Kisa sh. 100 ukatokea bonge la ugomvi

Kisa sh. 100 ukatokea bonge la ugomvi

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,402
Reaction score
1,618
Kiukweli jana nimeamini kuwa kuna mtu unaweza kuonana nae kwa mara ya kwanza na hujawahi kuongea naye ila ukamchukia mpaka basi.

Hii kauli inayotumiwa mitaani "damu hazipatani", ni kitu cha kweli kabisa na si masihala. Ngojeni niwape kisa changu cha jana.

Kuna mahali fulani huwa napenda kula chakula zaidi ya miaka miwili sasa, hiyo sehemu kuna mhudumu mmoja toka nimemuona siku ya kwanza na nilikuwa sijawahi kumuona kabla wala kuongea naye lakini nilijikuta namchukia sana (Mungu anisamehe kwa hili) bila sababu yoyote ile.

Lakini hata siku moja sikuwahi kukuonyesha kuwa ninamchukia, nilikuwa MNAFIKI kwa nje najifanya sina tatizo nae nikifika namsalimia ananipa chakula nakula naondoka.

JANA SASA, nimefika nikahudumiwa na mtu mwingine nikawa namdai sh.100 na yule aliyenihudumia akawa kaondoka amebaki huyo dada nisiyempenda, si nikaenda kudai change yangu.
akajibu : mi sina mia
Mimi; chukua hii sh. 100 unipe mia mbili
Akajibu: we vipi, mi sina change bwana tena hela yenyewe hujanipa mimi
Mimi: omba kwa mfanyabiashara mwenzio pembeni
Akajibu: hela yenyewe sh mia afu unanisumbua sumbua
oohoooo...... nilimtolea maneno machafu naye akaendelea na maneno machafu, yaani yule dada nahisi kabisa kipindi hicho chote naye alikuwa ananichukia sema alikuwa hapati sababu ya kuonyesha hisia zake...

TOKA JANA NIKAGUNDUA, UNAPOSEMA FULAN HUMPENDI TU BILA SABABU JUA HATA YEYE HAKUPENDI, MUNGU ATUSAIDIE KULIONDOA HILI PEPO.
 
Matokeo kidato cha nne yametoka ufaulu upo juu sababu grade A inaanza 75 haya hebu tupe point ya msingi maana sijakusoma bado
 
samahan ndugu inahusika vp na mahusiano, mapenzi na urafiki
 
"pepo"... still can't understand kwa nini kila kitu mnasingizia "pepo"
 
hivi unaanzaje anzaje kumchukia mtu usiemfahamu tena bila sababu.??
 
Kuna point moja tu ya msingi hapa ya kumuomba Muumba wako msamaha kwa kuchukia watu bila sababu,. na hapana shaka watu wa jamii yako uwa ni vilaza coz kwa watu waliostaarabika huwa hata tukikwazwa huwa tunasamehe moja mara sabini.. afu ushauri tu issue zingine unatakiwa kuuuchuna sio kupost thread ambazo haziendani na jukwaa hili, poor you!
 
Kuna point moja tu ya msingi hapa ya kumuomba Muumba wako msamaha kwa kuchukia watu bila sababu,. na hapana shaka watu wa jamii yako uwa ni vilaza coz kwa watu waliostaarabika huwa hata tukikwazwa huwa tunasamehe moja mara sabini.. afu ushauri tu issue zingine unatakiwa kuuuchuna sio kupost thread ambazo haziendani na jukwaa hili, poor you!

Usijifanye unajua sana. Kwani maana ya Mahusiano ni nini? au unafikiri mahusiano ni kukutanisha vikojoleo vyenu tu?
Yaani nimetokea kukuchukia ghafla....aaarrgh
 
Usijifanye unajua sana. Kwani maana ya Mahusiano ni nini? au unafikiri mahusiano ni kukutanisha vikojoleo vyenu tu?
Yaani nimetokea kukuchukia ghafla....aaarrgh
Unaona sasa dhambi ya kuchukia ghafla watu bado unayo kumbe msamaha uliomba pale kwa Mungu ulikuwa wa kinafiki,..May be u have to check your physiological status labda una Mimba!
 
Hiyo ni kweli ipo watu msijifanye hamjawahi kukutana na hali kama hizo, na kama hujawahi mshukuru Mungu, Pia hili ni jukwaa la mahusiano,au mahusiano yapi nyie myajuayo? Mleta mada kapost kuwa yeye amekuwa na mahusiano mabaya na mhudumu pasipo sababu so anajaribu kuelimisha na watu wengine ili wasiwe hivyo.
 
hivi unaanzaje anzaje kumchukia mtu usiemfahamu tena bila sababu.??

Hizo zipo sana! Inatokea tu, sio watu wote mtaendana. Wengine inakuwa ni kwa sababu anafanana na mtu uliyewahi kutofautiana naye, kuna wengine ni ile stereo type eg "watu wafupi ni wakorofi!", hivyo ukikutana na mtu mfupi, unamjaji kwamba ni mkorofi hata kama hajakukosea.

Kwa mfano mimi nikimwona mhaya hata kama hajanikosea namchukia kwanza, nitaifuta tutakapoanza kuongea nikamwona ni wa kawaida.

Au nikimwona mtu kavaa kanzu na kibaraghashia au hijabu, duh! Huyu ni chuki mwanzo mwisho.
 
kwenye bold, una maana gani? kwamba hata mtu akiwa anatafuta ajira akipata atasema ni pepo?? au??
usipende ku-generalize
"kaombewe" Ili Hilo "pepo" la kumchukia binti bila sababu (ilahali huchoki kula "gengeni" kwake) lishindwe...
 
Back
Top Bottom