Rais amefanya ziara Kisarawe na kuzindua Mradi mkubwa wa Maji Wilayani humo

Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
49,016
54,299
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania, Leo Atafanya Ziara Wilayani Kisarawe Kuzindua Mradi Mkubwa Wa Maji. Ambao Utawanufaisha Wakazi Wa Kisarawe Hadi Maeneo Ya Ukonga, Pugu

Bila Shaka Tutaaambiwa Mapya Mengi Kuhusu Maendeleo Ya Nchi Yetu. Pia Wakazi Wa Pembezoni Mwa Barabara Atakayopita Wategemee Neema, Hata Mradi Hautapita Kijiji Chochote Bila Wananchi Kupata Maji

Chanzo Cha Taarifa, TBC
===

Katika tukio hilo la ukaguzi wa Mradi wa maji Wilayani Kisarawe Rais Magufuli alifika sehemu ya uzinduzi ili kupata malelezo ya kina ya mtaalamu ili kujua namna mradi huu utakavyofanya kazi na maeneo mbalimbali ambayo mradi huo utahudumu.

Aidha, baada ya kupokea maelezo hayo Rais Magufuli moja kwa moja amelekea katika kuzindua rasmi mradi huo ikiwa pamoja na kujaribu namna maji yanavyotoka katika mradi huo.

Mwisho, Rais Magufuli alipiga picha ya pamoja na na viongozi na Wakandarasi wa mradi huo na kuondoka kuelekea uwanja wa Mkutano.

Mkutano huu umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwamo Mawaziri wa Sekta mbalimbali, Viongozi wa DAWASA pamoja na viongozi wa Wilaya ya Kisarawe.

Hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jaffo
Amemshukuru Rais kwa kumpa dhamana ya kuhudumu katika Ofisi yake pamoja na kuwashukuru Wanakisarawe kwa kumpa nafasi kama Mbunge wao.

Zaidi ya hayo, Mh. Jaffo amemshukuru Rais kwa kufanya Uzinduzi wa maji wenye thamani ya shilingi Bilioni 10.6 ambao anaeleza utasaidia kutatua kero ya maji Kisarawe shida iliyokuwapo kwa muda mrefu pamoja na ujenzi wa vituo vya afya na kazi zote kubwa ambazo Rais amezifanya.

Zaidi ya hayo, Mh. Jaffo amewashukuru na kuwasifu Watendaji wa Dawasa kwa jitihada kubwa waliyofanya katika kuhakikisha mradi huo unatimia vizuri.

Zaidi, Viongozi wengine waliopata nafasi ya kuzungumza ni pamoja na Profesa Kabudi na Waziri wa utalii Dr Hamis Kigwangwala ambao wote wamempongeza Rais kwa kazi kubwa na miradi aliyoifanikisha katika eneo la Kisarawe na mikoa ya Pwani.

HOTUBA YA RAIS MAGUFULI
Rais ameanza kwa kuwashukuru Viongozi kwa kumualika katika tukio hili muhimu la Uzinduzi pamoja na Kuwashukuru Wananchi wa Wilaya ya Kisarawe kumchagua mwaka 2015.

Rais Magufuli ameeleza kuwa mnamo tarehe 21 Juni 2017 alipokwenda Mlandizi kuzindua mtambo wa maji wa Ruvu Juu wa kuhudumia Kibaha na Jiji la Dar es Salaam alisema aliona Mradi ule usiishie khudumia Kibaha peke yake bali ufike mpaka Kisarawe kwa sababu aliona kuwa Wilaya hiyo Kongwe yenye Miaka zaidi ya 103 ilistahili kufikiwa na maji.

Aidha, katika hili Rais Magufuli amemshukuru Waziri, Naibu Waziri, Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu na Watendaji wengine wa Dawasa kwa kazi kubwa waliyoifanya kuhakikisha kuwa mradi huo mkubwa unafanikiwa. Kwa hili Rais ametoa rai kuwa Maslahi ya Wafanyakazi wa Dawasa yaangaliwe vizuri kwani hata Mapato yameongezeka.

