumba za walimu zipo mbili hajui watafanyaje. Agizo limeleta taharuki kwa sababu Kisarawe hakuna hata nyumba za kupanga nyingi na watumishi wengine walijenga Pugu, sasa wataacha familia na nyumba wakapange upya?

Na hata kama kuna maeneo zipo zoezi la kushtukiza, watumishi watapata wapi hela za pango?
 
Mazee una miaka mingapi?

Kisarawe mbona wilaya kongwe hiyo, kwa miji mikubwa kama New York, Tokyo na London ingekuwa kiunga cha Dar tu.

Ukipita Pugu Sekondari tu unaingia Kisarawe.
Hapana nimezoea wilaya Mpaya kama Wanging'ombe , Mkalama au Uyui, Mkinga ndio watu wanalazimishwa kuhamia wilayani sasa wilaya Kisarawe ya umri mkubwa watu hawaishi
 
DED naye anatafuta kiki huyo!! Sasa kama mimi kazi zangu ziko kwenye Kata kama afisa mifugo niende wilayani kufanya nini? Mimi naishi Ukonga na kazini nawahi kama kawaida, siku zingine siendi naenda kwenye mishe zangu!!
 
Mkurugenzi amewatwanga barua wakuu wa Idara zote za serikali wahakikishe watumishi wote wanahamia Wilayani Kisarawe ndani ya siku kumi na nne(14). Atakayekaidi kuchukuliwa hatua kali. Hii inahusisha kada zote za waajiriwa wa serikali.

Nimeongea na mdau wangu Mkuu wa Shule moja anasema yeye ana walimu 45 ila nyumba za walimu zipo mbili hajui watafanyaje. Agizo limeleta taharuki kwa sababu Kisarawe hakuna hata nyumba za kupanga nyingi na watumishi wengine walijenga Pugu, sasa wataacha familia na nyumba wakapange upya?

Na hata kama kuna maeneo zipo zoezi la kushtukiza, watumishi watapata wapi hela za pango?

nyumba za kutosha wilayani,pia inshu si kukaa wilayani inshu ni saa moja na nusu uwe ofisini.zamani ukipewa nyumba na serikali unailipa kodi ya nyumba serikali naona mpango huo umekufa.
sidhani km kwenye mkataba wa ajira suala la kupewa makazoi lipo.
kisarawe ni wilaya km si ya kwanza basi ni kati ya wilaya 10 za mwanzo tanganyika,ianzishwa na mjerumani sambamba na kiwanda cha kaolini miaka ya mwisho ya 1890s na miaka ya mwanzo ya 1900s.
kinachofanya wafanyakazi wasiende kuishi kule ni karibu na dar ambapo njia ya kisarawe mjini kwenda dar ni lami na pugu kwenda kisarawe km dk kumi mpaka 20 kwa gari.
foleni au uzembe wa kuwahi kuamka unawafanya wafanyakazi kuchelewa.mfano unaweza kuta kuanzia saa mbili kasorobo hadi tatu ndo majority wanashuka stendi kwenda kazini. japo wapo wanao wahi.
 
Waache uzezeta shughulika na taratibu za kazi na sio mtumishi anaishi wapi! Waache kuingilia maisha binafsi ya watu.Anachotakiwa mtumishi ni kufika kazini kwa wakati na kuondoka kwa wakati.mbane mtumishi kwa hilo na si vinginevyo.
 
Back
Top Bottom