Aidha, Rais amemsifu Mh. Jafo kwa juhudi alizozifanya kuhakikisha pesa ya mradi huo inapatikana kwani anaeleza wakati anaahidi jambo hilo bado alikuwa hajapata pesa hizo.

Zaidi ya hayo, Rais Magufuli amewapongeza Wana Kisarawe wote kwa mradi huu pamoja na kuzidi kuwa pongeza Dawasa kwa kujiongeza na kuufikisha mradi huo mpaka Pugu mahali ambapo Baba wa Taifa anahistoria napo.

Aidha, Rais Magufuli ameelaza kuwa moja ya ahadi kubwa walizozitioa kwenye ilani ya uchaguzi ilikuwa ni kuboresha miradi ya maji Mijini na Vijijini anafarijika kuona kuwa wametekeleza miradi hiyo kwa vitendo katika sehemu mbalimbali nchini yenye thamani ya Trilioni 3.

Akifafanuza zadi suala hili, Rais Magufuli amesema "Tumeweza kutekeleza miradi mbalimbali ya maji nchini yanye thamani zaidi ya trilioni 3, hii imefanya upatikanaji wa maji safi na salama uongezeke kutoka asilimia 47% ya mwaka 2015 kwa Vijijini na kufikia asilimia 70.1 kwa mwaka huu lakini pia Mijini kutoka asilimia 74% mpaka asilimia 84% kwa sasa."

Rais Magufuli anaeleza kuwa katika kipindi cha Miaka mitano wametekeleza miradi mbalimbali katika mkoa wa Pwani ambayo kwa ujumla wake ni miradi 45.

Zaidi ya hayo, Rais Magufuli ameeleza kuwa ukiacha mradi huu wa maji walioutekeleza katika Mkoa huu pia wametekeleza miradi mingine mingi ya Afya, umeme na barabara. Mathalani, katika mradi wa Afya Rais Magufuli ameeleza kuwa katika miaka 5 iliyopita wameleta takribani bilioni 12.8 kwa ajili ya kujenga na kukarabati hospitali za Wilaya tano na vituo vya afya 18 vikiwamo vinne vilivyopo katika wilaya hii ya Kisarawe pamoja na magari ya Wagonjwa 12 na kufanya Mkoa wa Pwani kuwa na magari ya Wagonjwa 36.

Sambamba na hilo, Rais Magufuli ameeleza kuwa Wameongeza idadi ya Watumishi wa afya na kuongeza dawa na kufanya upatikanaji wake uongezeke na kufikia asilimia 96%.

Katika sekta ya Elimu Rais Magufuli ameeleza juhudi mbalimbali ambazo Serikali yake imezifanya kuhakikisha kuwa elimu inakuwa katika mazingira mazuri. Rais ameeleza kuwa miongoni mwa juhudi hizo ni pamoja na kuwekeza pesa zaidi ya bilioni 30 na kuboresha mbalimbali.

Vilevile, Rais Magufuli ameeleza jitihada za Serikali yake Mkoani pwani katika sekta ya umeme na miundo mbinu mbalimbali ikiwamo kukubali ombi la Mkuu wa Mkoa juu ya ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami.

Rais Magufuli ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka 5 iliyopita Mkoa wa pwani umeongoza kwa kujenga viwanda ambapo umejenge viwanda vipatavyo 797 na hivyo kuufanya mkoa huu kuwa na viwanda 1192 kutoka viwanda 395 vilivyokuwapo mwaka 2016 ambapo kati ya viwanda vilivyopo katika mkoa huu vikubwa ni 69 vya kati ni 88 vidogo ni 216 na vidogo sana ni 819 hivyo wanaongoza Tanzania nzima kwa kujenga viwanda vingi.

Zaidi ya hayo, Rais amewasisitiza Wanakisarawe kuutunza mradi huu ili udumu. Amewaonya kukatakata mabomba chini pamoja na kutokuacha maji yakamwagika hovyo.

Rais Magufuli Amtengua DAS wa Kisarawe na kumteua Mwanana Msumi kuwa DAS mpya
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa DAS wa Kisarawe, Mtela Mwampamba kwa kuwa na tuhuma zisizoenda na kazi yake ikiwemo kutembea na wake za watu. Rais ameeleza kuwa aliisha muonya lakini hakuonyeka.

Katika hili Rais Magufuli amemteua Mwanamama Mwanana Msumi kuwa DAS mpya wa Kisarawe. Awali Mwanana alikuwa Afisa Tawala. Uteuzi huu umetokana na pendekezo alilopewa hapo hapo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Mwisho, Rais Magufuli amewashukuru Wananchi wote waliohudhuria Mkutano huo pamoja na kuvishukuru vikundi vya sanaa na Wasanii wote kwa kumtumbuizia na kumuimbia nyimbo mbalimbali.
 
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania, Leo Atafanya Ziara Wilayani Kisarawe Kuzindua Mradi Mkubwa Wa Maji. Ambao Utawanufaisha Wakazi Wa Kisarawe Hadi Maeneo Ya Ukonga, Pugu

Bila Shaka Tutaaambiwa Mapya Mengi Kuhusu Maendeleo Ya Nchi Yetu
Pia Wakazi Wa Pembezoni Mwa Barabara Atakayopita Wategemee Neema, Hata Mradi Haupita Kijiji Chochote Bila Wananchi Kupata Maji

Chanzo Cha Taarifa, TBC
"Ni aibu kuwa na mkuu wa wilaya ambaye hajaolewa, wewe Jokate umri umeenda uolewe sasa. Nasema uwongo jamanii?"

Jokate: Nitaolewa kutekeleza agizo la Rais Magufuli

Hayo ndiyo mambo ya walamba viatu na mkuu wao. Kwa leo wataegemea huko kwenye ngono ngono.
 
Muda tafadhali binafsi sipenfi kumiss hutba yoyote ya mkulu nyakati hizi Jojo leo anaweza kula shavu anafanya vizuri sana bosslady wa kisarawe
 
Nina Mashamba Kisanga mradi wa maji na Barabara utatusaidia kuboresha kilimo. Kisarawe kuna shida sana ya maji. Hata kuchimba visima ni shida kupata maji au unatumia gharama kubwa sana.
 
"Ni aibu kuwa na mkuu wa wilaya ambaye hajaolewa, wewe Jokate umri umeenda uolewe sasa. Nasema uwongo jamanii?"

Jokate: Nitaolewa kutekeleza agizo la Rais Magufuli

Hayo ndiyo mambo ya walamba viatu na mkuu wao. Kwa leo wataegemea huko kwenye ngono ngono.
Nachelea kuandika haya lakini ndio ukweli kukujibu wewe mpenda kukashifu watu.

Kiongozi Mkuu, aliyejijengea sifa hadi kuaminika na jamii ya ndani na kimataifa, analewa chakari hadi kuanguka na kuumia kifundo cha mguu (siyo kuvunjika), mnajitokeza kumtetea wakati hamkuwepo kwenye tukio, tuwape majina gani!

Si yeye, wala dereva wake, wamejitokeza hadharani kuelezea mkasa wote. Kwa tabia yake, ingekuwa kweli ameshambuliwa, kwa sababu za kisiasa, kama ambavyo mnadai, hakika asingekuwa kimya hadi sasa. Rejea taarifa yake kwa vyombo vya habari kuhusu kushambuliwa Lissu kwa risasi alivyoishutumu Serikali, lakini leo shambulio dhidi yake anakaa kimya!

Hamkisaidii chama kwa kufukua fukua majungu na kuanzisha uzushi wa kashfa dhidi ya Serikali na viongozi wake. Huo ni mtaji hasi wa kisiasa. Wapiga kura, naamini, wanahitaji kusikia Sera na Mikakati ya maendeleo mbadala kuwaondoa katika hali waliyo nayo kwa sasa, kuelekea kwenye neema.

WAKATI NDIO HUU BADILIKENI KIFIKRA NA MITAZAMO, tunapoelekea Uchaguzi Mkuu. Hizo fikra na mawazo yenu waachieni watoto wa chekechea.
 
Haya tusubiri kama Rais hataongea au kugusia niliyoyaandika. Kama unahitaji watu wawe na busara ni vyema ukaanza kumshauri Rais ili sisi tujikite zaidi kujadili busara anazoongea na kutenda. Vinginevyo acha tuelekee naye uelekeo anaofwata.

Kuhusu kujadili mambo ya kujenga tunafanya sana ila kwa kuwa tunampinga Rais kutokana na anayofanya, basi huwezi kuona vile vile. Endelea kusubiri maana baada ya muda mfupi tutakuja hapa kujadili aliyoongea leo ili uone kama tunamsingizia au kumtendea haki?
 
Najua mtajadili atakayoongea kwa sababu ni watu wa matukio tu, na Rais kwa kuelewa akili zenu ndivyo zilivyo, haachi kuwaondoa kwenye reli ya fikra pevu, kwa matamko.

Fumbo mfumbie mjinga ...
 
Nachelea kuandika haya lakini ndio ukweli kukujibu wewe mpenda kukashifu watu.

Kiongozi Mkuu, aliyejijengea sifa hadi kuaminika na jamii ya ndani na kimataifa, analewa chakari hadi kuanguka na kuumia kifundo cha mguu (siyo kuvunjika), mnajitokeza kumtetea wakati hamkuwepo kwenye tukio, tuwape majina gani!

Si yeye, wala dereva wake, wamejitokeza hadharani kuelezea mkasa wote. Kwa tabia yake, ingekuwa kweli ameshambuliwa, kwa sababu za kisiasa, kama ambavyo mnadai, hakika asingekuwa kimya hadi sasa. Rejea taarifa yake kwa vyombo vya habari kuhusu kushambuliwa Lissu kwa risasi alivyoishutumu Serikali, lakini leo shambulio dhidi yake anakaa kimya!

Hamkisaidii chama kwa kufukua fukua majungu na kuanzisha uzushi wa kashfa dhidi ya Serikali na viongozi wake. Huo ni mtaji hasi wa kisiasa. Wapiga kura, naamini, wanahitaji kusikia Sera na Mikakati ya maendeleo mbadala kuwaondoa katika hali waliyo nayo kwa sasa, kuelekea kwenye neema.

WAKATI NDIO HUU BADILIKENI KIFIKRA NA MITAZAMO, tunapoelekea Uchaguzi Mkuu. Hizo fikra na mawazo yenu waachieni watoto wa chekechea.
 
Najua mtajadili atakayoongea kwa sababu ni watu wa matukio tu, na Rais kwa kuelewa akili zenu ndivyo zilivyo, haachi kuwaondoa kwenye reli ya fikra pevu, kwa matamko.

Fumbo mfumbie mjinga ...
Magufuli kamwe hawezi kunitoa kwenye reli. Haya nyie mbona hatuoni mkija na mada za kujenga humu? Siku Mbowe akiongea ndiyo mtajua mnapokwamia. Kwa sasa endeleeni kuhoroja.
 
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania, Leo Atafanya Ziara Wilayani Kisarawe Kuzindua Mradi Mkubwa Wa Maji. Ambao Utawanufaisha Wakazi Wa Kisarawe Hadi Maeneo Ya Ukonga, Pugu

Bila Shaka Tutaaambiwa Mapya Mengi Kuhusu Maendeleo Ya Nchi Yetu
Pia Wakazi Wa Pembezoni Mwa Barabara Atakayopita Wategemee Neema, Hata Mradi Hautapita Kijiji Chochote Bila Wananchi Kupata Maji

Chanzo Cha Taarifa, TBC
Kiukweli kuna watu leo, wataangalia matangazo hayo mubashara kwa extra interest sio tuu kushuhudia tukio la rais na uzinduzi, bali pia kumuangazia DC wa Kisarawe, Jokate Mwengelo, hii ni nyota inayongara..

Nani hapendi kuona vitu vizuri?. Utafiti wa kisaikolojia, umebaini macho yakiona vitu vizuri vya kupendeza machoni, moyo unafurahi na kukupa furaha ya kweli, true happiness.

P
 
Back
Top Bottom